Living kereth
Member
- Feb 7, 2017
- 69
- 55
Hakika inatakiwa ajitangaze.Tangaza shughuli zako,weka mfano wa kazi zako ktk mitandao ya kijamii kama vile fb,whatssap,jf nk.
Kuhusu suala la mtaji Mkuu kwa kweli sina ila nalifikiria sana hilo jambo ..ila shida kazi ambayo ndo mtaji Wa kuanzia ili nipate kipato sipati za uhakikaPole sana mkuu kuna maswali kadhaaa inakupasa kujiuliza kabla ya kuja kwetu kuomba ushauri. Nakupa assignment jiulize maswali haya then majibu yake yatakupa mwanga mzuri wa kujua wapi pa kuanzia.
1) Umesema umejaribu kujichanganya lakini bado hali ngumu umewahi kujiuliza wale ambao unajichanganya nao wanaweza kuleta effect gani kwenye kazi yako kabla ya kujichanganya nao?
2) Je uzoefu wako na utendaji wako unaridhisha kiasi kwamba ukaaminika kupewa kazi?
3) Vipi kuhusu mtaji? Kumbuka mkono mtupu haulambwi. Kujuana na watu au kujichanganya hakutoshi ww kupata tender ni lazima uingie gharama tofauti tofauti kama kujitangaza n.k.
Naomba nisikuchoshe hayo yanatosha kwa sasa ukija na majibu. Tunaweza kujua wapi kwa kuanzia kukushauri ama kukupa tender kabisa.
Mkuu nashukuru sana kwa maelekezo haya maana umenifumbua macho na kunipa mwanga nilikuwa sina hii idea kwa kuwa nimeipata na hii link ninafuata maelekezoHakika inatakiwa ajitangaze.
Aitumie vyema JF na mafanikio atayaona.
My Take
- Tumia muda mwingi kuanzia sasa kuanda mistari michache ya tangazo lako ambayo itabebe fani zako.
- Tumia ukurasa huu: Matangazo madogo kuweka hilo tangazo lako.
- Ili kupa mwanga zaidi wa nini unatakiwa ukiandike basi pitia hapa: MWONGOZO: Zingatia haya unapoweka tangazo lako! - JamiiForums
- Hakikisha tangazo lako linakuwa na picha za kutosha kwa baadhi ya kazi ulizofanya.
- Kuwa na namba ya simu maalum kwa ajiri ya kazi na hakikisha inapatikana muda wote hewani ( muhimu) ikiwezwekana nunua simu ya pili hizi ndogo mfano nokia tochi ambazo chaji yake hukaa muda mrefu hivyo kukufanya uweze kupatikana muda wote.
- Kuwa na ahadi za kweli, kuwa muwazi, Tanguliza kazi mbele na mengine yatafuta.
- Hakika ukiitumia vyema JF utapata kazi nyingi na utaweza safiri toka sehemu moja kwenda nyingine kufanya kazi.
KILA LAKHERI NDUGU, Living kereth NINA HAKIKA UTAFANIKIWA SABABU UMEKUJA JF SEHEMU SAHIHI.