Simulizi : Endless Love

Kwanini wahenga waliweza kuishi na wake zaidi ya mmoja na wakaelewana kwa muda mrefu? Walifundwa.

Pitia uzi kwa kubofya hapo chini ujifunde kwa kina na upana zaidi kuhusu wanawake / wanaume 👇🏾

 
*****************************************
Simulizi : Endless Love
1 portion.

Ilikua ni jumatatu tulivu,upepo mwanana ukivuma na wingu jepesi likichukua nafasi yake. Kwa wakati huo wa saa 10 alfajiri watu wengi katika jiji la Dar es salaam walikua bado wapo usingizini isipokua kwa wanafunzi wanaosoma shule za mbali walikua wamekwishaamka ili kuwahi adha ya usafiri na foleni ndani ya jiji hili. Pia baadhi ya wafanyakazi walikua wapo macho wakijiandaa kuelekea kwenye majukumu yao ya kila siku yanayowawezesha kupata chochote ilimradi mkono uende kinywani.

Sekunde na dakika zilizidi kusogea na hatimaye ikatimia saa 12 asubuhi. Kijana Ally anaamka kutoka usingizini baada ya kushtuliwa na sauti kubwa ya alarm iliyokua inaita kwenye simu yake..Haraka haraka akainuka kutoka kitandani na kuchukua mswaki wake na kwenda kusafisha kinywa.Baada ya hapo akaingia bafuni kuoga na kumaliza haja zake zote.

Akatoka akiwa anaonekana kua ni mtu mwenye haraka sana na kitu fulani.Haraka haraka akajiandaa na kuvaa nguo zake nadhifu na kumaliza kwa kujipulizia perfume yenye manuka to mazuri.Hakika alionekana kupendeza pengine kuliko siku zote za maisha yake...

Akachukua simu yake na kuanza kuangalia notifications mbalimbali za marafiki zake.Akazijibu zote na baada ya hapo akaingia upande wa message na kukuta message mbili,moja ilikua ya rafiki yake aliyesoma nae secondary school aitwaye Saleh Mwaya na nyengine ya dada yake wa hiyari aliyekutana nae facebook aitwaye Diana.

Akawajibu wote na baada ya hapo akalog out. Akafungua WhatsApp akakuta message tatu za marafiki zake Abdallah Bin Kleb, Salum Kuziwa na rafiki yake wa dhati kabisa ambaye walikua ni kama ndugu,Tobby Aguriz. Wote walikua wanamtakia masomo mema pamoja na kumtumia picha zenye maneno mazuri hiyo yote ilikua ni kuonyesha upendo wa dhati kwa rafiki yao..Ally alifurahi sana na akawajibu wote kwa kuwashukuru kwa kumjali katika siku zote za maisha yake.

Ally alikua amejiunga na chuo cha Tanzania Institute of Accountancy (TIA) campus ya Dar es salaam kilichopo maeneo ya Kurasini katika viunga vya barabara ya Kilwa na Mandela akiwa anachukua Diploma in Accountancy (DA) na hiyo ndiyo ilikua siku yake ya kwanza ambayo alikua anaenda kuripoti chuoni..Akatoka sebuleni ambapo alikutana na mfanyakazi wao wa ndani akiwa busy kwa kufanya usafi wa ndani..

Mambo Sarah...ilikua ni sauti ya Ally akimsalimia mfanyakazi wao wa ndani...

Poa tu umeamkaje?

Sarah akamjibu huku akionekana kua na uso wenye tabasamu na bashasha la aina yake.

Namshukuru Mungu niko fresh kabisa,hofu kwako..

Mmhhh me mzima wa afya.

Sarah aliendelea kujibu..

Sawa! Vipi breakfast tayari umekwishaandaa?

Ndio tayari ipo mezani..

Basi sawa nashukuru.

Ally alijibu huku akielekea

dining room kwa ajili ya kupata kifungua kinywa...

Baada ya kama dakika tano mzee Mohammed Kirumbi, baba mzazi wa Ally alitoka chumbani kwake na kuelekea kupata kifungua kinywa pamoja na mwanae..

Good morning dady! (Habari za asubuhi baba)

Good morning son, how are you?(Nzuri

mwanangu,unaendeleaje?)

I'm fine!(Sijambo).

Hayo ndio yalikua mazoea ya mzee Mohammed pamoja na mwanae,.ndio salamu yao kila inapoanza siku mpya...

Wakamaliza kupata breakfast na wote wawili walikua wapo tayari kwa ajili ya kuondoka.

Ooh!sorry, I've forgotten my key. (Ooh!samahani nimesahau funguo yangu)

Mzee Mohammed alimwambia mwanaye huku akitoka nje kuelekea alikopaki gari yake aina ya Verrosa.

Where? (Wapi?)...

Ally akauliza.

On my dressing table. (kwenye dressing table yangu)

Okay I'm coming. (Sawa nakuja baba)

Ally alijibu huku haraka akirudi ndani kwenda kuchukua ufunguo wa gari..

Aliingia mpaka chumbani kwa baba yake na moja kwa moja akaelekea kwenye dressing table ili akachukue ufunguo..Baada ya kuupata wakati anaondoka kuna kitu alikiona hadi akahisi moyo wake ukimpasuka..

Akakisogelea hiko kitu huku akionyesha kuwa na uso wenye huzuni.Ilikua ni picha ya marehemu mama yake Bi. Amina Ally aliyefariki dunia miaka 14 iliyopita wakati huo Ally akiwa na umri wa miaka 7 tu. Kwa hakika hakuyafaidi sana mapenzi ya mama kama ilivyokua kwa baba na hiko kilikua ni kitu kinachomuumiza sana na kumkosesha raha haswa anapoiona picha ya mama yake kipenzi... Alikumbuka maneno aliyoambiwa na mama yake wakati anaanza darasa la kwanza katika shule ya msingi Wailes iliyopo Temeke, "Mwanangu kuwa makini sana katika masomo yako, usihadaike kabisa na

haya maisha mazuri ya hapa nyumbani. Kilichokua cha wazazi wako kitabaki kuwa cha wazazi wako. Inabidi usome kwa bidii ili utafute kilichokua cha kwako".. Ni maneno yaliyoingia vizuri akilini mwake na kuishi kwa takribani miaka 14..Aliichukua picha ya mama yake na kuibusu..

Ghafla akasikia sauti ya baba yake ikiita kutokea nje.

"We Ally unafanya nini ndani muda wote huo? Hebu toka haraka tuwahi kuondoka.

Haraka Ally aliirudisha ile picha kama ilivyokua kisha akatoa leso na kujifuta

machozi ambayo yalikua yameanza kutanda kwenye mboni za macho yake..Akatoka sebuleni akakutana na mfanyakazi ambaye aliiona hali ya

Ally ilivyobadilika usoni.

Vipi Ally mbona upo hivyo?..aliuliza Sarah.

Kwani nipo vipi mbona mimi nipo kawaida tu!..

Alijibu huku akililazimisha tabasamu usoni mwake.

Hapana wewe siyo Ally ninayekujua,lazima

kuna kitu kitakua hakipo sawa tu.

Usijali Sarah me nipo sawa kabisa,acha niwahi nje maana baba ananisubiri muda mrefu.

Aliongea Ally huku akiwa anafungua mlango wa kutokea nje..

Sawa bwana siku njema na masomo mema pia.

Sarah alimwambia Ally huku akiachia tabasamu pana usoni mwake..

Poa nawe pia na nashukuru sana kwa kunijali.

Ally alijibu huku akifunga mlango wa kutokea nje...

Vipi mwanangu mbona umechelewa sana, yani kuchukua funguo tu?

Aliuliza mzee Mohammed.

Samahani baba nilisahau wallet yangu halafu pia nilisahau mahali nilipoiweka.. Alidanganya Ally kwa ajili ya kujitetea.

Kwa hiyo sasa umeiona?

Ndio baba nimeiona.!

Akajibu huku akificha uso wake wa huzuni aliokua nao mwanzo..

Sawa panda kwenye gari tuondoke..

Wote wakaingia kwenye gari na safari ya kuelekea chuo ikaanza..

Safari ya kutoka Temeke hadi chuo cha Uhasibu haikua ndefu sana. Kwa dereva mzuri inaweza kumchukua dakika 10 mpaka 15 kama hakuna foleni..Walifika salama kisha wakaagana na mzee Mohammed akaendelea na safari yake ambapo alikua anaelekea Posta mpya

katika bank ya CRDB tawi la Azikiwe alipoajiriwa kama afisa masoko...

Kwa mwendo wa taratibu Ally alivuka barabara na kulielekea geti kuu la chuo.Aliingia ndani na kukutana na mamia ya wanafunzi wakiwa wamekaa

kwa vikundi vikundi wengine wakijisomea huku wengine wakipiga story..Hakuwa na rafiki hata mmoja chuoni hapo kwani alikua mgeni hivyo hakujua hata

aanzie wapi na aelekee wapi..Akasogea mbele zaidi na kukutana na wasichana watatu wazuri wakiwa wamekaa

wanatazama mahali anapotokea yeye..

"Kaka mambo."

Ilikua ni sauti ya mrembo mmoja kati
ya wale watatu. Alishtuka kidogo kwani hakutegemea kusalimiwa na mtu yeyote mahali pale..

Safi tu mzima wewe? mambo zenu jamani.

Ally alimjibu yule msichana huku pia akiwasalimia wale wenzake aliokaa nao.

Poaa...

Walijibu wale wasichana wengine wawili kwa sauti za madaha.

Me mzima kabisa, unaonekana kuwa

mpya hapa maana tangu unatokea kule nakuona kama mtu unayebahatisha njia.

Aliongea yule msichana wa kwanza kumsalimia Ally huku akionyesha sura ya ukarimu.

Yaah! ndo kwanza naingia leo eneo hili, yani hata application na mambo mengine yote nilifanyiwa na mzazi wangu.

Alijibu Ally huku akionekana kuwa

ni mwenye kujiamini..

Okay! so unachukua kozi gani hapa? aliuliza tena yule msichana.

Diploma in Accountancy.

Akajibu Ally huku akimtizama usoni yule msichana.

Okay! so unalijua darasa lako?

Hapana! yani hapa kusema ukweli hata sijui nianzie wapi.

Ally akajibu huku akitabasamu...

Okay never mind! may I escott you? (Sawa

usijali, naweza nikakusindikiza?)

Okay!I will thank you!(Sawa, nitakushukuru)

Ally alijibu huku akiachia tabasamu pana usoni mwake.

Hey guys,I will be back in ten minutes. (Hey jamani, nitarudi baada ya dakika10)

Yule msichana aliwaaga marafiki zake.

Poa usichelewe basi,,maana wewe huchelewi kuzusha safari nyengine huko huko juu kwa juu.

Aliongea kwa mzaha mmoja kati ya wale wasichana wawili.

I promise you! (Nawaahidi) sitachelewa.

Aliongea yule msichana huku akianza kuondoka na Ally..

Jamani asanteni sana tutaonana mungu akipenda.

Ally aliwaaga wale wasichana

huku akiondoka na yule msichana wa kwanza.

Poa usijali karibu sana.

Walijibu kwa pamoja wale wasichana.

Asante nashukuru sana.

Walianza taratibu safari ya kuelekea darasa analosoma Ally..Njiani waliongea mambo mbalimbali kuhusu pale chuoni huku yule msichana akimuonyesha Ally mazingira ya pale chuoni..Yule msichana alionekana kuwa mkarimu sana kupita maelezo kiasi kwamba mtu yoyote ni rahisi sana kuzoeana nae..

Mara ghafla Ally alimwomba yule msichana wasimame walipofika sehemu moja ambayo kulikua na mti wa mwarobaini...Yule msichana akasimama huku akimtizama Ally usoni bila ya kumwambia kitu chochote.

Napenda kukushukuru sana kwa ukarimu wako ulionionyesha kwa siku ya leo,mimi sina cha kukulipa ila Mungu mwenyewe ndio anajua akulipe nini...aliongea Ally huku akionyesha kuwa ni mtu aliye makini.

Nami nashukuru pia,ila usijali ni kawaida yangu kuwasaidia watu pale ninapoona inawezekana,so nahisi Mungu amepanga leo nikusaidie wewe..

Aliongea yule msichana huku akiwa

anatabasamu. Basi wote kwa pamoja

wakajikuta wanacheka..Meno meupe ya yule msichana yaliyopangiliwa

vizuri yalionekana barabara machoni mwa

Ally..Lips laini zilizopakwa lipshine zilichanua vizuri na kuyafanya mashavu yake kutengeneza vishimo vidogo maarufu kama dimpoz...Macho yake meupe makubwa wastani yalizidi kuupamba uso wa huyu msichana. Pua yake nyembamba ndefu wastani ikazidi kutia ndimu katika uso wake mzuri.

Samahani, ujue tangu tumeonana tumeongea mambo mengi lakini hata majina hatufahamiani.. Sijui mwenzangu unaitwa nani?

Aliuliza Ally huku akiliweka vizuri begi lake

mgongoni..

Naitwa Recho!

Alijibu yule msichana kwa sautia yake laini yenye uwezo wa kumwamshas ingizini mgonjwa aliyelala kwa miaka 10.

Aanha! Recho, nice to meet you. (aanha! Recho, nafurahi kukutana na wewe) Mimi naitwa Ally.

Aliongea huku akiendelea kuachia tabasamu usoni mwake.

Okay! me too, it's my pleasure.(Sawa,mimi pia nafurahi) Halafu unaonyesha kuwa mpole sana.

Aliongea Recho kwa mapozi.

Kidogo tu sio sana.

Alijibu kwa mzaha.

Mm mmh! okay! (Mm mmh! Sawa)

Wakaendelea kutembea hadi walipofika darasa analosoma Ally..Alimshukuru sana Recho kisha wakaagana maana mda wa kuingia darasani ulikua tayari umeshafika...Recho alirudi mpaka kwa rafiki zake na kuanza kuwahadithia kuhusu Ally..

'Yaani nyie acheni tu, yule mkaka ni mpole na mkarimu sana,halafu pia ni. handsome

sana mpaka Recho mimi akili yangu ikasimama kufanya kazi. Halafu anaonekana mcheshi na anajali..Sio siri jamani kiukweli amenivutia"

Aliongea Recho kwa maidoido huku akizungusha macho yake laini..

Mmhhh! wewe tena, haya bwana it's up to you mumy! (Ni juu yako mama)

Aliongea kwa mzaha rafiki yake Recho

anayeitwa Tayana...

Ila una haki ya kupagawa shoga yangu maana yule mkaka mmhhh! hata sijui niongee nini! Nahisi chuo kizima hapa yeye ndo handsome namba moja..akazidi kusifia rafiki yake mwengine Recho anayeitwa Najma.

Waliendelea kumuongelea Ally hadi mmojawapo alipowashitua wenzake..

Hey guys! time (hey!jamani muda) twendeni class.

Aliongea Tayana na wote wakainuka kuelekea darasani.

* **
Saa nane kamili mchana ndio ulikua mda ambao Ally anatoka darasani..Akatoka akiwa ameongozana na kijana mmoja wa rika lake.

Sasa Allan hii assignment inabidi nikaifanye nyumbani then nitakupigia simu tuwe tunashirikiana mpaka tutakapoimaliza, au sio?

Aliuliza Ally.

Fresh hamna noma mwanangu nakuaminia.

Alijibu Allan Stanford, rafiki mpya wa Ally aliyekutana nae chuoni hapo. Wakapeana namba za simu kisha wote wakatoka nje ya chuo na kwenda kusimama kwenye kituo cha mabasi..Allan ndio yalianza kuondoka kisha Ally nae akapanda basi linaloelekea nyumbani kwao Temeke.

** **

Jioni akiwa amekaa sebuleni anaangalia movie akasikia simu yake inaita..kuangalia akakuta rafiki yake Allan ndo anampigia.

Ally...oy!

Allan...Niaje mwanangu?

Ally...kama kawa,nambie

Allan...Mzuka,ile assignment vipi ushaanza kuifanya?

Ally...daah! bado mwanangu,nilikua nimelala yani ndo nimeamka mida hii hii.

Allan...Okay! so inafanyika leo au kesho asubuhi?

Ally...Inafanyika leo, ngoja kuna movie nacheki hapa ikiisha nitakuvutia waya, amanini?

Allan...Baridaa hamna noma mida basi.

Ally...poa.

Akakata simu kisha akaendelea kuangalia ile movie ya action...Mara kidogo mfanyakazi wao Sarah akaja akitokea jikoni.

Yani Ally leo tu kwenda chuo tayari ushapata rafiki?

Aliuliza Sarah kwa mzaha.

Yaah! mimi tena kama unavyonijua kipenzi cha watu nitakosaje rafiki.

Alijibu Ally huku nae akileta mzaha.

Hahahaaa yani wewe! Leo nilikumisije humu ndani? Nshakuzoea muda wote kukuona.

Aliongea Sarah huku akienda kufungua fridge na kummiminia Ally Juisi...

Wow! kitu cha embe, kama umeongea na koo langu vile. Nashukuru sana Sarah... Aliongea Ally na kuanza kuinywa ile juisi...

Poa usijali, mimi nipo hapa kwa ajili ya

kuwahudumia nyie, kwahiyo chochote

utakachokihitaji utaniambia..

Alijibu Sarah huku akitabasamu..

Poa acha mimi niendelee kuangalia hii
movie maana imefika patamu sana..

Poa acha na mimi niende jikoni ili nikamalizie mapishi..Sarah aliongea huku akielekea jikoni...

Baada ya kama dakika kumi na tano Ally alisikia makelele kutoka jikoni Sarah akiomba msaada. Haraka haraka Ally alitoka mbio mpaka jikoni ambako alimkuta Sarah akiwa ameanguka chini huku jiko la umeme likiwaka moto mkubwa na sufuria ya chakula ikiwa ipo pembeni. Akamsogelea Sarah ili ampe msaada. Upande mmoja wa kanga ulikua upo wazi hivyo kuliacha paja lake jeupe likiwa linamtazama Ally.

Mapigo ya moyo ya Ally yalianza kwenda kasi kwani katika maisha yake hakutegemea kuliona hata goti la Sarah kwani muda mwingi anakua amevaa nguo ndefu.

Sarah! Sarah!..Nini kimetokea?

Ally aliuliza huku akiwa ni mwenye wasiwasi sana..

Jiko limelipuka na kuniunguza mkononi.

Sarah alijitahidi kujibu huku akiwa analia kwa maumivu aliyokua anayapata...

Haraka haraka Ally akazima switch ukutani na kumuinua Sarah pale chini alipoanguka... Akamsaidia kutembea kwa kuuzungusha mkono wa kushoto wa Sarah begani kwake..Alimkokota mpaka chumbani kwake na kumlaza

kitandani..Akaenda chumbani kwake kuchukua first aid kit(box la huduma ya kwanza) na kurudi nalo hadi chumbani kwa Sarah.Akampatia Sarah huduma ya kwanza kwani alikua vizuri sana kwenye somo la Biology wakati yupo secondary school kisha alipomaliza akampa na painkillers ili apunguze maumivu. Baada ya hapo akamuuliza anajisikiaje...

Afadhali kidogo tofauti na ilivyokua mwanzo, nashukuru sana Ally kwa msaada wako kwani kama ningekua peke yangu hata sijui ingekuaje.. Alijibu kwa sauti ya chini sana..

Usijali,mimi nipo hapa kwa ajili yako haswa yanapotokea matatizo kama haya..Ally alijibu huku akiendelea kumwambia Sarah manenoe yenye kumfariji. Akamuaga Sarah na kurudi sebuleni kuzima TV na kwenda chumbani kwake ili akafanye assignment waliyopewa chuo yeye na rafiki yake Allan.

Akampigia simu Allan wakajadiliana mambo mbalimbali mpaka wakaimaliza ile assignment. Akiwa anajiandaa kwenda kuoga chooni kwake, ghafla alishtuliwa na hodi iliyopigwa chumbani kwake.

Akaenda kufungua mlango na kukutana uso kwa uso na baba yake..

Good evening dady(habari za jioni baba)

Ally alimsalimia baba yake huku akionyesha kuwa na uso wenye simanzi.

Good evening my son.(nzuri mwanangu)..mbona upo hivyo,kuna tatizo lolote?

Aliuliza mzee Mohammed.

Yes dady(ndio baba) Sarah amelipukiwa na jiko wakati alipokua anapika chakula. Ameungua sana kiganja chake cha mkono.

Yuko wapi?

Aliuliza mzee Mohammed hukuk akionyesha kuwa ni mwenye wasiwasi.

Chumbani kwake amelala.

Ally alijibu huku wote wakianza kuelekea chumbani kwa Sarah.. Wakapiga hodi kisha wakaingia mpaka ndani..Mzee Mohammed alisalimiana na Sarah

kisha akamuuliza hali yake.Sarah alimjibu jinsi anavyojisikia kisha mzee Mohammed akampa pole na kumtia moyo ili afarijike.

Walivyomaliza mzee Mohammed akamtuma mwanae akanunue chakula kwenye restaurant moja maarufu maeneo ya mtoni kwa Azizi Ali kwani ndani hakukua na chakula cha kula kwa usiku huo. Akachukua ufunguo na kuwasha gari la baba yake kisha akaondoka.

** *

Recho alikua amejifungia ndani kwake huku mawazo yake yote yakiwa yapo kwa Ally.Muda mwengine alijikuta mwili

ukimsisimka kila alivyofikiria jinsi ambavyo Ally atakua mwanaume wake na kumruhusu auchezee mwili wake jinsi anavyotaka. Alipata hisia za ajabu mpaka yeye mwenyewe akaanza kujishangaa.

"Kwanini mimi nakua hivi lakini?..Yani mtu niliyemuona

siku moja tu ndio ananifanya nafikiria mambo yote haya!! mmmhhh! Nahisi nampenda kwa dhati Ally.Natamani hata sasa hivi awe boyfriend wangu ili moyo wangu utulie.Lazima nifanye kila mbinu ili nimpate,. Lakini itakua rahisi

kweli?.. Maana kwa jinsi leo nilivyomuanza mimi kumuongelesha na kumfanyia yote yale hata kuniomba namba ya simu? Hapana haiwezekani

kwa wanaume wa sikuizi..Au labda ana girlfriend wake na anamuheshimu?"

Recho alijikuta akiongea maneno yote hayo na kujiuliza maswali ambayo hayakua hata na majibu kwa wakati huo. Mama yake alikuja kumuita ale chakula lakini alikataa kwa kisingizio kuwa ameshiba. Mama yake alilalamika sana lakini hakumsikiliza kabisa.. Kilichokua ndani ya akili yake kwa muda huo ni Ally tu na hakutaka mtu yoyote amuharibie hizo hisia. Aliendelea kuwaza mpaka usingizi ukampitia.

** **

Kesho yake asubuhi na mapema Recho aliamka na kuanza kujiandaa kwa ajili ya kuelekea chuo.Akamaliza na baada ya hapo akaenda kumsalimia na kumuaga mama yake.

Mbona leo mapema sana Recho? Yani hata saa kumi na mbili kamili bado haijafika?

Kuna kazi tuliachiwa jana mimi na kundi

langu kwahiyo bado hatujamaliza ndio tunataka tukamalizie hii asubuhi.

Ilibidi Recho amdanganye mama yake ili asiulizwe maswali mengi zaidi..

Mama yake akamuelewa na baada ya hapo wakaagana na Recho akaelekea chuo.. Alifika chuo mapema sana kuliko kawaida na kukutana na watu wachache sana wakiwa wamekaa vikundi vikundi wakipiga story huku wengine wakionekana kuwa busy kwa kujisomea. Akachukua simu na kuwapigia simu rafiki zake Tayana na Najma ambao wote walisema kuwa wapo njiani..Akatembea zaidi na kuelekea ilipo lecture room ya kina Ally..

Alikaa karibu kabisa na darasa analosoma Ally ili pindi atakapokuja tu amuone.. Alikaa kama nusu saa ndipo alipomuona Ally akitokea huku akiwa anachezea simu yake.Moyo wa Recho ulipasuka kwa woga huku akihisi mwili wake ukimuisha nguvu......

Pumzi zilikua zinamwenda mbio sana Recho kiasi kwamba alikua haamini kile ambacho anataka kukifanya.. Alipoona Ally anakaribia kufika aliinuka pale alipokua amekaa na kuanza kusogea upande ambao alikua anatokea Ally..

Hey! mambo.

Alikua Recho akianza kumsalimia Ally.

Wow! Recho? safi, mzima kabisa?

Yaah! Ndo mimi, mzima kabisa, vipi za tangu jana?

Nzuri,sijui wewe.?

Mmhhh!!

Vipi mbona unaguna, kuna tatizo?

Hapana hakuna tatizo!!

Mmhh! kama hakuna tatizo sawa.

Recho alikua kimya akiwa hajui hata aanzie wapi kumuambia Ally jinsi anavyojisikia kwake.. Akabaki akichezea vidole vyake vya mikono huku akiwa kama anatoa uchafu kwenye kucha..

Nahisi kuna kitu kinakutatiza Recho, tafadhali naomba uniambie labda naweza nikakusaidia hata kwa ushauri tu.

Aliongea Ally huku akimshika bega Recho ambae alikua ameinamisha uso wake chini..

Yaah! ni kweli Ally kuna kitu hakipo sawa kwangu, ila nashindwa hata nianzie wapi

kukuambia. Nahisi kuchanganyikiwa halafu kama sijielewi.

Aliongea Recho huku akiona aibu na kuangalia chini..

Ally alianza kushtuka hali aliyokua nayo

Recho.Alimuangalia sana usoni na kukubali yeye mwenyewe kuwa Recho ni msichana mrembo sana..Lakini kitu kimoja tu ndo kilikua ndani ya moyo
wake, alijiapiza kuwa hatajihusisha kimapenzi na mwanamke yeyote chuoni hapo..Akahisi labda atakua anakisaliti kiapo chake tena mapema sana hata wiki moja hajamaliza..Akamshika Recho mkono kisha akamwambia.

Samahani Recho, kwa mda huu sidhani kama itakua muda muafaka kuniambia hiko kitu kinachokusumbua. Nahisi yanaweza yakawa mazungumzo marefu kidogo yanayohitaji utulivu hivyo kwa muda huu naomba uende class maana imebaki kama robo saa vipindi vianze..

Baada ya kuambiwa hivyo Recho alimwangalia Ally usoni huku akionyesha waziwazi kuwa moyoni mwake ana huzuni..

Sawa Ally nimekuelewa, kwahiyo tutaonana lini tena?

Leo nilikua nina ratiba nyingi sana sidhani kama tutapata muda mzuri wa kuongea. Labda unipe namba yako ya simu tuwe tunawasiliana ili uniambie hilo tatizo lako.

Aliongea Ally huku akitoa mfukoni simu yake. Kwa Recho huo ulikua ni ushindi mkubwa sana. Akaichukua hiyo simu na kuandika namba yake kisha akajibeep.. Alipomaliza wakaagana kisha Ally akaingia class na Recho akaelekea darasani kwake.

***** ***** *****

Jioni ya siku hiyo Recho alikua ni mwenye furaha sana kwa kitendo cha kuongea na Ally na kupata namba yake ya simu.Alikua amekaa chumbani kwake akisubiri labda Ally atampigia. Alikaa mpaka saa 3 ya usiku lakini hakuona hata message ya Ally. Alianza kuingiwa na huzuni na kuhisi labda Ally alikua na girlfriend wake na hataki kabisa kumsaliti..Ilipofika saa nne usiku baada ya kumaliza kula na kufanya kazi zake zote aliamua kumpigia simu Ally. Simu iliita mara ya kwanza hadi ikakata lakini haikupokelewa.

"Mmhhh! kwanini lakini ananifanyia hivi. Yani hata kupokea simu yangu hataki"

Aliongea peke yake huku machozi yakianza kumtoka..Aliwaza sana mpaka aliposhtuliwa na mlio wa simu ilivyokua inaita.. Kuangalia alikua Ally ndiye anayepiga..Moyoni alifurahi sana na furaha yake ikaanza kurejea upya.. Akapokea simu na mazungumzo yao yalikua hivi.

Recho...Hellow!

Ally...Hellow! Mambo vipi?

Recho...Poaa, sijui wewe.

Ally...me nipo fresh kabisa,sorry bado sijakujua nani mwenzangu?

Recho...mmhhh! Ina maana namba yangu haukuisave?

Ally...Yaani mambo mengi halafu ni watu wengi wanaonipa namba zao kwahiyo sijakujua bado.

Recho...mimi Recho!

Ally...ooh! kumbe Recho,samahani sana..Unajua mida ile wakati naingia class nilikua na mambo mengi sana hadi nikasahau kuisave namba yako.

Recho...usijali,vipi uko wapi?

Ally...Nipo home ndio najiandaa kulala, niende wapi sasa hivi.

Recho...Okay!

Ally...Halafu nimekumbuka vipi kuhusu yale mambo uliyotaka kuniambia asubuhi, vipi unaweza kuniambia muda huu?

Recho...Natamani hata nikuambie sasa hivi lakini sidhani kama utanielewa...

Ally...Kwanini sasa nisikuelewe? Kwani mambo yenyewe yana uzito sana?

Recho...Ndiyo Ally yana uzito mkubwa sana kwangu ndio maana sidhani kama utanielewa.

Ally..Mmhh sawa nimekuelewa.Basi tupange siku kama weekend hivi tukutane ili uniambie vizuri hayo mambo yenyewe..

Recho...nashukuru sana kusikia hivyo.

Baada ya hapo walipanga sehemu ambayo watakutana kisha Ally akakata simu...Recho alikua ni mtu mwenye furaha pengine kuliko siku zote za maisha yake..Alichukua mto wake na kuukumbatia kwa nguvu akihisi kuwa Ally ndiye aliyekua pembeni yake.

Ashki zilimpanda sana na kujikuta akianza kuyaminya minya maziwa yake madogo yaliyosimama vizuri..Alishtuliwa na sauti ya mama yake akimuita ili akachukue hela yake ya kwenda chuo kesho..

Baada ya kuchukua Recho alifunga mlango kisha akaamua kulala..

** **

Dakika, masaa na siku zikasogea na hatimaye ikafika siku ya Jumapili..Recho alijiandaa vya kutosha ili akakutane na mwanaume anayempenda kuliko wote. Alitoka nyumbani mida ya saa sita mchana na kuanza kuelekea kwenye fukwe za Sea Cliff.

Alifika maeneo hayo huku akiwa anamsubiri Ally kwa hamu..Mara akasikia message ikiingia kwenye simu yake kuangalia alikua Ally akimuuliza amekaa kwa wapi..Recho alimjibu na baada ya dakika tatu akamuona Ally akija akiwa ametupia mpaka akahisi kama amemfananisha.

Ally akasogea mpaka pale alipokaa Recho kisha wakasalimiana. Recho alimsifia sana Ally kwa jinsi alivyopendeza huku Ally nae akimsifia Recho kwa jinsi alivyomatch mavazi yake kuanzia nguo,viatu mpaka hereni. Waliongea mambo mbalimbali na kufurahi kwa pamoja kiasi kwamba akipita mtu asiyewajua anaweza akadhani labda wamejuana miaka mingi iliyopita..

Vipi mbona hujaagiza kinywaji?

Ally alimuuliza Recho huku akiangalia kama kuna muhudumu aliye karibu..

Nilikua nakusubiri wewe ufike sasa nitakaaje nianze kunywa peke yangu wakati najua kuna mtu anakuja kuwa pamoja na mimi hapa..

Alijibu Recho na sauti yake kama inayotokea puani..

Yaah! ni kweli kabisa.

Walimuita muhudumu kisha wote wakaagiza juisi maana walikua hawatumii kilevi cha aina yoyote..

Muhudumu alirudi na vinywaji kisha akawaribisha na kuondoka.Walibaki kimya kama dakika mbili Recho akiwa hajui hata aanzie wapi kumwambia Ally. Pia aliona labda Ally atamuhisi kuwa ni malaya na hiyo ndiyo ilikua tabia yake kujirahisisha kwa wanaume. Hakuwa na cha kuanza kuongea mpaka Ally alipovunja ukimya..

Eeeh! niambie Recho nini kinakusumbua maana tangu siku ile tulivyoongea pale chuo basi muda mwingi sana huwa nafikiria una tatizo gani mpaka umeamua kunishirikisha na mimi..

Hapana Ally sina tatizo lolote kubwa isipokua....

Recho alishindwa kumalizia akabaki anamtazama Ally kwa macho yake yaliyolegea.

Isipokua nini Recho?

Yani nakosa kabisa ujasiri wa kuongea hata sijui kwa sababu gani..

Ally alimuangalia Recho kwa makini kisha akakumbuka mambo yote aliyofanyiwa na Recho tangu siku ya kwanza walipoonana.

Akakumbuka na ile siku aliyofuatwa nje ya darasa analosoma na jinsi Recho alivyokua anaminya minya vidole vyake na kushindwa kuongea..

"Nahisi atakua ananipenda ndio maana anashindwa kabisa kuongea. Lakini kwanini nisimpe nafasi kuliko kumuacha aendelee kuwa na hali hii?"

Ally alijisemea mwenyewe moyoni kisha akasogeza kiti chake mbele na kumkaribia kabisa Recho.

Recho!

Ally aliita kwa utulivu sana.

Abee!

Kuna kitu nakihisi kutoka kwako lakini sijui kama nitakua sahihi kwa asilimia mia moja.

Kitu gani hiko?

Ally alikohoa kidogo kisha akaendelea.

Nahisi unanipenda kwa dhati kabisa ndio maana unashindwa kabisa kuongea unapokua na mimi.

Recho alibaki kimya asijue hata ajibu nini..Alibaki kama mtu aliyeduwaa huku machozi yakianza kujitengeneza taratibu kwenye mifereji ya mboni za macho yake.

Ally hakuamini alipoona machozi yakitiririka kwenye mashavu laini ya Recho huku kilio cha kwikwi kikianza kusikika kwa mbali..Akahisi labda itakua amemuudhi kwa kumwambia mane no yale..Ikabidi aanze kumuomba msamaha kama itakua amemkosea..

Hapana Ally haujanikosea kitu chochote na wala sifikirii kama kuna siku utanikosea. Ni kweli kabisa nakupenda sana tangu siku ya kwanza nilipokuona. Moyo wangu umejikuta umezama kwenye mapenzi mazito juu yako ndani ya muda mfupi sana tangu tujuane mpaka nahisi kama akili yangu haifanyi kazi..

Aliongea Recho huku kilio kwa sasa kikiwa waziwazi..

Ally akazidi kumsogelea Recho na kuanza

kumfuta machozi kwa kutumia viganja vya mikono yake. Akamtazama usoni kisha akausogeza mdomo wake kwenye lips laini za Recho na kumbusu kisha kwa sauti ya taratibu akamwambia.

"I love you too Recho" (Nakupenda pia Recho.) Hata mimi kuanzia ile siku uliyokua unanisubiri nje ya darasa letu nilianza kuhisi kitu tofauti. Niliapa kuwa sitajihusisha katika mapenzi na mwanamke yeyote pale chuoni lakini wewe umeyabadilisha kabisa mawazo yangu.

Recho hakuyaamini masikio na macho yake kwa kile alichokua anakisikia na kukiona..

Nashukuru sana Ally wangu kusikia hivyo..Kwa hakika wewe ndiyo chaguo sahihi la moyo wangu na sijamuona mwanaume mwengine yeyote.. Nakukabidhi moyo wangu uwe nao milele na milele mpaka mmoja wetu atakapoondoka duniani..

Waliongea mambo mengi ya kimapenzi na kufurahi sana siku hiyo..Walipiga picha nyingi za pamoja akiwa wamekumbatina na nyengine wakipigana mabusu..Walikaa huko mpaka jioni ya saa 12 kasoro ndiyo wakaamua kuondoka kurudi nyumbani..

Walipofika eneo lenye parking za magari Recho alishangaa kumuona Ally akiliendea gari jeusi aina ya Verrosa..

Mmhhh! Kumbe una gari baby?

Ally alitabasamu kisha akamjibu.

Hapana sina baby..Hili ni gari la baba ila leo hajaenda ofisini ndio maana nimeamua kulitumia..

Ooh! Sawa.

Ally alimfungulia mlango kisha Recho akaingia ndani ya gari na safari ya kurudi nyumbani ikaanza..Ally alimpeleka Recho

mpaka nyumbani kwao Tabata Bima kisha

wakaagana kwa mabusu motomoto na kukumbatiana ..Ally alirudi nyumbani kwao Temeke na huo ndio ukawa mwanzo mpya wa penzi Lao.

** **
muendelezo ni lini?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom