Simuelewi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simuelewi

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Meritta, Jul 5, 2011.

 1. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #1
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hi wana jf,nina mpenzi wangu tuliyedumu miaka mitano sasa but kwa kipindi hiki simuelewi amebadilika,ananfanyia visa mara ohh mimi namdharau na muona boya,simpend but kiukwel nampend na sijawai kumdharau kibaya zaid anamwambia rafki yang mimi na yeye it over,me mwenyewe hajaniambi zaidi ya kuniambia nisimpigie wala nisimtumie masseg na namba zangu kafuta zote,sababu maalum hatoi,roho inaniuma bado nampend,nifanye nini ndugu zangu
   
 2. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #2
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280

  Pole sana,...ila kuna kitu mimi nashindwa kuelewa kidogo_inakuwaje mpnz wako anakuambia usimtumie tena sms na namba zako kafuta halafu wewe unajifanya kichwa ngumu eti bado hajakuambia muachane eti anamwambia rafiki yako,...mkuu achana na tabia za kulazimisha mambo_kama mwanamke anakuwekea vikwazo ambavyo vinakuumiza ni bora uachane nae mapema

  Acha kupenda pale pasipopendeka,....wewe una wako hapa chini ya jua na yeye pia usimlaumu kwani naye ana wake na labda ndio kampata...amka kung'uta vumbi halafu anza safari.....thats how we live/do
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,237
  Likes Received: 3,653
  Trophy Points: 280
  Huyo hajiamini dada,ni shida sana kuishi na mtu wa aina hii,huna sababu ya kuumia roho,pia huna sababu ya kulazimisha kupenda,acha na mawazo ya;"nitampata wapi kama huyu?"au "nampenda mno"kama angekua anajua thamani ya kupendwa asingefanya anayofanya,utapata mpenzi mzuri na atakaeitunza hesima yako na thamani yako pia,furahia maisha dada,usikubali mtu au mazingira yakuamulie hisia zako ziwe chungu au tamu!Amua mwenyewe!
   
 4. Mentor

  Mentor JF-Expert Member

  #4
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 14, 2008
  Messages: 18,651
  Likes Received: 8,207
  Trophy Points: 280

  "Akufukuzaye, hakwambii toka" - Wahenga
   
 5. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #5
  Jul 5, 2011
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Pole sana,... lakini asukushughulishe sana huyo hajui kupenda wala maana yakupendwa,kua mvumilivu,kama unafanya kazi jiweke busy na kazi yako sikwambi kama nirahisi kumsahau unaempenda lakini kama huna jinsi na wala usipoteze time yako kumbembeleza kwani staki mwenzie basi,kama yeye anakuona hufai basi vuta subra Mungu atakupa wako wakulishana zabibu.
   
 6. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #6
  Jul 5, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 395
  Trophy Points: 180
  Umekuwa boya of coz...
   
 7. Mkirua

  Mkirua JF-Expert Member

  #7
  Jul 5, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 5,667
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Ashakumwaga hivyo. Au lugha za kiutu uzima huzielewi?
   
 8. Jomse

  Jomse JF-Expert Member

  #8
  Jul 5, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Pole sana .Usiumie sana amini kwamba maisha yanawezekana bila yeye,tena mshukuru Mungu huwezi jua amekuepushia kitu gani.
   
 9. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #9
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Kuna marekebisho kidogo mm ni dada na si mkuu, pia asante kwa ushauri wako
   
 10. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #10
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nashkuru sana Eiyer ndo maana nakupenda, kwel kuishi na mtu hasiyejiamin ni kazi kubwa
   
 11. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #11
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  ni kwel ila mapenz yanatesa sana moyo
   
 12. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #12
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  na kwel
   
 13. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #13
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Keshakuacha huyo nawe hauna budi kumuacha. How comes mtu akuletee visa vya ghafla hivo halaf aende kumwambia rafiki yafiki yako eti we na yeye 'its over'! Ili uonekane unamng'ang'ania sana au? Jiongeze wewe penda unapopendwa!
   
 14. NATA

  NATA JF-Expert Member

  #14
  Jul 5, 2011
  Joined: May 10, 2007
  Messages: 4,516
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  It is over dear!
   
 15. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #15
  Jul 5, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,867
  Likes Received: 6,219
  Trophy Points: 280

  mwenzio keshasepa hapo!!! ila kaa chini jiulize ulijikwaa wapi
   
 16. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #16
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,750
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  Kwani mwanamke hawezi kua mkuu,......
   
 17. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #17
  Jul 5, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,459
  Likes Received: 3,711
  Trophy Points: 280
  pole kwa hayo je kulikuwa na ugomvi wowote kabla ya hapo?....kwa vile bado unampenda jaribu kumtafuta kwa njia nyingine tofauti na simu umsikie anasemaje...........mwisho kama unaona haiwezekani jipe moyo utampata mwingine atakayekupenda nawe umpende.
   
 18. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #18
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  nashukuru kwani naamini Mungu yupo atanisaidia kufanya vile unavyonishauri
   
 19. LD

  LD JF-Expert Member

  #19
  Jul 5, 2011
  Joined: Aug 19, 2010
  Messages: 3,021
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Mmmh, pole dada, jipe moyo songa mbele. Utapata wa kukupenda. Mwanaume ukijifanya unampenda wakati yeye hakupendi atakuumiza tu, atakutesa atakunyanyasa, achana naye.
   
 20. Meritta

  Meritta JF-Expert Member

  #20
  Jul 5, 2011
  Joined: Apr 26, 2011
  Messages: 1,304
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  hatukugombana ila alikuwa mbali kidogo ya mji alivyorudi akawa amebadirika,lakini nitamtafuta nimsikie anasemaje ikishindikana basi nitaachia ngazi
   
Loading...