Simuelewi wifi yangu


Kuna watu wana mtazamo hasi jamani, kama huna sababu huwez mchukia ndugu wa mume, kikawaida hata kama umgeni hutaki kukurupukia jiko la watu, utakaa karibu mke akiingia jikoni, utamwambia wifi nikusaidie kukuna nazi, wifi vyombo mnaoshea wapi, we uje ulale ndani me nije kukwambia njoo upike, c ndo ntatangazwa. vingine kama mwanamke unajiongeza tu
 
loh. tupo wengi, nitakusafishia nyumba yako nzima ila jikoni kwenye swala la mapishi labda niitwe. kwanza sipend wageni waje kwangu waanze kufanya kazi za nyumban, kwani bila huyo mgen kazi hazifanyki!!

Shost na we ukiwa mgeni ndo full kulala
 


Mkuu shkamoo
 
We bidada visa hivyo. Angeanza kuchangamka kuingia jikoni ungenuna na kumsusia jiko. "maana waswahili jiko linawauma sana.Tena huyo anaheshima na ustaarabu, ni kwa kakayake lakini kawa mgeni hataki makuu.
Hamkawii kuanza kuchonanisha MTU name kakake nyie.
 
Haya bana, ndiyo wake zetu wa .com hao, kitu kidogo tu keshapost status kwenye social networks, kama mimi ndiyo mumeo ningeshakulapua vibao! Mapokezi kwa mgeni ni kitu muhimu sana, kama ukionesha disinterest kama vile umetambulishwa mtu barabarani basi usitegemee ushirikiano.
 
Ungemchana live huyo wifi yko, tuna mambo mengi ya kuchangia humu ndani sio lako la uchoyo na ghubu.
 
Sioni mantiki ya mtoa mada ss ulitaka chakula cha bwanako apike dadake au? Huyo si housegirl wako ebo! Siku 3 tu lawama kibao akikaa mwezi itakuwaje? Ww timiza wajibu wako kama humuoni vile usihangaike na ndugu maana hawakai milele kwako wanapita tu! Ukianza mvutano na ndugu ndoa itakushinda maana wakati mnatongozana na bwanako ndugu hawakuwepo, wameshirikishwa tu! Fuata maisha yenu na mumeo!
 
mmmmh! kwa hapo hata simshangai huyo wifi yako coz inategemea wewe amekukutaje na huo ujio wake umeupokea vipi, ila wewe nahisi ndo wale ambao wanakuaga serious sana anajifanya yuko bize na mambo yake hapo hata mm siinuki ng'oo, hapo dada tumia busara zako hebu muweke karibu kama unavyowaweka ndugu zako ili akuzoee uone mambo yatakavyoenda sawa bila hata kuambiwa utashangaa anajituma mwenyewe
 

Mchane tu! Umesema ukweli mtupu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…