MamaBeata
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 325
- 112
Wifi yangu amekuja juzi. Ni dada wa mume wangu. Alipofika sikuwepo nilikua kazini. Nilipofika toka kazini nikamkuta amelala. Nikamsubiri alipoamka akaja tukatambulishana tukaendelea na maongezi.
Jana siku ya pili kaamka kaoga kawasha tv, akitoka anaenda kulala. Anaamka anakula anarudi kulala. Leo siku ya tatu ameamka mapema tu ameoga karudi tena kulala. Mwenzenu Simuelewi huyu mwanamke mwenzangu hata mlango wa jikoni haujui. Nimekua kama nina waume wawili. Kuolewa kuna shida wenzangu.