Simuelewi Mume wangu

Kwani na yeye anaweka pesa humo? je anatoa pesa au zimekaa tu?

Je umemuuliza juu ya maendeleo na yeye amekataa unachotaka kutumia pesa kufanyia au ni kila kitu unachotaka kufanya bila kuangalia ni nini au nini?
 
Kwanini usimuulize yeye anataka kufanya nayo kotu gani?
Pengine ana wazo la maana zaidi kama kujenga au kuanzisha biashara.

Badala ya kung'ang'ania kuzitumia kufanya hicho unachotaka wewe, jadili nae kuhusu nini chakufanya. Wote mtoe mawazo yenu kisha mpange muanze na mmalize na kipi.
 
Ninachotaka kufanya ni mradi mzuri tu naye alionyesha kukubaliana nami ila ndio full kuzungushwa.
 
Anadai kuwa anaweka pesa humo pia nimejaribu kumbana aombe internet bank niwenaweza kufuatilia akaniwashia moto nikajikuta naomba msamaha na issue ikaishia hewani.
Cha ajabu nikimwambia issue ya maendeleo ananiambia nlikuwa nafikiria hivyo hivyo mke wangu ila nikimwambia sasa tufanye hicho kitu anakuwa kimya tena na nipesa nyingi
 
Anadai kuwa anaweka pesa humo pia nimejaribu kumbana aombe internet bank niwenaweza kufuatilia akaniwashia moto nikajikuta naomba msamaha na issue ikaishia hewani.
Cha ajabu nikimwambia issue ya maendeleo ananiambia nlikuwa nafikiria hivyo hivyo mke wangu ila nikimwambia sasa tufanye hicho kitu anakuwa kimya tena na nipesa nyingi


Kwanini unataka internet banking, kwani account haipo katika majina yenu wawili? au?

usiseme ni jina lake tu na hujui kinachoendelea humo?
embu tueleze tukushauri
 
Kwanini unataka internet banking, kwani account haipo katika majina yenu wawili? au?

usiseme ni jina lake tu na hujui kinachoendelea humo?
embu tueleze tukushauri
Account ipo kwa jina lake tu si unajua kupenda sikuona kama ni shida na isitoshe ni mume.
 
Inafaa ufungue akaunti ya kwako peke yako hiyo achana nayo usije ukagombana na mume wako
 
Mipango hupangwa kitandani mama,
mume kwanza kazi badae.

hilo neno. nina rafiki yangu leo ameongea na mke wake yuko TBR wote ni waalimu. Mke anamuomba mumewe amuongezee fedha ili japo apate kibaiskeli cha kumfikisha kazini kwani amechoka kuazima kwa waalimu wenzake na kuvizia lift kila siku. Jamaa anamuambia mke kuwa hizo ni bajeti zake na kwamba yeye hafikirii baiskeli, anafikiria mambo makubwa sana.
Nikamshauri amuongezee mkewe fedha kwani ni kweli kutoka anapoishi hadi shuleni ni mbali sana.
Akaniambia nawaendekeza sana wanawake. tena anakongeza, mimi sikuwahi kumuomba fedha yake hata siku moja na hata sifahamu anatumia kiasi gani kwa mwezi.
Nikamuuliza ana mpango gani kuhakikisha kuwa wanakuwa pamoja ili kuondoa tatizo la matumizi mara mbili kwa mwezi kwa kitu ambacho kingelitumika mara moja? "Kama atachoka kukaa mwenyewe huko Tabora, atatafuta uhamisho mwenyewe". Hapo sikuchangia chochote.
 
Sasa kama umesha gundua anakuzuunguusha, na hayupo transparent,
unangoja nini kuanzisha account yako mwenyewe? Ukute hizo pesa hazipo tena...
Vile unasubiri kupewa maelezo kuhusu hizo pesa anza kwanza kuweka zako pembeni.
 
Unajua haya mambo ni magumu sana. Kila mtu huvutia kwake. Nina mfano mmoja wa kweli kabisa Dada yangu juzi kati tu kaolewa baada ya kutiwa mimba wakiwa chuoni na mwanafunzi mwenzake ambaye ni sasa ndo mume wake. Ndugu wa Mume mtu waligoma kufanya sherehe ila sisi hatukuwa radhi mwanetu aondoke bila sherehe mwisho wa siku tukafanya sherehe. Hii ni kwamba mwanamume ambaye kamuoa dada yangu atapenda sana upande wa mwanamke (Dada yangu).

Narudi kwenye topic mimi kama mimi nampa Big up mmeo (mwanamme mwenzangu) kwa maamuzi yake hayo. Ana akili kama yangu. Na ni kama kaka zangu.

Anachokifanya ni kuepuka risk siku anakufa ndugu zake kuhangaika. Bila shaka kishaandika urithi kwa mtu ambaye Ndugu yake ambaye ana hakika atakuangalia wewe na watoto kama unao bila kusahau ndugu zake.

Kama unaona anakosea ulikuwa wapi kutafuta za kwako?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom