Simuelewi huyu mwanamke

Sawa mkuu
 
Ni ngumu kuweka visa vyote hapa, ila anyway asante kwa mchango wako.
 
Nimesoma mpk mwisho halaf sijaelewa dhumuni la huu uzi
 
Futa namba yake kabisa, alafu tafuta mrembo mkali wa maana.

Huyo atarudi tu muda si mrefu. Maana inaonekana kanogewa na mbwembwe za mwanzo za bwana mpya.
 
Hapo kwenye usiku mwema saa 12 nimecheka maana hata mimi nina tabia hiyo. Iko hivi, inaweza kutokea umemmiss mtu and you are dying to talk to him mpeane michapo ya siku then anakuambia anahitaji kupumzika....najikuta kwa hasira namwambia usiku mwema kwa maana kuwa kama hauna nafasi ya kuongea na mimi sasa hivi hata mimi baadae sitakuwa na nafasi pia maana nitapumzika na mimi. Lakini ikitokea ukanitafuta baadae tutaongea tu vizuri labda wewe ndio uamue kufufua kesi au naweza kukutafuta tena mwenyewe hata hiyo baadae. Ulichokosea wewe ni kutomtumia sms tena wakati unaona yupo hewani na yeye akalikuza na hatimaye mmefika hapo mlipofika....kifupi ninyi wote wawili mna visirani na huenda angekutafuta yeye ungemwambia 'si ulinitakia usiku mwema wewe'...wanawake tunapenda kubembelezwa jamani teh. Nawatakieni kila la heri
 
Sweetest comment from you ever, anyway nadhani nilitakiwa kuwa mpole zaidi ila it was too late, kubembeleza penyewe ni kipaji
 
Kuna mda bora muachane tu maana unaweza tumia nguvu kubwa kumshawishi akuelewe kumbe ndio unakosea, binafsi mpenzi wangu akiniambia tuachane huwa sihtaji kujua hata sababu aende tu, mapenzi mda mwingine n kero ukionesha kujali sana kumtafuta mwenzi wako mara kwa mara inakuwa kero unaonekana msumbufu, ukisema uwe kmya unaonekana hujali
pole mkuu
 
Haya mapenzi ya kukaa kila muda sijui mnapigiana simu,mara sijui eti vi sms!! mtajikuta kila siku mnagombana nani aanze kumsalimia mwenzie badala ya kujikita kwenye maendeleo,wakati wapenzi wengine wanafanya mambo ya kimaendeleo kama vile kujenga nyumba,kuanzisha biashara e.t.c nyinyi mmekalia kugombana eti kwanini hukunipigia simu!! ndio maana nikasema,haya ni mapenzi ya kitoto.
 
Huyu alikuwa ameshakuacha,sababu umejitaftia mwenyewe tu maana yeye hakuwa na sababu kabisa.

Pole sana mkuu,ndio maana eti kuna wengine wanakushauri uwe nao wengi,akikuzingua mmoja unahamia kwa mwingine,ila mimi sikushauri hivyo.
 
Huyu alikuwa ameshakuacha,sababu umejitaftia mwenyewe tu maana yeye hakuwa na sababu kabisa.

Pole sana mkuu,ndio maana eti kuna wengine wanakushauri uwe nao wengi,akikuzingua mmoja unahamia kwa mwingine,ila mimi sikushauri hivyo.
Daah utakuwa kweli mkuu, ila hatukugombana kabisa...
 
Daah inakwaza sana, hizi shughuli za kuwekeza kwenye moyo wa mtu ni ngumu
 
Huo ni utoto tu unamsumbua. Kuna wakati wanawake huwa tunatamani kufikiriwa sisi tu kila muda yaani ile mtu akiamka akuwazie, akienda chooni akuwazie, akiwa na kazi zake aache akufikirie na tunaenda mbali zaidi hatutaki hata wawe na muda na marafiki na jamaa zao yaani all the time wawe na sisi tu. Na ukiona hajakutafuta ndani ya saa chache unamtishia kuachana. Nilikuaga na upumbavu huu ila mtu ukishakua ndo unaona ni upuuzi na ujinga uliopitiliza wenye uselfish ndani yake
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…