Simuelewi Huyu Muhindi

Simuelewi Huyu Muhindi

Tape measure

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2015
Posts
1,988
Reaction score
3,688
Habarini wanajukwaa,
Naombeni kujuzwa maana ya hii kitu kwani na amini kuna watu wenye ufahamu zaidi,. Katika harakati zangu za kutafuta green pasture nilikutana na wahindi watatu tukakubaliana kuanzisha kiwanda hapa nchini, basi wiki iliyopita siku ya jumatatu wahindi wakaja kutoka India kwani walikua safarini, na mimi nilikua Arusha.

Ilinipasa kusafiri kutoka Arusha kuelekea Dar es salaam na kushukia katika hoteli moja, ambapo pia na muhindi mmoja alikua akilala apo. tulikubaliana kuwa gharama zote ni juu yao nilikaa daresalaam kwa takribani siku 6 tukiwa tunaendelea na mambo mbalimbali ikiwemo kuandaa brandy name na mambo mengine ya usajili.

KISA CHENYEWE!!!
Ilikua siku ya jumamosi ambapo muhindi mmoja alinipigia simu na kuniuliza nipo wapi nikamjibu nipo maeneo ya Kimara matembezi akaniuliza Je funguo za rum kwangu niko nazo nikamjibu nimeziwacha reception basi akasema sawa, Kichwani nikajiuliza maswali mengi kwa nini aliniuliza kuhusu funguo za chumbani kwangu??? Au amehisi nmeamua kutembea nazo?? Au anataka kuniibia vyeti vyangu au passport yangu ya kusafiria?? Kwa nini aulizie kuhusu funguo?? Niliwaza sana.

Sikukawiaa sana nikarudi hotelini na kwenda kukagua chumbani kwangu sikukuta kitu chochote kimeibiwa lakini baada ya kuzidi kukagua uvunguni nikakutana na kitambaa chekundu pamoja na uzi wa kushonea pia mashuka yalikuwa kama kuna mtu aligusa kwani nilipoondoka niliacha baadhi ya document kwenye angle ya kitanda na hivo kukuta zimesogezwa mpaka katikati ya kitanda.

Niliamua kwenda kumfuata muhudumu wa mapokezi na kumuuliza ni nani ameingia chumbani kwangu alishtuka sana na kuniuliza kwani kuna kitu kimeibiwa?? sikumjibu nikamuuliza tena kwa ukali nani ameingia chumbani kwangu?? basi akanijibu kuwa boss wako alikuja akaniambia nimpe funguo aliingia dakika chache na kutoka. Nikamuuliza tena umejuaje kuwa yeye ndiye boss wangu?? Akajibu kwa kuwa ndiye anayekuja kulipia garama zako za hoteli na chakula.

Nikamwambia siku ingine kwa mteja mwingine nakuomba usirudie hiki kitendo mpaka upate ruhusa kutoka kwa muhusika Je ningekuta vitu vyangu havipo ungefanyaje?? Baada ya kumdodosa sana aliniambia kuwa yule mhindi anapenda kuchoma udi chumbani kwake na kufanya sala kwa namna fulani lakini kwa jinsi alivo nielezea nikatambua kuwa huwa atakuwa anafanya Meditation ila muhudumu alishindwa kutambua.

sikumuuliza yule muhindi kuhusiana na yeye kuingia chumba changu bila mimi kuwepo wala kupata ruhusa yangu, nilimwambia mhudumu anibadilishie chumba kingine na kuendelea na kazi yangu, ila bado najiuliza alikuja kufanya nini chumbani kwangu?? Je niendelee naye katika biashara au niachane nao???
 
Mkuu wahindi wanaamini sana uchawi.

Ila kingine nakuonea huruma kwa sababu mhindi akitaka kujua kitu kutoka kwako atajifanya rafiki yako na wakati huo huo wenzake wanajifunza, siku ya siku wakishapata walichokuwa wanataka wanakutosa.

Kama mna business deal, nakushauri iende kisheria. Documentations ziwepo zikielezea utakuwa unafanya
nini na utakuwa unapata asilimia ngapi.

Usipofanya hivyo, mwisho wake ni kulia.
 
Kutokana na maelezo yako na ushahidi uliopo, Muhindi alikuja kuchunguza business documents zako. Hicho kitambaa chekundu chini ya uvungu inawezekana kilikuwapo hata kabla hujahamia hicho chumba, unless ulichungulia chini ya uvungu wakati unapewa chumba na hukuona kitu.
 
Unaweza kumwambia kuwa kuna document au kitu fulani kilikuwa chumbani kwako na hukioni.....umeulizia reception wamesema mtu pekee (ukiacha cleaners) aliyeingia chumabni kwako ni yeye. Jifanye kumuuliza kama ni kweli aliingia na hiyo document ni yeye kaichukua. Hiyo itamlazimisha kwa kiasi fulani kusema kile alichoingia kufanya au kuchukua.

Kwenye biashara, kuaminia (TRUST) ni jambo la muhimu sana. Na uamnifu unajengwa, hauji hivi hivi tu.
 
Kutokana na maelezo yako na ushahidi uliopo, Muhindi alikuja kuchunguza business documents zako. Hicho kitambaa chekundu chini ya uvungu inawezekana kilikuwapo hata kabla hujahamia hicho chumba, unless ulichungulia chini ya uvungu wakati unapewa chumba na hukuona kitu.
Hakuna mtu mnyenyekevu kama mhindi anapokuwa anataka kitu kutoka kwako. Hawa jamaa nimewavulia kofia. Na kama wengi wanavyosema itakuwa huyo mhindi alimtega jamaa ili ajue a-z ya plan zake na akishajua kila kitu atamwacha solemba. Na kuhusu hicho kitambaa ni imani za uchawi. Wahindi wanaamini sana kwenye mambo ya uchawi. Ni sana tu. Hivyo hicho kitambaa kina lengo lake (japo mimi siamini kuwa kinaweza kuleta madhara yoyote).
 
Partnership na muhindi ni pasua kichwa.
Nina ndugu yangu alikuwa na business idea nzuri sana ila hakuwa na mtaji. Akaamua kuwashirikisha wahindi ila kwa makubaliano ya kugawana hisa 50% each.
Baada ya wale wahindi kulisoma lile wazo, wakamtosa na kwenda kuanzisha kivyao.
Wahindi au watu wa asia wamezaliwa kuwa wanyonyaji.
 
Nimewaza sana japo walinilipa pesa zangu zote lakini nilihisi harufu yahujuma

Mkuu kumbuka kwamba Wahindi na Wachina si watu wa kuaminika ni wanafiki sana, wanachotaka ni kukutumia wewe kwanza kama ngazi ya kupandia wakisha kamilisha malengo/mipango yao ya kujizatiti hapa nchini kibiashara/investment watakutosa. Member mwezetu hapa amekushauri kwamba akikisha unakuwa na wanasheria mahili wakati wa kutiliana mkataba wa ku run joint venture/investment na uhakikishe unakaa nao kwa machale, wengi wao ni ma racist na wanafikiri Waafrica ni mbumbumbu sana ni watu wa kuwatumiwa tu wakisha fanikisha malengo yao wanakugehuka - don't you forget kwamba they feel comfortable wakishirikiana na Watanzania wenye asili ya INDIA kuliko waswahili na actually katika tembea tembea yao hapa mjini si ajabu wamekwisha kutana na kufanya mazungumzo na Wahindi wa hapa nchini ambao wana hulka ya kuwaribia sifa waswahili.

Documents nyeti zinazo husika na makubaliano yenu usiwe unatembea nazo au kuziacha sehemu ambazo ni rahisi kuibiwa kirahisi, umekwisha ona dalili sio nzuri kilichobaki ni kujihami masaa yote unapokuwa nao, mazungumzo yote ya maana mshirikishe mwanasheria wako na ikiwezekana record mazungumzo yenu kwa kificho.
 
Partnership na muhindi ni pasua kichwa.
Nina ndugu yangu alikuwa na business idea nzuri sana ila hakuwa na mtaji. Akaamua kuwashirikisha wahindi ila kwa makubaliano ya kugawana hisa 50% each.
Baada ya wale wahindi kulisoma lile wazo, wakamtosa na kwenda kuanzisha kivyao.
Wahindi au watu wa asia wamezaliwa kuwa wanyonyaji.
Ni opportunist, always looking to get the most out of you and not in a good way.
 
Partnership na muhindi ni pasua kichwa.
Nina ndugu yangu alikuwa na business idea nzuri sana ila hakuwa na mtaji. Akaamua kuwashirikisha wahindi ila kwa makubaliano ya kugawana hisa 50% each.
Baada ya wale wahindi kulisoma lile wazo, wakamtosa na kwenda kuanzisha kivyao.
Wahindi au watu wa asia wamezaliwa kuwa wanyonyaji.

Kwa upande wa Asia na Mashariki ya mbali watu wanao aminika ni Wajapan labda kwa mbali na Wakorea ya kusini.
 
Hao wahindi wanakutumia sababu sio wazawa wa hapa..!kuhusu ushirikina,wanaamini sana.subria kurogwa.
 
Hakuna baya hapo endelea na mipango angekuwa na nia mbaya angetumia namna nyingine na sio hiyo
 
Back
Top Bottom