Simuelewi huyu kaka, wazoefu nishaurini

Simuelewi huyu kaka, wazoefu nishaurini

Ushimen

Platinum Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
44,853
Reaction score
113,305
Habari za uzima wanajamii,

Leo nimekuja na hili mnisaidie ushauri maana wakati wote naamini humu ndani kuna wazoefu na wenye hekima busara na ushauri wa kumrudishia hadhi mtu aliepatwa na sintofahamu ya kimapenzi.

Hii ni hali niliyohadithiwa na mdada akiniomba ushauri nami nimeamua,niilete kwenu kiukweli yuko ktk wakati mgumu kukubaliana na ukweli.

Ni mdada mwenye umri upatao 30-33, amewahi kuwa na mahusiano yasiyo na furaha kwa kipindi kirefu,ni member wa JFpia.

Akaamua,kutulia kwa takribani miaka minne bila mahusiano hadi hapo mapema mwaka huu alipoamua kujikabidhi mwili na roho nzima kwa mkaka wa kitanzania aishie nje ya nchi.

Penzi likakolea kweli kweli na mdada akaona sasa amepata faraja,kiukweli mbeba boksi alimueleza mengi mdada juu ya past relationships zake hivyo mdada alijiaminisha kwa kaka kuwa sawa amepata pumziko la nafsi.

Baada ya muda mfupi kaka akarudi bongo likizo hivyo furaha ya dada ikaongezeka.

Lol!! laiti mioyo ingekuwa inafunguliwa dada asingeingia miguu yote, inauma hiii ikikukuta,uushhh.

Ujio wa kaka ukawafanya wawe karibu sana wakipanga na kupangua mambo kadhaa wa kadha,kumbuka kaka alikuwa muwazi sana kwa dada hadi ID's zake JF akampa password,hiyo haitoshi wadada wanaomfuata PM na kwingineko pia dada alikuwa akioneshwa dialogue zote.

Hapo kiukweli lazima umwamini kaka huyo. Kila program dada alishirikishwa.

Kizaazaa kikaja kaka akawa anapigiwa sana simu muda mrefu na dada mwingine,ndipo kaka akamueleza ukweli dada mpenzi wake kuwa kuna mdada walikutana via JF ni mbongo pia anaishi ughaibuni lkn US anampenda ila yeye hana mpango nae coz ni mke wa mtu ingawa wapo kwenye mgogoro na mumewe na anataka kumwacha.

Dada akaridhishwa na utetezi penzi likaendelea, kadri siku zilivyosonga mawasiliano na mdada wa US yakazidi,ingawa kwa kificho lkn penzi kikohozi dada wa Bongo akawa anashtukia movie, kaka anazidi kujitetea kuwa hana issue na huyo mmarekani bali anataka tu kumtumia kiuchumi.

Hapo sasa ndo music ukaanza, dada haelewi iweje uwe na mtu tena mdada udate nae na huna hisia nae kisa tu unataka umtumie, ikaenda hiyo issue kimya kimya za mwizi fourty,bidada kutoka US akaona isiwe shida akatia timu TZ na akawa anahitaji close relationship na kaka.

Siku ikafika mdada wa Bongo akagundua mpenzi wake ametoka na Mmarekani coz hiyo siku mdada wa Bongo alikuwa anasafiri Mwanza from Dar na mkaka alipaswa kumsindikiza lkn cha ajabu hakutokea na simu haipokelewi,kesho yake kaka akajieleza kuwa mmarekani alimbana hivyo amsamehe coz yeye km alivyosema ana mahaba nae na anamtumia Mmarekani kimaslahi.

Hiyo hali inamtesa sana dada huyu wa kibongo,hamwelewi kaka mbeba boksi ambae likizo yake ikaisha yet bado yuko tight na Mmarekani.

Dada kajitutumua aongee na mbeba boksi yaishe coz kiukweli anampenda sana ,kilichofuata kaka kamwambia kwakuwa hunielewi nakutengenezea future sasa narudi Emirate likizo imeisha na wewe na mimi tuachane na yule Mmarekani namwacha nitaanza upya.

Wakati anamuaga hivyo bado kaka begi lake liko kwa Mmarekani na ndiye anayemsindikiza Airport, dada kachanganyikiwa,pressure ikashuka haamini kilichotokea.

Ushauri wako ni muhimu tumsaidie muhanga huyu wa mapenzi.

Wanajamii ushauri tafadhali.
 
Huyo mdada afanye yake, kama vp kuolewa cyo lazima ajipange, awe na subira kama yuko wake atampata tu, period...
 
Hasa kinachomchanganya hapo ni kipi?umri wake na mapenzi yake kwa huyo kaka yasimchanganye.....mwambie a-focus,huyo kaka hajui kupenda wanawake anajua kuwatumia tu hata akimuacha huyo mmarekani akamfuata yeye baadae atamuumiza tu na yeye,............atulie atampata mwingine
 
Yaani mtu mpenzi wako anakwambia anapenda kuwachuna ngozi wapenzi wake.... na wewe upo unakenua tuuu bila kushtuka ???
 
Ushauri gani sasa wakati liko wazi, mbeba box hana kosa hapo. We nae ninani wake mpaka akuadisie, mwambie siku nyingine asijifanye mzigo watu watakuwa wanapita tu!
 
Ushauri gani sasa wakati liko wazi, mbeba box hana kosa hapo. We nae ninani wake mpaka akuadisie, mwambie siku nyingine asijifanye mzigo watu watakuwa wanapita tu!

Mkuu hebu funguka zaidi,km sijakusoma vile
 
Una uhusiano gani na huyo dada? Kama kweli alimpenda mbeba box basi hakutimiza wajibu wake mapenzi ni 2 way traffic.

Huyo dada ni rafiki yangu.
Sasa kwanini asiambiwe kuhusu kutimiza huo wajibu km hiyo ndiyo sababu haswa.
Mmmmhhhh mapenzi, roho ya mtu kichaka
 
Back
Top Bottom