Ushimen
Platinum Member
- Oct 24, 2012
- 44,490
- 112,028
Habari za uzima wanajamii.
Leo nimekuja na hili mnisaidie ushauri maana wakati wote naamini humu ndani kuna wazoefu na wenye hekima busara na ushauri wa kumrudishia hadhi mtu aliepatwa na sintofahamu ya kimapenzi.Hii ni hali niliyohadithiwa na mdada akiniomba ushauri nami nimeamua,niilete kwenu kiukweli yuko katika wakati mgumu kukubaliana na ukweli.
Ni mdada mwenye umri upatao 30-33 amewahi kuwa na mahusiano yasiyo na furaha kwa kipindi kirefu,ni member wa Jamii Forums pia,akaamua,kutulia kwa takribani miaka minne bila mahusiano hadi hapo mapema mwaka huu alipoamua kujikabidhi mwili na roho nzima kwa mkaka wa kitanzania aishie nje ya nchi.
Penzi likakolea kweikweli na mdada akaona sasa amepata faraja,kiukweli mbeba boksi alimueleza mengi mdada juu ya past relationships zake hivyo mdada alijiaminisha kwa kaka kuwa sawa amepata pumziko la nafsi,baada ya muda mfupi kaka akarudi bongo likizo hivyo furaha ya dada ikaongezeka.
Lol laiti mioyo ingekuwa inafunguliwa dada asingeingia miguu yote, inauma hiii ikikukuta,uushhh, ujio wa kaka ukawafanya wawe karibu sana wakipanga na kupangua mambo kadhaa wa kadha,kumbuka kaka alikuwa muwazi sana kwa dada hadi ID zake Jamii Forums akampa password,hiyo haitoshi wadada wanaomfuata pm na kungineko pia dada alikuwa akionyeshwa dialogue zote.
Hapo kiukweli lazima umwamini kaka huyo. Kila program dada alishirikishwa, kizaazaa kikaja kaka akawa ana pigiwa sana simu muda mrefu na dada mwingine,ndipo kaka akamueleza ukweli dada mpenzi wake kuwa kuna mdada walikutana via jf ni mbongo pia anaishi ughaibuni lakini US anampenda ila yeye hana mpango nae cause ni mke wa mtu ingawa wapo kwenye mgogoro na mumewe na anataka kumwacha.
Dada akaridhishwa na utetezi penzi likaendelea, kadri siku zilivosonga mawasiliano na mdada wa US yakazidi,ingawa kwa kificho lakini penzi kikohozi dada wa bongo akawa anashtukia movie, kaka anazidi kujitetea kuwa hana issue na huyo mmarekani bali anataka tu kumtumia kiuchumi. Hapo sasa ndo music ukaanza, dada haelewi iweje uwe na mtu tena mdada udate nae na huna hisia nae kisa tu unataka umtumie.
Ikaenda hiyo issue kimya kimya za mwizi forty,bidada kutoka us akaona isiwe shida akatia timu Tanzania na akawa anahitaji close relationship na kaka, siku ikafika mdada wa bongo akagundua mpenzi wake ametoka na mmarekani cause hiyo siku mdada wa bongo alikuwa anasafiri mwanza from Dar es salaam na mkaka alipaswa kumsindikiza lakini cha ajabu hakutokea na simu haipokelewi,kesho yake kaka akajieleza kuwa mmarekani alimbana hivyo amsamehe cause yeye kama alivyosema anamahaba nae na anamtumia mmarekani kimaslahi.
Hiyo hali inamtesa sana dada huyu wa kibongo,hamwelewi kaka mbeba boks ambae likizo yake ikaisha yet bado yuko tight na mmarekani,dada kajitutumua aongee na mbeba boksi yaishe cause kiukweli anampenda sana ,kilichofuata kaka kamwambia kwakuwa hunielewi nakutengenezea future sasa narudi emirate likizo imeisha na wewe na mimi tuachane na yule mmarekani namwacha nitaanza upya, wakati anamuaga hivyo bado kaka begi lake liko kwa mmarekani na ndie anaemsindikiza airport, dada kachanganyikiwa,pressure ikashuka haamini kilichotokea.
Wanajamii ushauri wako ni muhimu, tafadhali tumsaidie muhanga huyu wa mapenzi.