Nampa pole sana mdogo wangu
Mimi naona kosa la lilianza pale alivyo ambiwa yupo na mmarekani kimaslahi; hapo ndio alitakiwa alete uzi ili tumpige stop huyo mmarekani, na kama haondoki tungemuacha huyo kijana wakati huo.
Naona dada yangu anawakati mgumu sana ila namwambia kutoka moyoni kuwa huyo kijana hakuwa mume, na kama wangeishi naye angemuumiza zaidi. Nivizuri mungu amemuonesha mapema.
Kwa kuwa mungu amembariki kuwa na kazi yake, naomba achape kazi kwa bidii zaidi na ajipe muda kidogo, afocus kwenye mambo ya maendeleo (kufungua ka biashara, kausafiri hata kama ni bajaji nk)
Pamoja na kuwa mume/mke hupatikana popote, nafikiri apendelee uhusiano na watu wa hapa nyumbani...hao wa nje wengi wao ni wazushi. Wanakuwa na mlolongo wa marafiki...na huwezi jua wewe ni wangapi kwenye list....