Simuelewi huyu demu

Simuelewi huyu demu

Atoke mjini akaolewe chaka nafikiri huo ni uongo wa dhahiri na huyo mchumba gani anamuoa wakati hawana mawasiliano yanayoeleweka au anatumia njia ya posta?
We rudi tena uongo ukiisha atakukubali tu.
 
Lakini siku hizi hutumii nguvu kubwa Mkuu, labda hakutaki kweli. Vumilia tu uone mwisho lakini huyo hakutaki pamoja na kumpa simu.
 
Kuna binti anaishi na dada yake pia anamsaidia dada yake kuuza msosi kwenye mgahawa wao.

Sikuwa na tabia ya kula gengeni ila nikaanza kula gengeni baada ya kumpenda huyu binti aliyekuwa akimsaidia dada yake kazi.

Nikamuomba namba ya simu hakuwa na simu ikabidi nimpatie simu moja maana nilikuwa na simu mbili.

Tulianza kuwasiliana nikamtongoza akasema yeye bado ni mdogo hawezi kuolewa kwa sasa niache kumsumbua.

Leo nimempigia kumkumbusha ombi langu anadai anaye mchumba huko kijijini kwao na mahari imeshatolewa anaenda kuolewa.

Swali ni kwamba je, atakuwa ananipima na kunikatisha tamaa au nikomae nae?

Yaani uko vizuri sana, ulivoona communication barrier ukaona bora utoe simu yako.Hahaha kabla ya kutoa simu yako ilibidi uwe umeshajiridhisha anyway sijui utafanyeje kuchukua simu yako ama ndiyo imekwenda na maji tena hiyo.Yaani kumuona tu unatoa simu hahahaha
 
Back
Top Bottom