Simu zenye camera zaidi ya moja zinapigaje picha?

uyui kwetu

JF-Expert Member
Oct 23, 2013
1,185
734
Nimekuwa natumia simu za kamera zaidi ya moja ila kuifunika kwa mkono zingine inaonesha inayopiga ni kamera moja tu je kuna sehemu ya ku set?
 
Uyui Kwetu,

Mfumo wa kiutendaji na mfumo wa uchakataji picha kutoka katika simu yenye kamera zaidi ya moja umegawanyika katika namna ya utendaji kama ifuatavyo;-

- Kamera / Camera ambayo ina kazi ya ufyatuaji au uchukuaji picha na utengenezaji

IMG_20200617_210415.jpg

Sharlene Taule (Picha halisia) Daniel Duran

- Sensa za Undani / Depth Sensor ambayo inafanya upangaliaji wa pikseli ( Seli za Picha ) / Pixels katika mtiririko iliyokuwa ndani ya uwezo wa kamera, kupitia hii ndio utapata Bokeh, Light Leak's, Blur na Len's Flares

Aaron Ramsey.jpg

Aaron Ramsey (Seli za Blur) ©FAWAL

- Upana katika pembe / Wide Angle hii inakusanya taarifa ya picha katika upana na kuitundika katika uhalisia huku ikisaidia upanuaji na ukuzaji wa picha husika

Arsenal_Wardrobe.jpg

Arsenal DR (Picha yenye kukusanya upana) © Arsenal

- Lenzi yenye upana zaidi / Ultra Wide Angel Lens ambayo husaidia ukusanyaji, usambazaji na uchakataji wa taarifa katika picha moja yenye upana zaidi hii Ultra Wide inaakisi zaidi kushinda wide angle pasi yakufikia Panorama Mode.

HECTOR.jpg

Hector Bellerin (Picha iliyokusanya eneo zaidi pasi ya nguvu ya asili ya picha) ©Hector Bellerin

- Lenzi mpangilio wa Rangi / Monochrome lenses na Telephoto lens hii inatumia hisia, na hali ya sasa kuchakata mpangilio wa rangi, mandhari na kuinakili picha katika mg'ao (Sharpen) pasi ya kupoteza uhalisia

Freddy Lju.jpg

Freddie (Uhalisia / Mawingu, Vivuli, Mwanga, Giza) ©Arsenal
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom