Chief-Mkwawa
Platinum Member
- May 25, 2011
- 32,265
- 44,396
kwa hiyo mkuu una maanisha kwamba simu za microsoft hazitatoka tena au itasitisha huduma yake ya simu? maana najua microsoft aliinunua nokia ndo akaondoa jina la nokia na kuweka microsoft but stil ukiandalia design ni ya hardware ni kama nokia tuu sema wamebadilisha jina pia na ile symbian OS wakaitoa.Sidhani kama watanza mwaka huu may be awamu ya kwanza mwaka 2017 kwa sababu mkataba wa Microsoft na Nokia unaisha mwisho wa mwaka huu.
kampuni ya Nokia imetangaza jana kwamba wanarudi tena kwenye soko la simu baada ya kuipa haki kampuni ya HMD kutumia jina na technology zote za Nokia.
Kampuni hii ya HMD ambayo imezinduliwa jana hio hio itakuwa na makao yake makuu Finland (kama Nokia), itakuwa inaongozwa na CEO Arto Nummela ambaye ni mfanyakazi wa Nokia toka mwaka 1994, pia Kampuni hii itakuwa na raisi anayeitwa
Florian Seiche huyu jamaa pia ni mzoefu sana alikuwa Siemens kipindi wanatengeneza simu na amefanya kazi Htc toka 2005.
unaweza cheki cv zao hapa
HMD global
na website ya HMD
HMD global
kampuni hii ya HMD watakuwa wanadesign simu, kufanya marketing na uuzaji wakati utengenezaji utafanywa na Foxconn
pia kampuni hii pamoja na Foxconn watanunua department ya simu ya Microsoft ambayo ilikuwa inahusika na Feature Phone hivyo Talent za Nokia zitarudi Nyumbani Finland.
vifaa watakavyotengeneza hawa jamaa ni smartphone na Tablets ambazo vyote vitakuwa ni vya android
Muono wangu
-Ni huzuni kwetu Fans wa Nokia sababu Nokia atakuwa hatengenezi simu (atleast kwa miaka 10 ijayo) lakini ndio mambo yameshatokea ni wakati wa kusogea mbele
-Hii kampuni ya HMD ina majina makubwa toka Nokia ya zamani lets Hope watatengeneza simu zenye quality kubwa na sio Kubrand simu za kichina
je umefurahia au hujafurahia kurudi kwa simu za nokia?
source
Nokia signs strategic brand and intellectual property licensing agreement enabling HMD global to create new generation of Nokia-branded mobile phones and tablets
Microsoft amewauzia Foxconn biashara yake ya simu za Feature phone, Ukumbuke Microsoft alikuwa anatumia jina la Nokia kwenye feature phone tu kwenye smartphone zilikuwa zinaitwa Microsoft Lumia, hivyo kuanzia sasa hivi Microsoft hana tena uhalali wa kutumia jina Nokia. HMD na Foxconn exclusive watatumia jina Nokia bila kushare na mtu yeyote.mkuu ntafrahi. sana ukinip hatima ya micrpsoft maana. najua ndo. walioinunua nokia. sasa yametokeaje hayo tena na mkataba ulikua miaka 10 au umevunjwa?? na microsoft ndo kwa. heri au b
au vipi tena?
Nokia wana miaka 150 katika hili game, ni kampuni ambayo hufanya maamuzi ya ajabu lakini matunda yake huonekana baadae. Miaka ya 80 wakati inaacha kutengeneza makaratasi na matairi na kujiwekeza zaidi kwenye mambo ya network (kipindi hicho hata network ya simu haijagunduliwa) watu walishangaa kama tunavyoshangaa sasa hivi lakini leo hii Imekuwa ndio kampuni kubwa zaidi ya Network za simu ikiwa na patents nyingi zaidi za 2G, 3G na 4G.Sasa umesema Nokia hata tengeneza simu kwa miaka 10, na hio HMD itakua makao makuu Finland ilipo Nokia, pia simu zitakazotoka zitakua android...hapo naona Nokia inazikwa rasmi...
Mkuu hapo HMD wakizingua ujue kuna miaka 10 bila Nokia,Nikiona Brand Name ya Nokia nafurah sana. Nilisikitika jina la Nokia kupotea kiaina badala yake Lumia kusikika sana.
Kama wanarudi kutengenezea Android phones hiyo ni habari njema nitanunua Nokia. By the way kwanini Chief umehuzunika badala ya kufurahi?
Microsoft amewauzia Foxconn biashara yake ya simu za Feature phone, Ukumbuke Microsoft alikuwa anatumia jina la Nokia kwenye feature phone tu kwenye smartphone zilikuwa zinaitwa Microsoft Lumia, hivyo kuanzia sasa hivi Microsoft hana tena uhalali wa kutumia jina Nokia. HMD na Foxconn exclusive watatumia jina Nokia bila kushare na mtu yeyote.
Kuhusu hatma ya simu za microsoft tetesi ni kwamba zitaungana na department ya Surface. kama unafatilia mambo haya nafkiri utakua unajua mafanikio ya Tablets za microsoft zinazoitwa surface pro sasa hivi zimeshakuwa billion dollar business na zinaipa joto Apple na Ipad zake. Microsoft kuanzia 2017 watatoa surface phone simu zinazorun software za computer nafkiri wanawasubiria intel wakija na processor za 10nm za canonlake ila ni tetesi tu inaweza isiwe kweli.
Makubaliano yalikuwa kwamba, Nokia wasitumie jina la NOKIA kwenye simu hadi tarehe 31 Disemba 2015. Nokia waliuza facilities zao, pia baadhi ya teknolojia waliwaruhusu microsoft wazitumie ndani ya miaka kumi ila si zote. Ina maana kuna baadhi ya teknolojia bado ni mali ya Nokia. Watakachofanya Nokia ni kuwaruhusu HMD watumie brand pia baadhi ya teknolojia za Nokia. Pia ili zitumie jina (brand) la NOKIA bidhaa za HMD zinatakiwa zifikie viwango ambavyo Nokia wataridhika navyo kwani kwenye nafasi fulani za maamuzi za juu (nimesahau ni chombo gani ila ni chombo cha maamuzi) wamepewa Nokia.
Kwa hiyo si kwamba HMD wata-design smartphone na kuzitengeneza tu, la hasha, lazima Nokia wahakikishe zinakidhi viwango (vinavyoendana na hadhi ya brand ya Nokia) wanavyovitaka.
mkuu hata mm ningependa iwe hivyo ila angalia microsoft wanavyotolewa jasho na windows yao watu siku hizi ku accept new thing wakati wamezoea android na os ya apple ni ngumu kweli kweli....Walichokosea ni kuweka Android kwenye hizo simu.
Binafsi hakuna OS inayochefua kama Android.
Nilitegemea wangekuja na OS yao kabisa.
Ningekuwa mteja wa kwanza kabisa, ila haya mambo ya Android wamenikosa.