Simu ya Zitto Kabwe yashikiliwa Polisi miezi 14

Simu ya Zitto Kabwe yashikiliwa Polisi miezi 14

Alexander The Great

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2018
Posts
4,514
Reaction score
23,703
JESHI la Polisi linaendelea kuzishikilia simu ya Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT Wazalendo), Zitto Kabwe, kwa miezi 14 sasa kwa ajili ya uchunguzi.
1.jpg


Kwa mujibu wa maelezo ya polisi walioshikilia simu hizo tangu Novemba mwaka jana, waliichukua ili iwasaidie kukusanya ushahidi wa takwimu alizozitoa (Zitto) kuwa uchumi wa nchi unasinyaa.

Akizungumza na Nipashe jana, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano ya Umma wa ACT Wazalendo, Ado Shaibu, alisema bado Jeshi la Polisi inashikilia simu hiyo kwa uchunguzi na hawajui wataipata lini.

“Jeshi la Polisi linaendelea kushikilia simu ya Zitto na walisema wakimaliza uchunguzi wao watamrudishia, sasa ingawa muda mrefu umeshapita hatujui watampatia lini,” alisema.

Pia alisema Jeshi hilo bado halijarudisha kompyuta ndogo, flashi, nakala za machapisho yao zilizochukuliwa Novemba 7, mwaka jana.

Simu hizo zilichukuliwa baada ya Zitto kuripoti Kituo cha Polisi Kamata, jijini Dar es Salaam, kutekeleza wito wa Jeshi hilo kwa ajili ya kuhojiwa.

Akizungumza na waandishi siku ya tukio, Shaibu alisema polisi wamechukua simu yake kwa maelezo kuwa itasaidia katika uchunguzi wao na kuahidi watairudisha siku iliyofuata.

Alipotafutwa jana kuzungumzia suala hilo, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.

Katika tukio hilo Jeshi la Polisi lilifanya msako mkali ofisi za Makao Makuu ya chama hicho, zilizopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam na kuchukua baadhi ya vifaa hivyo vya ofisi.

Mwishoni mwa mwaka jana, Zitto aliwaambia waandishi wa habari kuwa anajipanga kulifungulia kesi ya kikatiba Jeshi la Polisi nchini kutokana na kushikilia simu yake.

Zitto alisema simu yake inashikiliwa tangu Novemba 7, alipokamatwa kwa tuhuma za kuvunja Sheria ya Takwimu na Sheria ya Makosa ya Mtandao.

Zitto alisema Katiba ya Nchi kifungu cha 16(1) na (2) imeweka msingi wa nguvu sana haki ya faragha kwa raia na kwamba hata sheria ikitaka haipaswi kuingilia mawasiliano binafsi ya raia.

“Nina mashaka kuwa Jeshi la Polisi linakaa na simu yangu muda wote huu kwa sababu zaidi ya uchunguzi wao wa makosa wanayonituhumu nayo. Nimeamua kuwaachia simu mpaka hapo watakapotosheka, lakini wajiandae na kesi ya kikatiba ambayo pia italinda haki za wananchi wengi wanaothirika na matumizi mabaya ya Sheria ya Mtandao (Cybercrime Act ).

-IPP
 
ndio maana marekani analitukana jeshi la police,halijui kwenda na wakati,usikute hiyo simu kuna sanjent kajimilikisha.
 
ndio maana marekani analitukana jeshi la police,halijui kwenda na wakati,usikute hiyo simu kuna sanjent kajimilikisha.
Kabisa mkuu, nchi za wenzetu haupelekwi mahakamani au kulazwa rumande bila wapelelezi kuwa na ushahidi kamili wa kukufikisha mbele ya mikono ya sheria. Na hawakurupuki wala hauta sikia wamechukua sim yako kisha wakakaa nayo miezi kwaajili ya upelelezi.

Kuna wakati mtu unakamatwa umefanya kosa la jinai, ila kutokana na kukosekana na ushahidi wanakuachia huru (Huku wanakuambia kijana una bahati hatujapata ushahidi wa kutosha kukupeleka mahakamani, ila safari ijayo tukipata ushahidi utakoma).
 
Back
Top Bottom