Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,072
- 79,443
SIMU YA USIKU WA MANANE
Leo Taikon sina maneno mengi, nianze kwa kuwasalimia wote, Kalagabaho!
Sijui kama nakosea, lakini kama nikijiita mwenyeji wa mji wengi wanaweza kunikazia macho yao mabaya wakiniita Mjuaji. Najua siwezi kukataa kuwa wapo wenye miji yao ambao hawataniruhusu nijipe anuani hiyo 'Mwenyeji wa Mji'. Nimepata wazo, nafikiri ni wazo bora kabisa. Nimeona niteremke mpaka njia panda yalipomakutano ya mji, zilipo njia nne zitokazo pande nne za dunia.
Huko nitakutana na mwenye mji, kisha niambatane naye, atanitembeza huku, huko na kule ndani ya mji huu. Hata wageni na wenye mji wengine wakituona tupitapo watatupa salamu za heshima, nami sitakawia kuzipokea na kuzijibu, kama wakiniuliza habari zangu nitajitambuisha kama mwenyeji wa mji huu huku nikicheka kwa tabasamu la ufahari wa majibu yangu.
Nikashuka mpaka Njia panda kubwa ya mji ule, huko nikakutana na wapita njia wengi, hapo macho yangu nikayapa kazi ya kutambua mwenye mji ule. Nikaona Kilinge pembeni ya yale makutano, ilipo barabara yenye lami. Nikajipa mwendo nikasonga, hapo nikawa nimeshakikabili kile kilinge, wazee wakicheza bao la kete.
Kama nitasalimia nitahitajika kujidhihirisha kwa majina, na hapo ningezua balaa kubwa. Nikaona si vyema kujisalimia, nikasogea kama hatua kumi tuu huku macho yangu nikiyapa kazi kuwatazama wazee wachezao bao kwenye kile kilinge, nikiamini hapo nitapata Mwenye Mji. Hapo nikavutiwa na Mzee mmoja hivi, haiba yake ndio ilinikosesha ujanja wa kumkwepa, Alikuwa na mvi za kijivu na ndevu zenye mvi nyingi, uso wake ulikaribia uso wa mwenye Falsafa za Kimarx, mara kwa mara aliongea wa sauti yenye ishara ya msalaba. Kila mara alitabasamu alipokuwa akisukuma kete zake.
Nafikiri wengi wa wazee pale walimheshimu, sikujua heshima hiyo waliyompa ilitokana na nini hasa, nikafikiri bila dhamiri kuwa huenda yeye ni Bingwa wa mchezo wa Bao la kete. Hata hivyo fikara hizo zilipotea katika kope zangu tuu pale nilipoona kijitabu fulani hivi kikiwa kwenye goti la mguu wake. Kitabu chenye jalada la rangi ya damu ya mzee.
Punde mchezo uliisha, na yule mzee alinyanyuka; muda wake wa kuondoka uliwadia, alichukua Mkongojo wake, hapo akaaga wana Kilinge wenzake na kuondoka mimi nikiwa namtazama, mwendo wake ulizipeleka fikara zangu mbali mno. Nilikumbuka Msafara wa Siriel na Janalaidana, kama sio kusemeshwa na yule mzee, sijui kama fikra zangu zingerudije maana zilienda mbali mno.
Mzee aliniuliza ninaitwa nani, nikafikiri kwa tahadhari, kama ningejitambulisha Mliberali pengine angenipiga kwa ile fimbo yake.. Basi kwa uzee wake nikaona nikijiita MJAMAA Ningemfurahisha.
Basi ningepaswa kusema kijamaa, kutabasamu kijamaa, kucheka kijamaa na kutembea kijamaa. Hapo ndipo nikataka kujua nimefikia kiwango gani cha sanaa ya thietre. Nikajitambulisha kwa sauti iiyojawa mitetemo ya kijamaa.
Azimio la mababu lilizaliwa, nami nikapata jina langu humo, unakumbuka mwaka 1967? Nikamuuliza; hapo akanishangaa kwa uso wa kinabii ndevu zake zenye utukufu na macho yenye hekima nyingi yakanitazama.
Mimi ni mjamaa,, ndilo jina langu, pengine ni jina la kizamani nililopewa mtu wa zama hizi, sijali kama haliendani nami, ninachojali ni kuwa linanifaa na limenifanya mtu mwenye heshima kubwa sana kwenye mji huu. (Hayo niliyasema kujifanya kama mimi ni mtu mashuhuri eneo mji ule, nikiadhimia anione mwenyeji wa mji ule hata kama yeye ni mwenye mji).
Hapo akanitazama akiyakunja macho yake kama mtu anayetaka kunikumbuka, pengine aliniona ni mjukuu wa moja ya wazee wa Mji ule.
Basi baada ya kumrubuni mzee wa watu na sasa tukawa tunatembea katika barabara za mji ule nyakati za jione, yeye akijiona kama anatembea na moja ya wajukuu wa Azimio la Mababu, akijionea fahari nami nikawa kama mmoja wa wenyeji wa mji ule. Kila tulipopita alinitambulisha kwa wakuu na wenyeji wa mji ule, nami nikijifaharisha kwa kujigeuza mwenyeji wa mji. Bila kusahau sauti ya kijamaa, miondoko ya kijamaa, tabasamu la kijamaa na mikao ya kijamaa.
Basi giza likafukuza nuru ya mchana, usiku ukaingia mlango wa nyuma na nuru ikitokea mlango wa mbele. Palipokuwa nuru pakawa giza, huo ndio usiku katika mji ule. Basi muda wa kula ulipofika, sikusahau kula kijamaa, kutafuna na kumeza kijamaa. Nikikumbuka nabaki kucheka sana. Hapo wakahitaji kujua habari za Azimio la Mababu na yaliyomo ndani ya azimio hilo.
Nikawaambia, lilikuwa azimio la mababu mji huu uwe mji wa wenyeji, matajiri wakubwa watokane na wazawa wa mji huu, tena katika azimio lile ilikuwa jinai kubwa kwa mgeni kumiliki utajiri wa mji huu labda nusu yake, nashindwa kushangaa, jiungeni nami kustaajabu, oneni sasa, tazameni, hapo niliongea kijamaa zaidi nikitoa mishangao ya uzalendo wa kijamii.
Hili la wageni kuwa matajiri zaidi yetu limetushangaza mno, wageni wameutwaa mji huu na kuumiliki huku sisi wenyeji na wenye mji tukihangaika na kuwa watumwa wao. je hili halishangazi, mimi sio tuu kushangaza bali hata kuumiza pia. Unajua Azimio la Mababu lililenga mambo ya msingi sana..
Mimi nikasema, labda tuenda katika makaburi yao tukayafukue kisha tuchukue sanda zao, zile ziiandikwa habari za elimu ya kujitegemea, unajua sera za azimio la mababu hazikulenga elimu ya kitumwa kama hivi leo.
Elimu iliyokusudiwa ni ile ya kujitegemea na kuzikomboa jamii na changamoto zinazotuzunguka. Elimu ya azimio la mababu ilizikwa na wajasiriamali walioingiza ubinafsi wao wa kibiashara kwenye elimu. Tazameni vijana wa mji huu sasa wanavyogeuka watumwa kwenye mji wao.
Elimu ya kileo imewafundisha vijana wa mji huu kuwa wapumbavu na wajinga, niliwaona wasomi wa mji huu wenye shahada wakiandamana kwenye lango kuu la mji huu, kila aingiaye na kutoka aliwaona wakilalama na kuomba msaada kama masikini. Elimu iliyokusudiwa ni ya kuvumbua na kubuni ajira zitakazo saidia vijana wengi zaidi.
Hapo niliongea mno, nikahisi ningewakasirisha wenye nyumba akiwemo yule mzee ambao walikuwa wakinitazama, huku sahani zilizobaki na makombo zikiwa zinatutazama, pengine ningenyimwa chakula kama ningezungumza habari hizi kabla ya chakula. Haya.
Nikalala, nisisahahu kulala kijamaa, na kuota ndoto za utaifa na uzalendo, nikaomba shuka lenye bendera ya mji ule. Hatimaye nikalala mpaka usingizi ukalala nao, hii ni kusema sikujua nimelala na usingizi wenyewe haukujua nimelala au nimekufa.
Sikumbuki ni lini ilikuwa mara yangu ya mwisho kuota ndoto za usiku nilalapo. Ni takribani miaka 28 sasa sijaota ndoto yoyote ile. Ndoto yangu ya mwisho niliyoiota ilikuwa mwaka 1992. Ilikuwa ndoto mbaya sana. Ilikuwa ndoto ya machafuko ya kisiasa na kisera katika mji huu. Ile ndoto ilihusisha mambo ya kidunia na mwenendo wa kisera, na hapo ni baada ya waliberali na mabepari kuingiza sera za Kibeberu katika Mji huu.
Sasa nillisikia simu ikiita, sikujua ninaota au nisimu kweli ilikuwa ikiita. Nikapokea simu, upande wapili naliusikia ukinisalimu kwa kibepari.
Nikamwambia ajitambulishe yeye ni nani, na anahitaji nimsaidie jambo gani.
Akasema, wao wamekula ndoto zao walalao usingizi, wamefuta maono ya vijana wa mji ule. Hawataota ndoto tena pindi walalapo, watalala kama wafu walalao. Wataishi bila maono kama wanyama, wakisubiri kesho yao wasioijua wala ambayo hawajawahi kuiona.
Kama wangekuwa na maono wangeiona kesho yao, na kama wangekuwa wanaota wakilala basi wangekuwa na matarajio.
Lakini sasa wamekuwa wakiliona jua likizama na kuchomoza pasipo kuhesabu siku zao, leo husema kesho tutafanya hivi, jua likizama huzama na mipango yao, kesho ikifika wamesahau walichopanga jana"
Nikamuuliza kwani wewe ni nani usemaye nami, je ninaota au ni kweli umenipigia simu? Lakini kama ningekuwa naota, si umesema vijana wa mji huu hatuoti tena ndoto pindi tulalapo, nami ni kweli ni zaidi ya miaka 28 sijaota ndoto yoyote mpaka sasa.
Na kama umenipigia simu, ni wapi na nani allikupa namba zangu, ulizipata wapi namba za Mjamaa kama mimi?
Akanijibu Akasema;
Mtumwa haoti ndoto kama Bwana wake" Kisha nikazinduka usingizini nikiwa nimeshika simu. Sikujua nilikuwa naota au ni kweli nilikuwa naonngea na simu; kwa maana nikisema nilikuwa naongea na simu na nilikuwa sioti mbona nilikuwa nimelala na nimezinduka kweli? Nikisema nilikuwa naota na nilikuwa siongei na simu; mbona nimeshika simu na nimeiweka sikioni?
Basi nikaangalia kwenye kioo cha simu,, nikakuta simu imezima chaji. Nikafikiri labda ni kweli nilikuwa naongea na simu na wala haikuwa ndoto, na yule Bepari aliyekuwa akiongea nami hakukata simu bali simu illizima chaji.
Basi nikaona niwaandikie habari hizi ili nanyi mpate kujua mambo haya.
Kwa leo sitaki maswali, wala majibu...
Taikon nimemaliza, Mwenyeji wa Mji wa Njia nne.
Robert Heriel
Taikon wa fasihi
0693322300
Kwa sasa Dar es salaam