Simu ya muuaji: Apple yajibizana na serikali ya US

Simu ya muuaji: Apple yajibizana na serikali ya US

Troll JF

Platinum Member
Joined
Feb 6, 2015
Posts
10,015
Reaction score
14,622
Majibizano makali yameendelea kati ya serikali ya Marekani na kampuni ya Teknolojia ya Apple, baada ya kampuni hiyo kukataa kusaidia kufungua simu ya mmoja wa washambuliaji waliowaua watu kwa kuwapiga risasi mwezi Disemba.

Idara ya sheria iliwasilisha ombi mahakamani ikisema simu ya mshambuliaji huyo huenda ina ushahidi kuhusu shambulio hilo.

Pia idara hiyo imelaumu Apple kwa kuwa na ukaidi. Kampuni hiyo imejitetea na kusema shirika la ujasusi la FBI linatumia njia za mkato ili kuweza
kudukua simu zote kwa kutumia kisingizio cha simu moja.

CHANZO: BBC

Writer's questions: Hivi vyombo vyetu vya Usalama vitaweza kweli mziki wa Apple/iPhone?

Kwa maana hiyo iPhone ni simu yenye security zaidi duniani?
 
Majibizano makali yameendelea kati ya serikali ya Marekani na kampuni ya Teknolojia ya Apple, baada ya kampuni hiyo kukataa kusaidia kufungua simu ya mmoja wa washambuliaji waliowauawa watu kwa kuwapiga risasi mwezi Disemba. Idara ya sheria iliwasilisha ombi mahakamani ikisema simu ya mshambuliaji huyo huenda ina
ushahidi kuhusu shambulio hilo.
Pia idara hiyo imelaumu Apple kwa kuwa na ukaidi. Kampuni hiyo imejitetea na kusema shirika la ujasusi la FBI linatumia njia za mkato ili kuweza
kudukua simu zote kwa kutumia kisingizio cha simu moja.

CHANZO: BBC

Writer's questions: Hivi vyombo vyetu vya Usalama vitaweza kweli mziki wa Apple/iPhone?

Kwa maana hiyo iPhone ni simu yenye security zaidi duniani?
OGOPA SANA
 
Sasa wahalifu wengi watatumia i phone kwa mawasiliano,market ya bidhaa za apple itapaa
 
Back
Top Bottom