Simu ya kisasa kali kuliko zote

evonik

JF-Expert Member
Jun 12, 2015
3,998
5,131
Ni simu yenye specifications zifuatazo RAM GB 12, Uhifadhi wa GB 1,000(TB 1)…Ni vigumu kuamini simu kuwa na uwezo (specifications) wa kiwango hichi ila simu ya Turing Phone Cadenza iliyopo njiani inavyo.
Muonekano wa toleo lililopita la simu ya Turing
Simu janja ya Turing Phone Cadenza imetengenezwa na kampuni inayofahamika kwa jina la Turning Robotics Industries ya nchini Marekani.

Sifa kuu- vigumu kudukuliwa, vigumu kuvunjika…hivyo kiwango cha usalama wa juu

Simu za Turing zinatengenezwa pia kwa kutumia madini magumu ya ‘liquidmorphium’ ambayo yanafanya ‘housing’ ya simu hiyo kuwa ngumu sana. Kuvunjika kwa simu hii kutaitaji nguvu ya ziada, madini haya ya chuma ni magumu sana – zaidi ya mara 1.5 ukilinganisha ugumu wa madini ya titanium.

Bei ya simu hii inategemewa kuwa kwenye kati ya Tsh 1,500,000/= – Tsh 2,500,000/=.
bfc00c769c6be68d55363df14fe6369d.jpg
a03b237e671317a460606f98beebab6d.jpg
debbf9c8e53cec13297be8463388b906.jpg


Sifa za undani;
Inakuja na ukubwa wa inchi 5.8, kioo (display – QHD) .
Kamera ina Megapixel 60, na megapixel 20 kwa kamera ya selfi.
Itakuja na prosesa mbili za kisasa ndani yake za Snapdragon 830, (prosesa zinategemewa kuanza kupatikana mapema mwakani)

Diski uhifadhi (storage) kiasi cha TB 1 , ndani kabisa ina GB 512 alafu inakuja na sehemu mbili za memori kadi ya GB 256 kila moja.
Ina kiwango cha RAM cha GB 12 – ikiwa na RAM mbili za GB sita sita..hiki ni kiwango cha juu sana, suala la uzito wa vitu kufanya kazi halitawezekana.
Unalaini nyingi za simu? Simu hii inauwezo wa kutumia laini 4 ndogo (Nano) kwa wakati mmoja .

Programu endeshaji: Inatumia programu endeshaji ya Swordfish OS (toleo la Sailfish OS) lilotengenezwa na kampuni ya Jolla – programu endeshaji hii ilianzaga kwa jina la MeeGo zamani na ilikuwa ‘project’ chini ya kampuni ya Nokia. Programu endeshaji hii imepewa uwezo wa kutumia apps za Android.

Turing Phone Cadenza imepewa uwezo mkubwa wa kiusalama wa data. Na utumiaji wake wa programu endeshaji ya Swordfish inazidi kuiweka sehemu salama zaidi kiusalama.

Kampuni ya Turin bado haijatoa bei rasmi ya simu janja hiyo ila wamesema itaingia sokoni rasmi mwaka 2017 na tuna uhakika bei yake itakuwa juu sana.
Tuambie mtazamo wako juu ya simu janja hii…

Source :www.teknokona.com
 
Ina fire extinguisher? Battery inamaana charger muda gani kwa matumizi ya kawaida?
 
Teknolojia ya sasa inaruhusu kabisa kutengeneza simu yenye uwezo na zaidi ya hivyo.​
 
Xiaomi bezel mix ndo beast ktk industry sasa hivi so far. Youtube it
 
hizo kamba tu na nyie mnaamini, simu yenye highend soc moja tu ni ngumu kuipoza hadi makampuni yanapoza simu kwa maji siku hizi, sembuse wao waeke soc mbili? labda wanatengeneza simu ya kukaangia mayai?
Kwa teknolojia tunayoiendea posibility ya kutengeneza Poa
 
Back
Top Bottom