Ashura9
JF-Expert Member
- Oct 21, 2012
- 740
- 485
Kampuni moja nchini India inatarajiwa kuzindua simu ya kisasa inayodhaniwa kuwa ya bei rahisi zaidi duniani. Kampuni ya Ringing Bells imesema simu yake iitwayo Freedom 251 itaunzwa chini ya rupia 500 (dola 7.3), lakini vyombo vya habari vya India vinasema huenda ikauzwa kwa rupia 251 (dola 3.67). Taarifa zinasema simu hiyo ina 8GB na ina kamera mbele na nyuma. India ni soko la pili kwa ukubwa duniani la simu, ikiwa na watumiaji bilioni moja. Freedom 251 inatarajiwa kulenga soko ambalo tayari lina simu za bei rahisi. "Hii ndio itakuwa simu yetu kinara na tunadhani italeta mapinduzi katika sekta hii," shirika la habari la AFP limemkariri msemaji wa kampuni. Kwa sasa kampuni hiyo inaagiza vifaa kutoka nje ya nchi na kuunda simu hizo nchini India, lakini mipango ni kutengeneza kila kitu ndani ya nchi katika kipindi cha mwaka mmoja, ameongeza kusema msemaji huyo. Riging Bells ilianzishwa miezi michache iliyopita na kuzindua hivi karibuni moja ya simu za bei rahisi za kisasa zinazotumia 4G kwa rupia 2,999 kwa mujibu wa Press Trust of India.