Simu hizi kutoka makampuni ya simu ni chunusi yenye maumivu makali kwa watumiaji wa simu

analysti

JF-Expert Member
Aug 24, 2009
731
614
Huduma ya simu (hasa simu ya mkononi) ni moja ya huduma muhimu sana kwa maisha ya mwanadamu, hasa mwanadamu huyu anayeishi dunia hii ya utandawazi. Umuhimu huu hutonaka na ukweli kwamba kupitia simu ya mkononi mtu anakuwa na uhakika wa kufikiwa na mtu anaemtafuta au kumfikia mtu amtafutaye wakati wowote ule. Aidha jambo lolote linalohitaji kumfikia mlengwa kwa dharura njia ambayo ni sahihi ni kumfikishia kwa njia ya simu.

Kutokana na hali hiyo, simu katika wakati fulani inaweza kuwa bize sana, kwani tarifa zinazomfikia mtu zinaweza kuwa nyingi kutoka kwa watu mbali mbali anaofahamiana nao, zikiwa na umuhimu tofauti. Hali hii inaweza kusababisha kadhia wakati fulani, hasa mtu anapokuwa anashughulikia suala lenye umuhimu wakati huo. Kwa sababu hii mtu anaweza akaizima simu, au akaiweka kwenye mfumo wa kimya (Silence mode). Lakini options hizi huwa ngumu kuzitumia iwapo mtu ana jambo la muhimu analolitarajia kumfikia kupitia simu, kwani kuzima, kuweka silence au vinginevyo kunaweza kumfanya akayakosa mawasiliano muhimu. Kwa sababu hii mtu anaweza kuiacha simu yake ikiwa na mlio ilhali anajambo la muhimu anaendelea kulitekeleza.

Kwa kipindi sasa kumekuwa na tabia ya makampuni mbali mbali ya simu kufikisha tarifa mbali mbali kwa wateja wao kupitia simu zao za mikononi. Taarifa hizo huwa na maudhui mbali mbali, ikiwemo matangazo ya promosheni mbali mbali za mitandao hiyo nk. Taarifa hizi zimekuwa zikipelekwa kwa wateja wa makampuni haya kwa njia ya jumbe fupi za maandishi na hivi karibuni wameanza kupeleka kwa kupitia simu. Ikumbukwe kuwa, matangazo haya hupelekwa kwa mteja huyu pasipokuwa na ridhaa ya huyu mteja. Kwa kuzingatia hayo niliyoyaeleza hapo juu, simu hizi na meseji hizi zinaweza kusababisha usumbufu mkubwa kwa mteja katika mazingira fulani.

Kuna wakati unakuta mtu X amejipumzisha (Kalala), wakati huo huo anasubiri simu muhimu kutoka kwa mtu Y. Ilhali akiwa amepumzika, simu inaita, huyu bwana X ananyanyuka akijua ni Y anampigia kumpatia habari aliyokuwa akiisubiri, anashangazwa anakuta ni namba ngeni, hivyo anaipokea na kukumbana na matangazo ninayoyaita ya KIPUUZI.

Wakati mwingine unakuta mtu yupo kwenye mkutano muhimu unaendelea, simu inapigwa, anatoka nje kupokea na kukuta ni sauti iliyorekodiwa ya muhudumu wa simu ikimtaarifu juu ya shindano la bahati nasibu.

Wakati mwingine mtu anamgonjwa kijijini, katika wakati kama huo, ukiona namba ngeni tuu, moyo unalipuka, just to find kuwa ni matangazo ya promosheni.

Usumbufu huu huletwa na njia zote nilizozitaja hapo juu, yaani sms na call, japo usumbufu huwa mkubwa zaidi kwa call.

Kutokana na ukweli kwamba serikali hii imejipambanua kuondoa kero of varrying degrees kwa raia wa Tanzania, ningeomba waziri wa Mawasiliano atuokoe sisi wananchi na usumbufu huu unaosababisha kero kwa watumiaji wa mitandao ya simu pasipo na umuhimu wowote. Hili linakuwa na umuhimu zaidi sasa, kwakuwa ni kipindi ambacho tunahamasisha uchapa kazi na si kukaa na kusikiliza stupid advertisements kutoka kwa makampuni ya simu.

Ningependekeza matangazo na tarifa hizi, zifikishwe kwa watu watakaoridhia kupokea habari hizi, wengine waachwe watumie simu zao kwa malengo waliyoyakusudia wao, na si kupokea matangazo ya biashara na mambo mengineo.

KAMPUNI ya STARTIMES NAYO HIVI KARIBUNI IMEANZA MCHEZO HUU AMBAO HAKIKA UNASABABISHA USUMBUFU MKUBWA KWA WANANCHI.

Muheshimiwa Waziri wa mawasiliano, hiki ni kichunusi chenye maumivu makali mtu kwa mgonjwa.
 
Nakuunga mkono ndugu Mtz mwenzangu. Simu nimenunua,airtime nalipia,kwa nini waniletee upuuzi wao? Yapo makampuni maarufu kwa ushenzi huu. Halotel hawana upuuzi huu. Heko M-Vietnam.
 
Haya uliyozunguzia ni tone tu ktk ndoo ya maji,kwenye tasinia ya mawasiliano huko sio majipu bali ni matambazi.

Una uhakika gani kama kifurushi unachonunua na dakika unazopewa kama zimeisha,
Unapoambiwa kifurushi chako kimeisha.

Je ikitokea mawasiliano yakakatika kwa siku nzima wale wenye vifurushi vya siku nani anawarudishia thamani ya pesa yao waliyolipia?na kiasi gani kwa siku kinapotea?
Hata Mimi nimegusa kidogo tu.
Ngoja waje wengine.

Tanzania ni shamba la bibi.
Tunashukuru kumpata jpm.
 
Kwakweli kuna matatizo makubwa sana, na ilivyokuwa inaonekana hakukuwa na mtu wa kututetea sisi kama watumiaji wa mawasiliano ya simu. Hivi, nafahamu kuna chama cha abiria, je hakuna chama cha watumiaji wa mawasiliano ya simu?. Nafikiri kuna haja kubwa ya kuwa na chama, ambacho kitakuwa na viongozi ambao watakuwa ni watetezi wetu sisi kama watumiaji wa simu. Maana hali ilivyo hivi sasa, mtu unaweza ukaibiwa pesa kwenye simu na kusiwe na mahala pa kulalamikia.
 
inakera pale unapompigia mtu badala ya kusema namba unayopiga haipatikani au busy wanaanza na matangazo yao tena marefu kweli mpaka inakeraaa
 
Hapa kwenyewe nimetoka kupokea simu ya kipuuzi kama hiyo!
Yaani nimepokea kwa heshima zote nikijua anaweza kuwa mtu wa maana kumbe ni matangazo yao hayo.....! Kwakweli inakera sana hembu waheshimu simu za watu wasitake kutuharibia siku bure...!
 
Back
Top Bottom