Donald Bakari
Member
- Sep 4, 2020
- 32
- 30
- Thread starter
- #21
Yap, kama Mhe. MtakaViongozi Bora wanatoka ndani ya CCM
Yap, kama Mhe. MtakaViongozi Bora wanatoka ndani ya CCM
Uchambuzi wenye hoja, Mhe. Mtaka anastahili kupongezwa sana. Ana kipawa cha uongozi.SIMIYU: “USIONE VYAELEA UJUE VIMEUNDWA.”
Na Donald Bakari.
View attachment 1557956
Mnamo tarehe 13 Machi 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli alimteua kijana mwerevu, mnyenyekevu na asiye na mihemko mwenye umri wa miaka 33 Anthony Mtaka kuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu. Mtaka akaingia katika vitabu vya kihistoria na kuwa mmoja wa wakuu wa mikoa wenye umri mdogo kuwahi kutokea nchini.
Hakutaka kiki, aliitazama ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015 – 2020, kwa upole, busara, hekima na maarifa akaianza kazi na kututimizia maneno ya wahenga yanayosema “Usione vyaelea ujue vimeundwa”.
JPM leo (04/09/2020) atakuwa pale mkoani Simiyu kunadi sera za CCM na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kwa kipindi cha pili katika nafasi ya urais. Kazi yake itakuwa nyepesi sana kwa sababu Mtaka na watendaji kazi wengine walishaviunda na sasa vinaelea.
Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika Mkoa wa Simiyu.
Mtaka ameutendea kazi muongozo huu, mkoa wa Simiyu umefungua fursa za uwekezaji na kunufaika nao. Katika hili JPM ataomba kura bila jasho.
- Uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji umebaini na kunadi fursa za uwekezaji katika mkoa wa Simiyu.
Simiyu ni moja ya mikoa michanga, Serikali ya awamu ya tano ikaamua kujenga hospitali ya rufaa ya Simiyu kwa lengo la kusogeza huduma za rufaa karibu na wananchi kwa sababu Simiyu ni mkoa mchanga kwa namba za kuanzishwa ila sio kwa kuweza kujitegemea. Hapa Chama Cha Mapinduzi na JPM wataomba kura kwa lugha nyepesi sana.
- Kujengwa kwa hospitali ya rufaa katika mkoa mpya wa Simiyu.
Mradi huu una thamani ya shilingi bilioni 400, ukigharamiwa na Serikali ya Tanzania, Shirika la GCF na Serikali ya Ujerumani. Mtaka ameusimamia barabara, ameshaunda JPM ataomba kura na kuondoka kwa furaha.
- Utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji na wa kimkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya mazingira mkoani Simiyu (Simiyu Climate Resilience Water Project).
Chama cha Mapinduzi kinazingatia utoaji wa haki, Ujenzi wa mahakama ya hakimu mkazi umetimiza azma ya wengi ya kuona huduma za kimahakama zinapatikana kwa ubora na wakati. JPM atawapungia mkono wananchi wa Simiyu, nao watampa kura bila kinyongo.
- Ujenzi wa mahakama ya Hakimu Mkazi wa Simiyu umekamilika.
Serikali ilihakikisha watendaji hawa wa mkoa wanakuwa na makazi bora, unajua nini kilifuata? Mtaka na wenzake wakaiongoza Simiyu katika kuhakisha wanafunzi pale Simiyu wanafaulu. Walipigana kufa na kupona kuhakisha Simiyu inapaa katika elimu.
- Ujenzi wa nyumba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu na katibu tawala wa mkoa wa Simiyu umekamilika.
Ukienda pale NECTA watakuambia Simiyu huwa haikosi kumi bora katika matokeo. JPM akifika atawaeleza kuhusu elimu bure, wananachi watasema watoto wetu wanasonga mbele kielimu kura zote Kwako JPM mzalendo wa nchi.
Usichukulie poa, Serikali iliamua. Pamba ni dhahabu nyeupe inatakiwa kuhifadhiwa vema. Mtaka alisimamia vema, JPM atasisitiza juu ya kujenga viwanda vya kutengeneza nguo zetu wenyewe na kuachana na mitumba, atafunga na kuondoka na kura zake kedekede.
- Kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao kwa kujenga ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 34,000.
Tuendelee kufurahia mafanikio makubwa na yenye tija yaliyopatikana katika Serikali ya awamu ya tano na tuwasisitize watanzania kuendelea kufanya kazi kwa bidii. “Kwa pamoja tumekeleza kwa kishido, tunasonga mbele pamoja” kura kwa JPM na Chama Cha Mapinduzi.
Wenu Donald Bakari
Email: donaldbakari4@gmail.com
Hapana hakuna aliyetumia nguvu nyingi, jambo kubwa ni kujifunza kutoka wa kiongozi huyu naYaani nikiona watu wanatumia muda na nguvu nyingi kueleza walichokifanya,huwa napata shida kama wamefanya kitu kweli,kwanini mliyoyafanya yasijieleze yenyewe kwa watu,
Hapana, Mtaka yupo vizuri. Hii taarifa sio sahihi. Tunamjua vizuri Mhe. Mtaka.Huo mradi wa maji umekamilika wapi wewe wakati nyuma tu ya hapo mkutano unapofanyikia leo hawana maji, Kuna kimto kidogo hapo nyuma shule ya msingi bariadi hakuna daraja watoto wanachelewa shule wanasubiri maji yapungue ndiyo wavuke.Uwekezaji na viwanda upo wapi hapo Simiyu.Mtaka yupo overated tu sioni alichofanya kwa Simiyu.Viwanda havionekani ni propaganda tu za kisiasa.
Kabisa mtaka hakosi 40 to 50Unaweza kua sahihi au si sahihi kwenye baadhi ya sehemu. Ni wapi kwenye ilani ya ccm imeandikwa utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za RAS na RC?
Kitu kibaya zaidi ni kusema uongo kua mwaka 2016 mtaka alikua na miaka 33; namfahamu sana Mtaka ni famili friend sana tokea utotoni na hapo Nyaumata kwake hua tunapiganae story sana..usisema uongo kwenye suala la umri kwa kiongozi wako.
Kitu kizuri kwa Mh Mtaka ni kutowaingilia ki majukumu wale wadau wa maendeleo katika mkoa wake kama Wakandarasi bali anawapa sana support na alipewa RAS Jumanne Sagini aliyegombea Ubunge Butiama.
Amna viwanda ulivyosema hapa Simiyu wenda kama unamaanisha Simiyu ya Japan.
Baraza la Mawaziri lijalo litakuwa supa, na kuna uwezekano likaanza na watu wale wale na kumaliza na watu hao hao. Ni kwa sababu Mkuu sasa hivi ana orodha ya watu wengi sana ambao kwa sasa anawajua kikamilifu utendaji wao wa kazi. Kipindi anaingia mwaka 2015, yeye naye alikuwa Waziri kama wengine, na hakuwa na makundi kwa hiyo watu wote aliokuwa akiwachagua, alikuwa anachaguliwa na watu kwa kushauriwa. Safari ijayo atakuwa anachaguliwa, huku na yeye akiwa anashiriki katika kuamua chaguzi za watu hao. Naomba nibashiri kwa asilimia za juu kabisa kuwa Mh. Mataka atakuwa mmoja wao, assuming atapita ubungeJambo jema, muda ni rafiki mzuri. Sote tusubiri naamini tutakuwa na furaha.
Hapana, pitia taarifa zote. Makala hii imeandikwa kwa kuzingatia mambo yote ya uandishi na taarifa zimetolewa katika vyanzo rasmi. Usitake kupotosha watu.Unaweza kua sahihi au si sahihi kwenye baadhi ya sehemu. Ni wapi kwenye ilani ya ccm imeandikwa utekelezaji wa ujenzi wa nyumba za RAS na RC?
Kitu kibaya zaidi ni kusema uongo kua mwaka 2016 mtaka alikua na miaka 33; namfahamu sana Mtaka ni famili friend sana tokea utotoni na hapo Nyaumata kwake hua tunapiganae story sana..usisema uongo kwenye suala la umri kwa kiongozi wako.
Kitu kizuri kwa Mh Mtaka ni kutowaingilia ki majukumu wale wadau wa maendeleo katika mkoa wake kama Wakandarasi bali anawapa sana support na alipewa RAS Jumanne Sagini aliyegombea Ubunge Butiama.
Amna viwanda ulivyosema hapa Simiyu wenda kama unamaanisha Simiyu ya Japan.
Inaweza kutokea, Mhe. Mtaka ni mfano wa kuigwa. Viongozi wengi hususani vijana wanaokua katika uongozi wanatakiwa kujifunza kutoka kwake. Ni kiongozi ambaye hufanya maamuzi kwa ajili ya maendeleo jumuishi, hafanyi kwa ajili ya kuwafurahisha watu wachache. Anazingatia weledi, nidhamu, uadilifu, bidii na maarifa katika kazi na utumishi wake wa umma. Mwenyezi Mungu amuongoze.Baraza la Mawaziri lijalo litakuwa supa, na kuna uwezekano likaanza na watu wale wale na kumaliza na watu hao hao. Ni kwa sababu Mkuu sasa hivi ana orodha ya watu wengi sana ambao kwa sasa anawajua kikamilifu utendaji wao wa kazi. Kipindi anaingia mwaka 2015, yeye naye alikuwa Waziri kama wengine, na hakuwa na makundi kwa hiyo watu wote aliokuwa akiwachagua, alikuwa anachaguliwa na watu kwa kushauriwa. Safari ijayo atakuwa anachaguliwa, huku na yeye akiwa anashiriki katika kuamua chaguzi za watu hao. Naomba nibashiri kwa asilimia za juu kabisa kuwa Mh. Mataka atakuwa mmoja wao, assuming atapita ubunge
Naamini mwezi wa kumi na moja au kumi na mbili tutashuhudia mambo mazuri.Kabisa mtaka hakosi 40 to 50