Donald Bakari
Member
- Sep 4, 2020
- 32
- 30
SIMIYU: “USIONE VYAELEA UJUE VIMEUNDWA.”
Na Donald Bakari.
Mnamo tarehe 13 Machi 2016 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. John Pombe Magufuli alimteua kijana mwerevu, mnyenyekevu na asiye na mihemko mwenye umri wa miaka 33 Anthony Mtaka kuwa Mkuu wa mkoa wa Simiyu. Mtaka akaingia katika vitabu vya kihistoria na kuwa mmoja wa wakuu wa mikoa wenye umri mdogo kuwahi kutokea nchini.
Hakutaka kiki, aliitazama ilani ya Chama Cha Mapinduzi ya 2015 – 2020, kwa upole, busara, hekima na maarifa akaianza kazi na kututimizia maneno ya wahenga yanayosema “Usione vyaelea ujue vimeundwa”.
JPM leo (04/09/2020) atakuwa pale mkoani Simiyu kunadi sera za CCM na kuomba ridhaa ya kuchaguliwa kwa kipindi cha pili katika nafasi ya urais. Kazi yake itakuwa nyepesi sana kwa sababu Mtaka na watendaji kazi wengine walishaviunda na sasa vinaelea.
Yafuatayo ni baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika Mkoa wa Simiyu.
Ukienda pale NECTA watakuambia Simiyu huwa haikosi kumi bora katika matokeo. JPM akifika atawaeleza kuhusu elimu bure, wananachi watasema watoto wetu wanasonga mbele kielimu kura zote Kwako JPM mzalendo wa nchi.
Tuendelee kufurahia mafanikio makubwa na yenye tija yaliyopatikana katika Serikali ya awamu ya tano na tuwasisitize watanzania kuendelea kufanya kazi kwa bidii. “Kwa pamoja tumekeleza kwa kishido, tunasonga mbele pamoja” kura kwa JPM na Chama Cha Mapinduzi.
Wenu Donald Bakari
Email: donaldbakari4@gmail.com

- Uzinduzi wa muongozo wa uwekezaji umebaini na kunadi fursa za uwekezaji katika mkoa wa Simiyu.
- Kujengwa kwa hospitali ya rufaa katika mkoa mpya wa Simiyu.
- Utekelezaji wa mradi mkubwa wa maji na wa kimkakati wa kukabiliana na athari za mabadiliko ya mazingira mkoani Simiyu (Simiyu Climate Resilience Water Project).
- Ujenzi wa mahakama ya Hakimu Mkazi wa Simiyu umekamilika.
- Ujenzi wa nyumba ya mkuu wa mkoa wa Simiyu na katibu tawala wa mkoa wa Simiyu umekamilika.
Ukienda pale NECTA watakuambia Simiyu huwa haikosi kumi bora katika matokeo. JPM akifika atawaeleza kuhusu elimu bure, wananachi watasema watoto wetu wanasonga mbele kielimu kura zote Kwako JPM mzalendo wa nchi.
- Kuongeza uwezo wa kuhifadhi mazao kwa kujenga ghala lenye uwezo wa kuhifadhi tani 34,000.