SIMIYU: Mahakama za kimila zilizookuwa zikiamuru walimu kupigwa viboko zapigwa marufuku

RUCCI

JF-Expert Member
Oct 6, 2011
1,701
1,714
Serikali mkoani Simiyu imepiga marufuku mabaraza ya kimila maarufu kama(dagashida) ambayo yamekuwa yakiamuru kupigwa viboko waalimu,kutozwa faini na hata kutengwa na jamii pale ambapo watumishi hao wamekuwa wakikataa kufuata mambo yao wanayoyataka katika vijiji wanakofanyia kazi.

Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa amelitoa wilayani Itilima wakati alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara ambapo amesema serikali imechoshwa kuona waalimu na watumishi wengine wakionewa na mahakama hizo ambazo amesema haziko kisheria,na zimepitwa na wakati.

Kufuatia agizo hilo la Mkuu wa Mkoa chama cha waalimu wilaya ya bariadi kimepongeza hatua hiyo na kusema itarudisha imani kwa waalimu ambao wengi wao walikuwa katika harakati za kuhama kutokana na kukithiri kwa vitendo vya kupigwa na kufanyiwa vurugu na mabaraza hayo ya kimila.

Uchunguzi uliofanywa na ITV umebaini kuwa mahakama hizo zilikuwepo tangia awali na kazi yake kubwa ilikuwa ni kusimamia nidhamu katika jamii lakini hivi sasa zimekuwa zikienda kinyume hali ambayo imefanya zilalamikiwe kila mahali kutokana na kuendesha mambo yake kwa kukiuka sheria za nchi na haki za binadamu.
 
Walimu wameonewa sana kwenye nchi yetu hii, yaani leo hii ndiyo wanakumbuka kuzipiga marufuku wakati walimu wamekwisha chapwa bakora muda mrefu mweee
 
Back
Top Bottom