Simbachawene: Serikali yasitisha Kuwanyang'anya Mihuri Wenyeviti wa serikali za Mitaa

Troll JF

JF-Expert Member
Feb 6, 2015
7,804
12,233
MEDIA=twitter]821296440563683328[/MEDIA]

Serikali yasalimu amri yasitisha agizo la kuwataka wenyeviti wa serikali za mitaa nchi nzima kurudisha Mihuri kwa maafisa watendaji. Hayo yamesemwa na Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mheshimiwa George Simbachawene.

Waziri Simbachawene amefafanua kuwa, Serikali imeamua kuwaruhusu Wenyeviti wa S/Mitaa kumiliki mihuri huku ikiendelea kuwapa elimu ya matumizi yake.
 


[HASHTAG]#Habari[/HASHTAG]:Serikali yasitisha agizo la kuwataka wenyeviti wa serikali za mitaa nchi nzima kurudisha Mihuri kwa maafisa watendaji.



Walikuwa wananyang'anywa mihuri kama adhabu au kutumbuliwa, ama ilikuwa ni maboresho/mabadiliko ya mfumo?
 
Nitaliamini hili tangazo pale tu likitolewa kupitia redio mbadala au kipindi cha 360!
 
Nani stelingi wa hii Movie?.
Jamani hata maji ya mvua yana mikondo yake!. Harakati hii ya kufanya maamuzi kwa staili ya zima moto kwenye utumishi na uongozi siyo mazuri.
Wakamateni wapiga madili na siyo kuwapa adhabu wapiga kura.
 
Walikuwa wanatumia mihuri kupata 2000 kila barua na wanaweka mfukoni, anyway ni sawa sbb hawalipwi mishahara.. haya bana
 
Mbona ana-surrender mapema hivyo. Naishauri serikali iwe na msimamo inapotoa matamko yake, ni mbaya sana kutoa tamko halafu unasikilizia response ya watu. Hawa wenyeviti wa mitaa wasingejikusanya na kuomba mwongozo wa kisheria ndo i9ngekuwa imepita hivyo. Serikali inatakiwa itambue kwamba kwa dunia ya leo watu wana ufahamu mkubwa sana juu ya mambo ya kisiasa na kijamii.
 
Back
Top Bottom