Simbachawene: Mitambo ya Gesi Mtwara ing'olewe

Simbachawene: Mitambo ya Gesi Mtwara ing'olewe

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Naibu Waziri wa Nishati na Madini na Mbunge wa Kibakwe-CCM,George Simbachawene ametoa mpya.

Amependekeza mitambo ya kuchimba gesi asilia mkoani Mtwara ing'olewe ikiwa ni kuwaadhibu wananchi wa Mtwara aliowaita wahaini. Katika mazungumzo yake kwa njia ya simu na Makada wa Chama cha Mapinduzi walioko Ofisi Ndogo za CCM -Lumumba Dar es Salaam, Simbachawene alisema watu wa Mtwara ni waasi na wanapaswa kushughulikiwa ipasavyo.

Mazungumzo hayo yalifuatia nia ya Makada wa CCM kutaka kupata maoni ya Naibu Waziri huyo juu ya nini hasa alijionea alipofanya ziara ya kushtukiza mkoani Mtwara. Simbachawene, bila kubana maneno, amesikika akisema: 'Cha kufanya ni kuwaamuru Wawekezaji wote waliopo katika machimbo ya gesi Mtwara kung'oa mitambo yao ili tuone kama gesi hiyo itatumika nao wananchi hao'

Katika kile kinachoonekana ni kuchoka kuoongoza kwa CCM,baadhi ya makada maarufu wa CCM akiwemo William Lukuvi,kwa nyakati tofauti leo, wameonesha kuguswa na kukubaliana na pendekezo la Simbachawene. Pia inapendekezwa kuwa Mh.Murji (Mbunge wa Mtwara Mjini-CCM) afikishwe kwenye vikao vya chama ili kufunzwa uzalendo wa kusimamia maamuzi ya chama na Serikali.

Wenu,
VUTA-NKUVUTE a.k.a Mzee Tupatupa wa Lumumba Dar es Salaam
 
Sidhan kama anastahili kuendelea na hiyo nafasi aliyonayo! Awaachie wanaoweza kuongea na wananchi. Kama taarifa hii ya ukweli.
 
Mzee Tupatupa huyo Waziri zamani tulielezwa zamani na mwana JF mmoja kuwa alikuwa mpiga debe pale kituo cha mabasi Dodoma, kukua na kuendelea kisiasa kumemfanya awe kipofu, yeye amesikia wananchi wamekasirika kwa jinsi mkuu wa mkoa, na waziri Muhongo matusi yao yalivyowaudhi wananchi.

Kama sio kulewa madaraka fedha zote zilizolipwa za utafutaji gesi, uaandaaji wa mradi na mikopo iliyokopwa atalipa mama yake hivi haya MACCM tumeshindwa vipi kuyang'oa mbona yanajifanya yako juu ya sheria na wananchi.

Wang'oe wana mtwara watafurahi wakichagua serikali nyingine watazungumza namna ya kuendesha mradi huo isiwe tabu
 
Naanza kuamini kuwa huu ni mradi mkubwa wa chama (ccm), maana hayo matamko ni makali utafikiri huo mtambo wa kuchakata gas ukijengwa Mtwara basi mapato yatanufaisha Msumbiji na si Tanzania. Wananchi wamechoka kuburuzwa na gas haitatoka kirahisi pamoja na ubabe wenu.
 
Mnara wa Babel(CCM) huo taratibu unaanza kudondoka, Mtu akitumwa nyundo anapeleka Shoka! wakitumwa mbao wanapeleka misumari...

CCM Wangefanya lamaana sana kwa kuwaondoa wawekezaji wote nchini...hadi wale wanaochukua Dhahabu zetu burebure kule Geita, Kahama, Singida, Nyamongo, Serengeti na Chunya...Waondoeni wote wenye kuchimba Uranium, Almasi, Tanzanite, Gesi, Nickel na hata Gypsum kule upareni...Mkimaliza waondoeni wawekezaji mliowapa vitalu vya uwindaji kwa bei chee...sababu, nia na uwezo mnao coz Wananchi wote kwa sasa ni Wahaini Kwa CCM na Serikali yake...

...mgetusaidia sana ili 2015 tuanze upya ...!!! kisha baada ya miaka 10 tuwatoe keko/ukonga mshuhudie kwa mshangao nchi ya ahadi tunayo iota kila kukicha...
 
Big up Simbachawene! tutapataje hasira za kuing'oa ccm madarakani bila ya statement zenye maudhi kama hizi!?? we need more of the alike statement ili hata alielala aamke! aione ccm katika sura yake halisia ya unyang'au!
 
Ngoja ngoja ngojea mbona mwaka huu 2013 patafahamika Na hii kitu unaambiwa Bunge halijaanza.. Ngojea lianze..
 
Wanatakiwa waichimbe kwa mikono hii gesi hawa wamakonde.
Umekosea mkuu tumeshafikia zama Za jembe mkulu.. So wakifanya oganaizesheni Za majembe, wakaichimba hii kitu halafue wakaiunguza fasta elekitirisit itapatikana..chezea nshale wewe..!!
 
hivi atakuwa anamkomoa nani?? ila kwa ninavyomfaham huyo bwana, ni ngumu kuamini kama ni kweli maneno hayo yametoka kinywani mwake.....angesema lukuvi (std VII) Nisingekuwa kuwa na shaka sana......:becky::becky:
 
Sishangazwi na kauli ya Simbachaweni. Kwa tabia yeye ni mmoja wa 'liwe na liwe'.Refer kauli zake mjengoni. Atafaidi nini yeye kama wanamtwala watkosa gesi yao waliojaliwa na Mungu. Ni mmoja wa watu hatari sana. He is in my black book.
 
Wanatakiwa waichimbe kwa mikono hii gesi hawa wamakonde.

Ni sawa kabisa hao wamachinga ndivyo walivyo hata ndani ya familia zao wakivuna ufuta au korosho ni mzozo hadi mahakamani na ndoa kuvunjika! sishangai wao kung'ang'ania gesi! Ng'oa tu mitambo tuwaomne ala!
 
Wao wamakonde hawana tatizo, wanamchakato wa kuanzisha nchi yao ambayo itahusisha Mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma na wana Mpango wa kuiita nchi hiyo tarajiwa REPUBLICA DE MAKONDE LAND! wanaandaa proposal ya kuipeleka AU na UN kama ilivyokuwa Sudan Kusini
Simbachawene ang'oe tu hiyo mitambo, wamakonde hawajali! Alikwenda hawa ghasia akagawa bahasha kwa wazee wakala but msimamo pale pale, wanamsubiri Vasco da gama wakale zake!!
 
Kama alivyosema mkuu mmoja hapo juu, nahisi huu mradi ni mojawapo ya mbinu kubwa ya magamba kujipatia kipato cha uchaguzi mwaka 2015!
 
Wao wamakonde hawana
tatizo, wanamchakato wa kuanzisha nchi yao ambayo itahusisha Mikoa ya
Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma na wana Mpango wa
kuiita nchi hiyo tarajiwa REPUBLICA DE MAKONDE LAND! wanaandaa proposal
ya kuipeleka AU na UN kama ilivyokuwa Sudan Kusini
Simbachawene ang'oe tu hiyo mitambo, wamakonde hawajali! Alikwenda hawa
ghasia akagawa bahasha kwa wazee wakala but msimamo pale pale,
wanamsubiri Vasco da gama wakale zake!!

moto2012, kwani kura zao zipo ngapi? acha wasipige tu, na kuanzisha jamhuri ndani ya jamhuri ni uhaini na ubavu huo hawana!
 
Last edited by a moderator:
moto2012, kwani kura zao zipo ngapi? acha wasipige tu, na kuanzisha jamhuri ndani ya jamhuri ni uhaini na ubavu huo hawana!

Hahahahaha! Hata sudan kusini walianza hivyo hivyo! Wana mifano ya nchi ndogo kama Rwanda, Burundi na Cape Verde
 
Back
Top Bottom