barafu
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 6,739
- 32,865
Akiongea na Kipindi cha Clouds360,Waziri wa TAMISEMI anasema ni makosa kwa Mameya wa Wenyeviti wa Halmashauri wa UKAWA hawataruhusiwa kutekeleza sera za vyama vyao sbb sio vilivyounda serikali.
Waziri Simbachawene anasema wote wanaodhani kwa kushinda umeya toka vyama pinzani ni kutekeleza sera za vyama vyao hawajui sheria na taratibu za uongozi katika Serikali za Mitaa.
Sera na ilani itakayotekelezwa na Mameya na Wenyeviti wote wa UKAWA ni ya Chama cha Mapinduzi ambacho ndio kimeshinda uchaguzi na kuunda Serikali.
Simbachawene anasema wanaojidanganya kuwa watatekeleza sera nje ya zile za chama tawala ni sababu ya kutaka kufurahisha genge na wanaongea kihisia tu ili kuwafurahisha wanachama na wapenzi wao wa vyama.
Waziri anazidi kutoa ufafanuzi kuwa kuna utata unaosemwa mitaani kuwa kati ya Meya na Mkuu wa Wilaya ni nani mwenye madaraka ndani ya eneo la kiutawala, Waziri anasema Mkuu wa Wilaya ni juu ya Meya, sababu ndio anamuwakilisha mkuu wa mkoa katika eneo lake la Wilaya na mkuu wa Mkoa anamuwakilisha Rais, hivyo mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya ni waajiliwa wa Serikali kuu na wawakilishi wa moja kwa moja wa Rais, hawawezi kuwa chini ya Meya au Mwenyekiti wa Halmashauri ambao ni viongozi katika muundo wa Serikali za mitaa na wanawajibika kwa Waziri wa TAMISEMI.
Waziri Simbachawene ametumia muda huo kuelezea marufuku ya Mameya kutumia magari ya serikali muda wote,isipokuwa pale tu wanapokuwa wanahitajika kuhudhuria vikao vya "Full Council",amesisitiza kuwa Meya hana kazi zaidi za kumfanya afike mara kwa mara ofisini, kikawaida Meya anaweza fika ofisini mara mbili au tatu kwa juma.
Hivyo Halmashauri za Jiji na Miji zihakikishe Mameya hawatumii vibaya magari ya serikali kwa shughuli zao binafsi kwani hawahitajiki sana kuwepo ofisini kwa nafasi zao za umeya.
Simbachawene ametoa agizo kwa watendaji wote wa Serikali inayoundwa na chama tawala ambacho kimsingi ndio kilichoshinda uchaguzi na kukabidhiwa dola wanahakikisha kuwa wanashirikiana na Mameya wote wa vyama vya upinzani na chama tawala popote nchini kutekeleza "sera na ilani ya Chama cha Mapinduzi"