Simbachawene: Askari wote nchini kuongezewa Posho

Simbachawene: Askari wote nchini kuongezewa Posho

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,129
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema serikali imeanza mazungumzo yenye dhamira ya kuboresha maslahi, ikiwemo makazi na posho kwa askari wote nchini, ili kuboresha mazingira ya kazi pamoja na kuwaongezea ujuzi na utaalamu ili kuendana na mazingira ya sasa ya kiuhalifu, ikiwemo uhalifu wa mitandaoni.

Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Maofisa, Wakaguzi, Askari wa Renk na Faili wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar pamoja na mikoa mitatu ya Unguja.
 
Baada ya kuwaua watanganyika wanataka kuongezana posho?Mimi kama GenZ nitaenda somalia kuichukua mabomu na kuwashughulikia hawa WAHUNI ili na wao waumie kama walivyotuumiza sisi kuwaua wapigania haki29/10/2025
 
Asiumeume maneno.Aeleze tu kwamba ni "shukrani kutoka kwa mama" baada ya kazi nzuri ya kabla,wakati na baada ya "uchafuzi" 2025.Kwamba,katika watumishi wote nchini,ni wao tu wenye uhitaji wa kuongezewa "posho"? Katika utawala, kuanzia Magufuli hadi Samia hao polisi wameshaongezewa posho mara ngapi kwa kulinganisha na watumishi wengine?
 
Waongezewe posho haraka kwa kuwashikisha nyumbu adabu, nyumbu wahalifu walijaribu kufanya unyumbu wa kuchoma nchi na kuiba mali za watu ila wakatulizwa vizuri sana hadi leo hakuna anaetaka kuskia habari ya maandamano uchwara.
 
Posho wataongezewa ili kuendelea kuipigania Chama Tawala na Bado wataendekeza Rushwa na Kunyima watu wa hali chini haki zao....
Na kwanini wao tu waongezewe, na sio pia watumishi wengine wa Umma wa mishahara ya chini na baadhi wasio na posho kabisa kama walimu,manesi na watumishi Halmashauri nk,...
Na hii si ndio itaiongeza zaidi huduma mbovu na rushwa zaidi za ofisi za Umma/serikali km hospitalini,shuleni,ofisi za NIDA,tanesco,mahakamani nk baadhi Yao ndo watazidi kutoa huduma mbovu,Lugha chafu(poor customer care) maana ht morali kazi itashuka kuona polisi na wanajeshi(Wana usalama) tu ndo wanathaminiwa nchi hii na wenyewe wanasiasa.
 
Pesa za laana hata ulipwe milion 10 kwa mwezi zitaishia kupotea zote bila kufanya jambo lolote la maana!, iyo kazi ya upolisi ilishalaaniwa kabisa.
 
Polisi ndo kazi pekee unaamka asubuhi kwenda kugombana na watu ndo upate pesa!, inabidi ugombane nao raia wengi zaidi ili uwe na pesa bila ivo unakosa pesa!, ndio maana wakishastaafu huwa wanaishi maisha flani magumu sana ya kukosa hata marafiki ndio maana hufa mapema!.
 
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene, amesema serikali imeanza mazungumzo yenye dhamira ya kuboresha maslahi, ikiwemo makazi na posho kwa askari wote nchini, ili kuboresha mazingira ya kazi pamoja na kuwaongezea ujuzi na utaalamu ili kuendana na mazingira ya sasa ya kiuhalifu, ikiwemo uhalifu wa mitandaoni.

Ametoa rai hiyo wakati akizungumza na Maofisa, Wakaguzi, Askari wa Renk na Faili wa Makao Makuu ya Polisi Zanzibar pamoja na mikoa mitatu ya Unguja.
hao polisi wa Mitandaoni ndio wanaiba simu mara ya pili! wakishajua simu yako ya bei wanafatilia halafu wanabeba wao
 
Daah posho na maslahi ya wasizwa imemla kichwa Jamaa..
Amna' Kuna kauli aliitoa week iliyopita kuhusu nafikiri ni Maandamano akasema kaagizwa na Anayemuita Rais, ile kauli kuwa kaagizwa haikuwa sahihi....

Next time akumbuke kuepuka kuongea ongea hovyo
 
Duh unajitenga na watu wenye akili, Weredi na Nia ya kweli kulisaidia Taifa, unakumbatia akija Bashite.

Halafu kesho, Utasema kuna watu wanakuhujumu
 
Back
Top Bottom