Kim Il Kwon
JF-Expert Member
- Nov 13, 2015
- 1,219
- 1,034
Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji na Vipindi, Ruge Mutahaba akizungumza leo na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa - TAMISEMI, George Simbachawene mara baada ya kutoka kwenye kipindi cha Clouds360 cha CloudsTv.
Waziri wa Tamisemi George Simbachawene asema ajira za walimu zitatoka baada ya bajeti kupita kuepuka mishahara kucheleweshwa.
Simbachawene ameyasema hayo leo kupitia kituo kimoja maarufu cha redio nchini. Kwa miaka mingi ajira zimezoeleka kutoka mwezi Februari mpaka mwishoni mwa mwezi Machi japo mara chache zilikuwa zikizidi kidogo.