Simba yawakana wa TFF

JuaKali

JF-Expert Member
Nov 14, 2007
776
118
Klabu ya soka ya Simba, imewaonya wapiga kura wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kuwa makini na baadhi ya wagombea waliojitokeza kwenye kinyang`anyiro cha uchaguzi wao mkuu utakaofanyika mwezi ujao.

Katibu Mwenezi wa klabu hiyo, Seydou Rubeya, alisema kuwa wapo baadhi ya wagombea waliojitokeza si kwa nia ya kuleta maendeleo ya soka nchini na hivyo ni fursa ya wapiga kura wa TFF kuchagua chuya na mchele.

Seydou alisema wapo wagombea waliojitokeza kuomba ridhaa ya kuiongoza TFF kwa nia ya dhati ya kuleta maendeleo, lakini wapo wengine waliojitosa kwa lengo la masilahi yao binafsi na hivyo ni wasaa wa wapiga kuwa makini.

``Tayari wapo wanaohisi ndani ya TFF kuna fedha na hivyo wanajitokeza kwa nia ya maslahi na sio maendeleo ya soka, hivyo ni wasaa wa wapiga kura kufanya kweli kwa kuwachagua wanaoamini wataipeleka Tanzania mbele,``

Mwenezi huyo alisema na kuongeza pia kwa kuwaonya baadhi ya wagombea waliojitokeza kupitia mgongo wa klabu ya Simba kutoihusisha harakati zao na klabu kwa vile hawajaridhiwa na Kamati yao ya Utendaji.

``Kwa kawaida kamati inaweza kukutana na kupendekeza mtu wa kugombea kwa niaba ya klabu yetu, lakini wengi waliojitokeza wameenda kwa matakwa yao na hivyo wasiihusishe Simba kwa namna yoyote,`` Seydou alisema.

Kinyang`anyiro cha uchaguzi mkuu wa TFF unatarajia kufanyika Desemba 14 na tayari wagombea kadhaa wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa shirikisho hilo wengi wakitoka klabu za Simba na Yanga
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom