Simba yapokwa pointi za Azam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Simba yapokwa pointi za Azam

Discussion in 'Sports' started by JuaKali, Apr 1, 2009.

 1. JuaKali

  JuaKali JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 785
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limeipokonya timu ya Simba ya Dar es Salaam ushindi wa pointi tatu na mabao matatu ilioupata juzi katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Azam FC, ikidaiwa kumchezesha Haruna Moshi mwenye kadi mbili za njano.

  Habari zilizopatikana jana kutoka ndani ya TFF, zilieleza kuwa uamuzi huo ulifikiwa kwenye kikao cha Kamati ya Mashindano ya TFF kilichofanyika mapema jana kwenye ofisi za shirikisho hilo, Uwanja wa Karume, Ilala, Dar es Salaam.

  "Kesho (leo), Kaijage (Florian-Ofisa Habari wa TFF), atatoa taarifa rasmi kwa waandishi, lakini tayari uamuzi umeshafikiwa, maana ni suala ambalo liko wazi kwamba Haruna ana kadi mbili za njano. "Viongozi wa Simba wanalijua hilo, wameshapewa taarifa na hata ukiwasiliana nao watakueleza," kilisema chanzo chetu cha kuaminika bila kutaja michezo ambayo Moshi alipewa kadi hizo.

  Katibu Mkuu wa Simba, Mwina Kaduguda alipoulizwa jana hakuwa tayari kuzungumzia suala hilo zaidi ya kusema naye amezisikia, huku akisisitiza kama ni wa kweli TFF imechukua uamuzi huo itakuwa imekurupuka na kuwa nia yao ni kuwazuia wasitwae nafasi ya pili.

  Kwa upande wake Kaijage alisema hajui lolote na asingeweza kuzungumza kwenye simu jambo hilo, badala yake akashauri atafutwe Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Ramadhan Nassib ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya TFF, ambapo alipoulizwa alikiri kamati yake kukutana jana kujadili mambo mbalimbali. "Ni kweli kuna mambo yamejadiliwa likiwamo hilo la Simba, hivyo saa tatu asubuhi kesho (leo), nitazungumza na waandishi ofisi za TFF, kila kitu kitawekwa wazi," alifafanua Nassib.

  Kutokana na uamuzi huo wa TFF, Simba ambayo ilishinda mabao 3-0 katika mchezo huo uliofanyika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam na kufikisha pointi 30 ikishika nafasi ya pili, sasa imebaki nafasi yake ya tano ikiwa na pointi 27. Nafasi ya pili sasa inashikwa na Mtibwa Sugar yenye pointi 28, sawa na Kagera Sugar na Prisons, lakini timu hiyo ina uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa, huku Prisons ikishika nafasi ya tatu na Kagera ya nne.

  Timu zote zimebakisha michezo minne kumaliza ligi hiyo, hivyo Simba sasa imejiweka katika mazingira magumu ya kutwaa nafasi ya pili, ambayo ingeiwezesha kushiriki michuano ya Kombe la Shirikisho mwakani. Yanga tayari imeshatwaa ubingwa huo. Mwaka 2006 Simba ilinyang'anywa pointi katika mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, baada ya kudaiwa kumchezesha Mussa Hassan 'Mgosi' aliyekuwa na kadi tatu za njano.

  Pia mwaka jana Simba ilipokwa pointi tatu na Kamati ya Mashindano ya TFF kwa madai ilimchezesha Juma Nyosso aliyekuwa amefungiwa na shirikisho hilo kucheza soka kwa miezi mitatu Novemba mwaka juzi, akidaiwa kumpiga kiwiko mchezaji wa Toto African katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, wakati huo akichezea Ashanti United. Nyosso alisajiliwa Simba katika dirisha dogo la usajili siku chache baada ya kuanza kutumikia adhabu yake, ambapo Simba ilimtumia katika mchezo dhidi ya Coastal Union.

  Wakati huohuo, habari zilizopatikana jana jioni wakati tukienda mitamboni ni kuwa aliyepata kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa TFF, Ismail Rage amepitishwa kuwa Katibu Mkuu mpya wa kuajiriwa wa Simba. Kulingana na chanzo chetu, Rage ameshakamilisha taratibu zote na anatarajiwa kuanza kazi leo makao makuu ya klabu hiyo mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam saa mbili asubuhi.

  Rage imeelezwa kuwa ameikwaa nafasi hiyo kutokana elimu yake na uzoefu wake mkubwa katika soka, ambapo amepata pia kuwa Katibu wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), pia Katibu Mkuu wa TFF wakati huo ikiitwa FAT. Simba kwa muda mrefu ilikuwa katika mchakato wa kutafuta Katibu wa kuajiriwa. Leo ni Siku ya Wajinga.
   
 2. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Nafikiria tu gharama ya space kwenye gazeti + muda/malipo ya kuandika hii 'habari'.
   
 3. Next Level

  Next Level JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Nov 17, 2008
  Messages: 3,159
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Was too long for the fools!
   
 4. MpigaFilimbi

  MpigaFilimbi JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 133
  .....But who are the fools?
   
 5. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwanza ni walioiandika wenyewe kwa sababu wameshindwa kuwadanganya walengwa
   
 6. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Walioandika ndio Wajinga kwa sababu

  1: Wanaamini kwamba Simba hawawezi kunyang'anywa points kwamba there is no way out yani

  2: Wanaamini kwamba Rage hawezi kuwa Katibu mkuu Simba, kwamba Rage amefungiwa Kuongoza Simba Maisha.
   
 7. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #7
  Apr 1, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...ingekuwa 'kandambili' ndio wameiambiwa habari hii weeeeeeeeeee...pangekuwa hapatoshi hayo mawe yake, machungwa, nyanya na maembe ambayo yangerushwa leo mjini! ..si mnawajua walivyo waswahili waswahili na matenga yao kuanzia feri, sokoni mpaka mnadani...:D:D:D
   
Loading...