Simba yapigwa na watotot wa oman

Simba yapigwa na watotot wa oman

simba wamefungwa na timu ya waosha vyombo na wafua mashuka wa Hotel
 
Source radio1 imepigwa 1:0 leo.

Mfumo wa mpira wetu umetengeza mashabiki wa kipekee sana duniani. Mashabiki ambao wako radhi kukiita au kukipa kitu sifa zisizostahili ili mradi wafurahishe nafsi zao. Kwa mfano, Watanzania ni wagumu sana kukubali kuwa timu inaweza kufungwa kwa kuzidiwa uwezo! Lazima tutafute visingizio hata vile vya kitoto kabisa, mara refa, mara rushwa ma hujuma ili mradi kuukana ukweli.

Watu kubishana na kucharuana ni kitu cha kawaida lkn kufikia mahali kulishana uongo uliopitiliza hakufai kitu.

Kwa mfano Yanga kufungwa na timu ya daraja la kwanza uturuki sio ajabu kabisa. Kwanza ni ukweli usiopingika kuwa Uturuki iko juu kimpira. Pili timu yenyewe pamoja na kuwa daraja la kwanza inaweza kuwa katika fomu ya hali ya juu. Pia Yanga inaweza kuwa ilikuwa off-form ('au kukosa bahati'). Lakini kubwa zaidi, mechi za kirafiki ni kwa ajili ya kujifunza mbinu mpya, na sio kutafuta matokeo.

Vivyo hivyo Simba kufungwa na timu ya taifa ya Oman chini ya miaka 23 haiwezi kuwa ajabu. Taifa stars yetu sasa hivi ina wachezaji ambao wastani wa umri wao ni miaka hiyo hiyo 23! Sasa mtu hafaidiki chochote kwa kubadilisha eti simba imefunwa na timu chini ya miaka 17! Na hata hivyo simba isifungwe kwa nini?

Lakini kubwa zaidi wakati sisi mashabiki tunasubiri matokeo ya mechi ili tuzodoane, makocha wana kitu kingine kabisa wanachotafuta, nani acheze na nani, timu ishambulie vipi, n.k. Tuziache timu zijiandae kwa sababu kwa kweli timu zetu huwa hazina maandalizi mazuri kabla ya mashindano
 
Mnyama kalambwa thalatha leo Oman

SIMBA YATANDIKWA 3-1 OMAN, BOBAN APIGA L:A KUFUTIA MACHOZI

MABIGWA wa Ligi Kuu ya Vodacom, Simba SC wameendelea kufanya vibaya katika michezo yao ya kirafiki nchini Oman baada ya leo kutandikwa mabao 3-1 na timu ya ya Qaboos,katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Qaboos nchini Oman.

Kwa mujibu kocha wa zamani wa Simba mwenye makazi yake nchini Oman, Talib Hilal alisema licha ya kipigo hicho, Simba ilionesha kandanda safi na ya kuvutia, huku bao la kufutia machzi la Simba lilipachikwa na mshambuliaji, Haruna Moshi ‘Boban’.

Simba ambayo ipo huko tangu wiki iliyopita, kwa kambi maalum ya kujiandaa mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Vodacom pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika, juzi ilitandikwa bao 1-0 na timu ya taifa ya soka ya Oman chini ya umri wa miaka 23.
Aidha, Simba inayonolewa na Patrick Liewig inatarajiwa kucheza mechi nyingine ya kirafiki na Fanja Fc, kabla ya kurejea nchini Januari 23 tayari kwa kuanza mzunguko wa pili wa Ligi unaotarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 26.​
 
huko wamefata nini kama wanapigwa na timu za hovyo kama hizi
 
Back
Top Bottom