Simba yaondoka kwa mafungu mafungu kwenda Misri? Nini shida

Hustler_

Member
Jan 17, 2022
42
41

Simba yaondoka kwa mafungu mafungu kwenda misri? Nini shida​

Kikosi cha Simba kimeondoka nchini leo Julai 14 mchana kwenda nchini Misri huku katika msafara wao walikuwepo wachezaji 19, benchi la ufundi pamoja na kiongozi mmoja ambaye ni Meneja wa habari na mawasiliano Ahmed Ally.

Wachezaji walioondoka walikuwepo, Shomari Kapombe, Ally Salim, Benno Kakolanya, Gadiel Michael, Erasto Nyoni, Pape Sakho, Chris Mugalu, Augustine Okrah, Meddie Kagere, Jimson Mwanuke, Victor Akpan na Habibu Kyombo.

Wengine, Clatous Chama, John Bocco, Israel Mwenda, Joash Onyango, Henock Inonga na wengine wawili ambao hawakuonekana.

Kocha msaidizi wa Simba, Selemani Matola alisema katika muda wao wa maandalizi ya msimu ujao watafanya mazoezi aina mbalimbali pamoja na kucheza mechi za kirafiki.

Matola alisema ndani ya wiki ya kwanza tu watacheza mchezo mmoja wa kirafiki kutokana na ratiba ya kocha mkuu, Zoran Maki ilivyo.

“Timu itakuwa Misri kwa makundi matatu la kwanza ndio hili la leo, lingine ni wale ambao viza zao zimechelewa kutoka na kundi la mwisho litakuwa wale waliopo kwenye kambi ya Taifa Stars,” alisema Matola.

Baada ya kambi ya huko Misri kikosi cha Simba kitarejea nchini Agosti 5, kwa ajili ya maandalizi wiki ya Simba pamoja na mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya watani zao Yanga utakaopigwa Agosti 13, Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Source: vanforumtz.com
 
Mzee ni kwamba nawe umefosi ulete uzi ama, unauliza swali ambalo jibu lipo kwenye uzi wako,

Wameemda kwa makundi sababu, kuna ambao viza zimechelewa, kundi la pili, kuna ambao wapo kambi ya NESHNO TIM kundi la tatu, sasa hapo shida iko wapi? Au mimi ndio sijasoma vizuri uzi wako?
 
Simba yaondoka kwa mafungu mafungu kwenda misri? Nini shida

“Timu itakuwa Misri kwa makundi matatu la kwanza ndio hili la leo, lingine ni wale ambao viza zao zimechelewa kutoka na kundi la mwisho litakuwa wale waliopo kwenye kambi ya Taifa Stars,” alisema Matola...
Yanga mnazidi kuonyesha ujinga wenu. Sasa unauliza swali kwenye title, halafu unatoa jibu kwenye maelezo. Sisi tufanye kitu gani sasa?
 
Sasa hapo ndo nini!!

Umeuliza harafu ndani umetoa majibu!! Aisee inashangaza sana
 
  • Thanks
Reactions: BRN
Mafungu kama ya nyanya sio?
Si tulikubaliana pre season itakuwa kule kwa mzee biden?

Kumbe ni huko kwa firauni? Tusishangae bocco akarudi hana rinda
 
Mzee ni kwamba nawe umefosi ulete uzi ama, unauliza swali ambalo jibu lipo kwenye uzi wako,
Wameemda kwa makundi sababu, kuna ambao viza zimechelewa, kundi la pili, kuna ambao wapo kambi ya NESHNO TIM kundi la tatu, sasa hapo shida iko wapi? Au mimi ndio sijasoma vizuri uzi wako?
Amechanganyikiwa huyoo, achana nae,
 
simba wakishaamua kumpenda mtu huwa hawaambiwi hawasikii, hawa wazee bado wapo?

Mkuu iko hivi, viongozi walitaka wapitishe panga pale kikosini Kocha mkuu alikataa hadi pale atakapowaona wachezaji wote halafu ataandaa repoti nani abaki nani aachwe.

Umeelewa??

Mugalu anaweza akabaki kwa sababu ya muonekano wake, ila Kagere sidhaaaani!!
 
kuuliza wananchi wenzako haina shida ila kuuliza watani kuhusu mbwembwe imekuwa nongwa!
 
Back
Top Bottom