Simba yampa kibali Said Ndemla kufanya majaribio Sweden

MASTER291

Member
Nov 4, 2017
6
0
Simba imetangaza kumpa ruhusa kiungo wake Said Hamis Ndemla kwenda kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa nchini Sweden

Taarifa rasmi kutoka Simba imethibitisha kiungo wao mshambuliaji Said Hamisi ‘Ndemla’ anaondoka kesho kwenda Sweden kufanya majaribio ya kucheza soka la kulipwa.

Atafanya majaribio hayo kwenye klabu ya AFC Eskilstuna inayoshiriki ligi kuu nchini Sweden. Majaribio hayo ni ya wiki mbili (siku 14).

Msemaji wa Simba, Haji Manara amesema ni utamaduni wa Simba kuwapa nafasi wachezaji waliopata nafasi ya majaribio.

"Kama ilivyo kawaida ya Simba, tumetoa nafasi kwa Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio," alisema.

Miezi kadhaa iliyopita, Simba ilimzuia Ndemla kwenda Sweden kufanya majaribio katika timu hiyo kwa madai taratibu hazikuwa zimefuatwa.

Eskilstuna ndio klabu ambayo anakipiga mtanzania mwingine Thomas Ulimwengu ambaye kwa sasa anauguza jeraha la goti baada ya kufaniwa upasuaji.
TAZAMA VIDEO HII

TANZANIA INAPAA
 
Halafu liOmog linamuingiza dogo dk 90,simpendi hyu kocha,anaua vibaya vya madogo.hebu cheki alivyotaka kumuharibia mkude
 
Bora aende huko kwa wanaojuwa thamani ya Mchezaji kuliko kuendelea kusota huku wanakojuwa thamani ya Majungu kuliko mchezaji..,
 
Halafu liOmog linamuingiza dogo dk 90,simpendi hyu kocha,anaua vibaya vya madogo.hebu cheki alivyotaka kumuharibia mkude
Omog hafai kuwa pale na hajawahi kuwa kocha mzuri toka akiwa Azam FC ... Ndemla & Mkude ni wachezaji wenye ubora wa hali ya juu pale Simba SC cha kushangaza amekuwa kama ana chuki nao..
 
Back
Top Bottom