Simba vs Yanga (shairi: utani wa jadi)

Kajole

JF-Expert Member
Apr 12, 2011
1,667
1,642
SHAIRI

UTANI WA JADI YANGA NA SIMBA

Leo siku imefika
Siku tuliyoitaka
Mwali wetu atatoka
Bikira tutamtoa

Ukweli ninatamka
Malengo tuliyaweka
Kwa mwali kumualika
Tupate jifaidia

Msimbazi ametoka
Gauni amejivika
Umbo lake kaanika
Vidume kutamania

Na Yanga pasipo shaka
Mahaba kayatamka
Demu Simba nakutaka
Uroda kunipatia

Manara akatamka
Ipo siku itafika
Nitakupa ulotaka
Hadi raha kusikia

Leo sasa imefika
Ahadi twaikumbuka
Uroda tunautaka
Taifa twakungojea

Uje huku warembeka
Macho yako kurembuka
Mashine tumeiweka
Yasubiri kukoboa

Kiunoni kujivika
Mapambo sitotamka
Wayajua pasi shaka
Ashiki kutuletea

Mabao ya uhakika
Matatu uliyotaka
Ubikira kukutoka
Uroda kuuachia

Kidile mwali kivika
Leo mwali anatoka
Yanga tutafurahika
Kichuna kujipatia

Mwisho hapa nimefika
Utani kuuandika
Mapovu sitoyataka
Utani ni asilia.
 
Kama mpira huwezi
Kucheza ukachezeka
upewe hata penati
Hata mpira wa kona
utacheza upuuzi
hadhira kukutukana.

Upewe hata na messi
Na kocha upewe wenga
kupata ushindi kazi
kama hujui namna
yatakutoka mashuzi
ubaki kugunaguna.
 
SHAIRI

UTANI WA JADI YANGA NA SIMBA

Leo siku imefika
Siku tuliyoitaka
Mwali wetu atatoka
Bikira tutamtoa

Ukweli ninatamka
Malengo tuliyaweka
Kwa mwali kumualika
Tupate jifaidia

Msimbazi ametoka
Gauni amejivika
Umbo lake kaanika
Vidume kutamania

Na Yanga pasipo shaka
Mahaba kayatamka
Demu Simba nakutaka
Uroda kunipatia

Manara akatamka
Ipo siku itafika
Nitakupa ulotaka
Hadi raha kusikia

Leo sasa imefika
Ahadi twaikumbuka
Uroda tunautaka
Taifa twakungojea

Uje huku warembeka
Macho yako kurembuka
Mashine tumeiweka
Yasubiri kukoboa

Kiunoni kujivika
Mapambo sitotamka
Wayajua pasi shaka
Ashiki kutuletea

Mabao ya uhakika
Matatu uliyotaka
Ubikira kukutoka
Uroda kuuachia

Kidile mwali kivika
Leo mwali anatoka
Yanga tutafurahika
Kichuna kujipatia

Mwisho hapa nimefika
Utani kuuandika
Mapovu sitoyataka
Utani ni asilia.
Nimependa ulivyo malizia...Kipaji unacho mkuu...
 
Back
Top Bottom