Habari zilizonifikia punde toka kwa jamaa zangu waliopo mkoani Singida ni kwamba timu ya Simba sc ambayo leo inategemea kupambana na wapinzani wao wa jadi Yanga,imepata mkosi mara baada ya gari lao walilotumia kusafiria toka Manyoni walikopiga kambi ya siku moja kuharibika.Ikabidi juhudi zifanywe na mbunge wa Singida mjini Mohamed Dewji na kuweza kupata usafiri mwingine wa costa iliyoandikwa CHAMI TRANS inayomilikiwa na Dr.Cyril CHAMI ambayo hufanya safari za DODOMA SINGIDA na kuwawezesha kuondoka majira ya saa 2 asubuhi hii.Na taarifa niliyoipata hivi sasa tayari wameshaingia IGUNGA wakiitafuta NZEGA.
Kwa mujibu wa mtoa ripoti wetu,timu ya Simba walikuwa Manyoni kufuatia kamati ya ufundi kubaini kuwa mambo yalikuwa hayajakamilika nje ya uwanja.
Kwa wale wanaongalia hiyo mecho watupe list ya wachezaji kwanza
hilo nalo neno
sawa PwezaJamani TBC1 hawaonyesha maana huku kwetu tena Dar local channels hazishiki kabisa, mie local huwa natazama TBC1 through DSTV otherwise itabidi niende kwenye baa mbali kidogo nahuku nikacheki mtanange huu laini kwa watoto wa Jangwani kumchapa mnyama asiye na meno 3-1
kulingana na maelezo yako ufafanuzi kidogo hapo kwenye red na bluemi naona Startv wako vizuri kuliko tv station yoyote hapa Tanzania yaani (ITV,TBC na STARTV) na swala la kutokuonyesha baadhi ya mechi za Uingereza ni swala la kimikataba sidhani kama wamepewa haki ya kuonyesha mechi zote..
kwenye black hapo mkuu!Manake tulipewa list ya wachezaji kibao wa Simaba hapa kuwa hawatocheza mechi ya leo