Simba vs Yanga Okt 16, 2010

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Mtanange wa watani wa jadi Kati ya SIMBA na YANGA utakaopingwa Jmosi utaonyweshwa moja kwa moja (live) na kituo cha Startv kuanzia saa 10 jioni, timu zote zimejinasibu kuwa zimefanya maandalizi mazuri hivyo tutegemea mtanange wa kufurahisha kwani safari hii yanga wametokea Bagamoyo wakati Simba waliweka kambi yao pale Tabora na Mwanza simba kuna kila dalili za kumkosa salum Kanoni, Mohamed Simba Banka,Uhuru Seleman, Musa Hasan Mgosi, Hilary Echesa na kapteni wa wao Nicodemus Nyangawa walio majeruhi kwa upade wa watani wao yanga watamkosa Kenneth Asamoah raia wa Ghana ambae haja pata ITC

mwenye habari zaidi juu ya kinacho endelea atujuze maana mechi hizi huwa na vituko na vijambo
 
Simba waliweka kambi yao pale Tabora na Mwanza simba kuna kila dalili za kumkosa salum Kanoni, Mohamed Simba Banka,Uhuru Seleman, Musa Hasan Mgosi, Hilary Echesa na kapteni wa wao Nicodemus Nyangawa

Kama ni hivyo basi Yanga wacheza na Simba B (almost)
 
STAR TV KWA KWELI WANATUYUMBISHA AY NISEME WANAWAYUMBISHA WANANCHI, MAANA WALIKUJA NA MKWARA MZITO JUU YA eapl LAKINI UONYESHAJI WA MECHI HIZO UMEKUWA WA KUSUASUA, WAKAPEWA HAKI ZA KUONYESHA TANZNIA PL lakini bado hawajaonyesha mechi yoyote(kwa ufahamu wangu) sasa kesho wasije wakawafanya watu wawe glued to their TVs then wakasema ooh kutokana na matatizo ya kiufundi hatujaweletea mechi hiyo

ni angalizo tuuu!!!
 
sijui kama wataonyesha,star tv, na kwanin wameng'ang'ania hii tender ya kuonyesha wakati hawana uwezo
 
walisema Kufungwa kwa uwanja wa Uhuru uliwahalibia mipangilio yao maana walitegemea wangekuwa dar maana gari lao la matangazo ni garama kubwa kulitoa kituo kimoja kwenda kingine ndiyo maana wakasema wataonyesha mechi mhimu tu, Kesho watakuwa na mechi Tatu Mechi ya marudia kati TZ na Morroco (2PM) ikifatiwa na Simba na Yanga (4PM) na ya mwisho ligi ya uingereza kati ya FUllham Tottenham...
 
sijui kama wataonyesha,star tv, na kwanin wameng'ang'ania hii tender ya kuonyesha wakati hawana uwezo
mi naona Startv wako vizuri kuliko tv station yoyote hapa Tanzania yaani (ITV,TBC na STARTV) na swala la kutokuonyesha baadhi ya mechi za Uingereza ni swala la kimikataba sidhani kama wamepewa haki ya kuonyesha mechi zote..
 
Mtanange wa watani wa jadi Kati ya SIMBA na YANGA utakaopingwa Jmosi utaonyweshwa moja kwa moja (live) na kituo cha Startv kuanzia saa 10 jioni, timu zote zimejinasibu kuwa zimefanya maandalizi mazuri hivyo tutegemea mtanange wa kufurahisha kwani safari hii yanga wametokea Bagamoyo wakati Simba waliweka kambi yao pale Tabora na Mwanza simba kuna kila dalili za kumkosa salum Kanoni, Mohamed Simba Banka,Uhuru Seleman, Musa Hasan Mgosi, Hilary Echesa na kapteni wa wao Nicodemus Nyangawa walio majeruhi kwa upade wa watani wao yanga watamkosa Kenneth Asamoah raia wa Ghana ambae haja pata ITC

mwenye habari zaidi juu ya kinacho endelea atujuze maana mechi hizi huwa na vituko na vijambo

Umepata Authority ya kudhibitisha kuwa mechi hiyo itarushwa live Startv? tupe majibu ili tuwe na uhakika.
 
Habari zilizonifikia punde toka kwa jamaa zangu waliopo mkoani Singida ni kwamba timu ya Simba sc ambayo leo inategemea kupambana na wapinzani wao wa jadi Yanga,imepata mkosi mara baada ya gari lao walilotumia kusafiria toka Manyoni walikopiga kambi ya siku moja kuharibika.Ikabidi juhudi zifanywe na mbunge wa Singida mjini Mohamed Dewji na kuweza kupata usafiri mwingine wa costa iliyoandikwa CHAMI TRANS inayomilikiwa na Dr.Cyril CHAMI ambayo hufanya safari za DODOMA SINGIDA na kuwawezesha kuondoka majira ya saa 2 asubuhi hii.Na taarifa niliyoipata hivi sasa tayari wameshaingia IGUNGA wakiitafuta NZEGA.
Kwa mujibu wa mtoa ripoti wetu,timu ya Simba walikuwa Manyoni kufuatia kamati ya ufundi kubaini kuwa mambo yalikuwa hayajakamilika nje ya uwanja.
 
Mwaka huu Startv wamezoea kutuonyesha marudio ya mechi na si mechi za moja kwa moja!
 
Jamani TBC1 hawaonyesha maana huku kwetu tena Dar local channels hazishiki kabisa, mie local huwa natazama TBC1 through DSTV otherwise itabidi niende kwenye baa mbali kidogo nahuku nikacheki mtanange huu laini kwa watoto wa Jangwani kumchapa mnyama asiye na meno 3-1
 
Hainivutii kuangalia soka ya kiwango cha chini, na hivi Maximo ameondoka ndio basi tena. Tunarudi kwenye kichwa cha mwendawazimi, yes huwa kinaanzia kwenye klabu.
 
Kambi ya siku moja Manyoni ya nini? Kama sio mambo yaleeee yanaturudisha nyuma kwenye soccer. Kwa ninavyojua timu inatakiwa iende kufanya mazoezi mepesi siku moja kabla au siku ya mchezo asubuhi kwenye uwanja watakaochezea mechi ili wauzoee. Simba badilikeni ili soccer letu likue acheni mambo ya ajabu
 
hahahaha hahahaha
kamati za ufundi zina nguvu kubwa sana mpaka kwenye kampeni za uchaguzi za chama fulani
 
kwa mtaji huu leo sijui kama mnyama atatoka; haya ni mambi ya kienyeji sana wasafiri kwa basi zaidi ya masaa 7 barabara yenyewe ilivyo jaa matutat harafu wacheze???!!!!!! toba!!!
 
Watani acheni "fujo"..tutawafunga kiungwana 2-0
naamini bakora hazitatembea msimbazi..:biggrin1::biggrin1::biggrin1:
 
Walishwa zidiwa wiki moja kabla leo ni kipigo tu sijui Star TV wataonyesha?
 
Back
Top Bottom