Tisha-TOTO
JF-Expert Member
- Feb 10, 2010
- 1,175
- 604
Simba wameanza kuchoka yanga wameanza kuonana.
Dakika chache zilizopita nilikuwa nasikiliza Capital Radio walikuwa na Simba v Yanga match preview programme. Mmoja wa wachangiaji waalikwa alikuwepo "Dk" Uwesu ("mtaalamu" wa tiba asilia na mtabiri wa nyota).
Nanukuu hapa chini alichokisema "Dk" Uwesu...
"Utabiri wa mechi ya Simba na Yanga ni mgumu sana. Lakini hadi dakika hii inaonyesha Simba 2 na Yanga 1. Hata hivyo, kwa kawaida Jumatano huwa ni siku ambayo hutawaliwa na rangi ya njano. Hii maana yake nini? Tafsiri yake ni kwamba Simba watatawala sana mwanzoni mwa mchezo lakini Yanga nao watatawala sana mwishoni mwa mchezo na hivyo kinyota matokeo ya mchezo yatageuka kuwa Simba 1 Yanga 2"
Uwanja umejaa sana
pole muda bado sana dk. 27Yanga wanataka kuniharibia siku.
Kama Mshabiki wa Simba naona Yanga wanacheza Gonga safi Simba tunakimbia tu na mpira bila kuangaliana na Ngassa anao anao sana lazima tuzitoe pasi na tusikae sehemu moja.
Kama Mshabiki wa Simba naona Yanga wanacheza Gonga safi Simba tunakimbia tu na mpira bila kuangaliana na Ngassa anao anao sana lazima tuzitoe pasi na tusikae sehemu moja.
SHAME MAN simba kitu gani pale tumefanya mtu mpira unao uweke mguuni jaribu kwenda sasa kajiangushia nini hawa ndio wanatuharibia sasa Simba.
We endelea kuwapa uchuro tuYanga yasawazisha
Yanga wanataka kuniharibia siku.
Ndoto?Yanga yasawazisha
Wanabodi, niko mahali, naangalia mechi, SS!, kusema ukweli, hizo kamera zinazotumika hapo, ziangalieni hivyo hivyo tuu, Tanzania hatuna hata kituo kimo cha TV chenye hata nusu ya quality ya kamera hizo!.
By the way , nimemuona mtangazaji binti kidoti wa SS na Florian Kaijage, kiukweli wako juu!.
Hapa nilipo, maeneo fulani ukanda wa Gaza (ya bongo), baada ya Simba kufanya mambo, ukumbi mzima ulishangilia as if wote hapa ni washabiki wa Simba!. Katikati ya ushangiliaji, kuna mwendawazimu mmoja akachomekea "nani CCM?", ukumbi wote kimya!, jee inawezekana Yanga ni CCM halafu Simba ni ..., no wonder kwa nini naipenda Simba!.
P.
Hahahahaa!! Politiki everywhere.Wanabodi, niko mahali, naangalia mechi, SS!, kusema ukweli, hizo kamera zinazotumika hapo, ziangalieni hivyo hivyo tuu, Tanzania hatuna hata kituo kimo cha TV chenye hata nusu ya quality ya kamera hizo!.By the way , nimemuona mtangazaji binti kidoti wa SS na Florian Kaijage, kiukweli wako juu!.Hapa nilipo, maeneo fulani ukanda wa Gaza (ya bongo), baada ya Simba kufanya mambo, ukumbi mzima ulishangilia as if wote hapa ni washabiki wa Simba!. Katikati ya ushangiliaji, kuna mwendawazimu mmoja akachomekea "nani CCM?", ukumbi wote kimya!, jee inawezekana Yanga ni CCM halafu Simba ni ..., no wonder kwa nini naipenda Simba!.P.