Simba vs Yanga msimu wa 2020/2021: Sijaona sababu ya mechi kusogezwa mbele

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu Habari za saizi.

Aibu ya jana mechi kuahirishwa aisee inaonesha viongozi wetu hawana weredi kwenye kuongoza mpira ndio maana miaka yote soka letu lipo pale pale tu.

Adjustments.jpg


kwenye taarifa yao hapo sijaona sababu zaidi ya kusema tu imepokea kutoka kwa wizara,nini kilikuwa kina fichwa hapo?

Maana nakumbuka wakati tunafundishwa kinge unaambiwa ukiambiwa why lazima uanze na because.

Sasa sisi huku mechi inapelekwa mbele bila sababu .sababu Inaonesha sio ya msingi ndio maana imefichwa?

Juzi tumeona hapo kwa Man U na Liverpool mechi imeahirishwa sababu ziko wazi kabisa kila timu imekubali ahaaa sawa.

Nadhani wangesema sababu, na sababu ingekuwa na uzito, yanga wangecheza hiyo saa moja lakini huna sababu(usemi sababu) Halafu unataka watu wacheze.

Wangesema sababu kila mtu uenda wangeona sawa huwezi kucheza mpira na wakati uwanjani labda bado hauko vizuri hata Yanga wenyewe wangekubali tu, hata kanuni kama zimevunjwa lakini wewe usemi sababu halafu unataka watuwafate tu na wakati umevunja kanuni za mchezo.

Me nilisikia eti jenereta zimezingua sasa kutumia umeme gharama sana,walikuwa bado wanazitengeneza.

Nyingine nikasikia hii eti mwinyi anazindua kitabu,nikabaki na maswali tu kichwani.

Kingine nikasikia eti mheshimiwa raisi alikuwa anataka afturu kwanza ndio aje kuangalia mpira na yeye.

Anaejua sababu za kusogezwa mbele mchezo wa simba na yanga na uwe saa moja baada ya saa kumi na moja atujuze.
 
Kuna mtu yuko nyumba nyeupe hana habari na footballu. Wala haimhusu. Subirini onyesho la sauti za busara ndo mtaona anademka.
 
Back
Top Bottom