LwandaMagere
JF-Expert Member
- Mar 15, 2020
- 264
- 2,490
Kwa mimi naona tiger is better
Huyu tiger anauwezo wa kuingia kwenye mto na kumchukua mamba akiwa mle mle kwenye maji jambo ambalo sio rahisi ukizingatia na kwamba nguvu ya mamba ni maji lakini si kwa chui
Halafu hata skills za uwindaji chui yuko vizuri zaidi, kama silaha basi naweza kumfananisha na AK47 wakati simba namfananisha na gobole
Action za chui ni noma hadi ndege anawinda, yani anajiviringa juu huko huko aliko ndege kisha anamdaka kwa mikono kama mtu
Simba dume ndo kabisa hata kuwinda halijui lenyewe kula kulala tu kazi zote limemuachia shemu
Upo sahihi ndugu. Ni juzi tu niliona jaguar akiwinda majini kwa kumkaba nyuma ya shingo alligator.Sidhani kama uko sahihi huyo unaemsema wewe anaitwa jaguar [emoji249] anapatikana marekani ya kusini huyo unaemuita mamba ni alligator [emoji246] ... tiger kwa asili anapatikana Asia ... na kwa taarifa tu hakuna mnyama anaeweza kufanya huo upumbavu wa kuwinda mamba mtoni ( the strongest bite on earth [emoji288] ) Hakuna mnyama anaeweza kuwinda hawa jamaa nile crocodile au salt crocodile labda alligator they’re more like lizards than mazafaka crocs
huyo unaemuita mamba ni alligator 🐊
Nimependa maelezo haya. Yamechambua vizuri nguvu na udhaifu wa kila mmoja katika aina hizi za paka. Ni kweli Simba hana mzaha linapokuja suala la kupambana. Huwezi ukamtoa nduki kama unavyoweza kufanya kwa Tiger and the like. Utamuua akijilinda huku akitafuta uwezekano wa kukumaliza na weweSimba sio mkubwa kama Tiger
Kiasili Tiger wanapatikana Asia na Ulaya Mashariki ambayo ni Russia na Tiger wakubwa kbsa wanapatikana Siberia
Tofauti na wa india na kadhalika
Kwenye sifa za kuwinda
Simba ndio paka ambao wanawinda kwa ushirikiano tofauti na jamii nyingine ya paka
Kwenye kupiga simba Tiger wa umri mmoja
Kwanini simba atashinda na Tiger atashindwa
Simba anapigana kwa kutumia mguu mmoja wa mbele na kusimama kwa mitatu iliyobaki wakati Tiger yeye anapigana kwa miwili kwa wakati mmoja na miwili ya nyuma anasimamia
Simba kwenye mapigano anamoyo wakupigana mpaka kifo atakama anajua anashindwa lakini Tiger hanauwezo huo wakupigana kwa muda mrefu
Simba dume ana mane nywele za pale shingoni ile nisilaha tosha kwake inamkinga zidi ya Adui wakati Tiger hana hizo
Simba kwa kimkakati anauwezo mkubwa sana wakumpiga Tiger kuliko mikakati ya Tiger kwakuwa Tiger sio mvumilivu kama simba
Ukitaka kujua Roho ngumu ya simba ..Dume moja la simba lipo tayari kupigana na madume manne akijua kbsa hanauwezo ila analinda Heshima yake mpaka umauti unamkuta ,kwa hiyo simba amepewa sifa za ziada ambazo nitofauti na paka wengine
Pia tambua simba anaona usiku mara nane ya binamu kwa usiku
Tambua kuwa simba Dume anapounguruma sauti yake inasikika mile 8
Tambua pia simba nipaka wanaoishi kaya ambapo wapo mashangazi mabibi mama na watoto mabinamu na Baba zao na ni mwiko mwanaume kumpanda Mama au Dada yake tofauti na paka wengine
Pia tambua simba ndio paka pekee ambao wakiamua leo wale mnyama wanayemtaka wanafanya hivyo mfano tembo twiga nk
Simba jike watoto wao wanaruhusiwa kunyonya kwa mama yoyote wakaya yao na mtoto analindwa na kina mama wote atakama sio wake
Sent using Jamii Forums mobile app
Hello,habari za majukumu wadau,bila shaka mtakuwa mko vyema na mnaendelea kuchukua hatua na tahadhari dhidi ya hili gonjwa dharimu la Covid-19 linalosababishwa na virus hatari wa corona,Mungu awabariki sana!.
Niende moja kwa moja kwenye mada.
Kuna mjadala mahali fulani nimekutana nao kuhusu mnyama SIMBA na TIGER (Chui milia).
Kiukweli kama mnavyofahamu mijadala mizito mara nyingi huwa ina vuta nkuvute,kulingana na tafiti mbalimbali pamoja na Historia kadha wa kadha!,sasa kuna wengine waliosema ya kwamba SIMBA ni hatari zaidi ya Tiger na kuna wengine waliosema Tiger ni hatari zaidi ya Simba,na huo uhatari wao ni pale wanapokutana wao kwa wao.
Wapo waliosema SIMBA kwa uwezo wa nguvu,uwindaji,mapigano basi akikutana na Tiger atapokea kipondo kikali,lakini pia wapo vilevile waliosema kwamba Tiger kwa uwezo,minguvu,uwindaji na mapigano basi akikutana na Simba atampiga mpaka achakae kabisa,na si kuchakaa tu bali pia kuua kabisa.
Mtazamo wako wewe ni upi hapa,hebu lete facts za uhalisia,kiroho na kimwili pia unaweza kuhusisha!!
Tulia hivyo hivyo dawa ikuingie..[emoji382]
Nimependa maelezo haya. Yamechambua vizuri nguvu na udhaifu wa kila mmoja katika aina hizi za paka. Ni kweli Simba hana mzaha linapokuja suala la kupambana. Huwezi ukamtoa nduki kama unavyoweza kufanya kwa Tiger and the like. Utamuua akijilinda huku akitafuta uwezekano wa kukumaliza na wewe
Ila nina swali moja mkuu. Umesema Simba ndio mnyama wa aina ya paka anaewinda kwa pamoja. Je mbwa mwitu hawako kwenye kundi hili maana wao haswaa ndio wawindaji kwa group
Umevuruga tenses ile mbaya. Achana na hiyo lugha mkuu tumia kiswahili tu mbona rahisi.Once they have been subjected in the ring, I bet a tiger will win...
Sent using Jamii Forums mobile app