Simba Vs Kagera Sugar. Yanga Vs Jkt Ruvu tukutane Hapa

Sodoku

JF-Expert Member
Feb 3, 2016
1,261
2,864
Mji wa shinyanga upo katika hali ya shamra shamra za kusbiria mpambano wa leo jioni kati ya Team ya Simba kutoka katika sehemu ya Jiji yenye shamrashamra dar es salaam ambayo asilimia 99 ya watu wanaotoka mikoani lazima wakatembelee huko yaani kariako mtaa wa mnyama aka msimbazi na wana utamu toka mkoa wa watu wanaokula sana senene na ndizi yaani Kagera. Sijajua kama Simba pia huwa wanalamba sukari na je ikitokea hakuna madhara kiafya.
tusubiri dka 90 la mtanange huu nayewaletea taarifa hizi kwa ushirikiano na wapenda michezo wote ni mimi Sodoku pamoja na wewe mdau wa mchezo huu wa kandanda, soka,gozi,kabumbu n.k

Pia jiji la dar baada ya kukoswa koswa huko Mbeya na wajela jela timu ya Yanga inayotokea katika lile bonde lenye kujaa maji na kusababisha maafa mara kwa mara nao watakuwa uwanjani jiji dar huku kwneye wapenzi na mahaba lukuki kwa timu hii dhidi ya timu ya JKT Ruvu katika pambano ambalo Yanga watakuwa na nafasi nzuri ya kurudisha imani kwa washabiki wao hasa baada ya kutetereka kidogo hapo nyuma. Kuna matumaini makubwa kwa Yanga kumgonga mtu mechi hii ya leo kwa mujibu wa habari kutoka ndani zinasema kuwa kila kitu kipo sawa hivyo suala si ushinidi ila ni ushindi wa Bao ngapi. wanachosema wadau kuwa yanga leo inamchapa mtu zaidi ya bao 3 kwa mujibu wa watoa habari za harakati za ushindi kwa timu ya Yanga. pamoja nami Socoku watakuwepo washika dau mbalimbali wa kandanda karibuni sana.
 
Yanga wanaongoza goli moja limefungwa na Simon Msuva dakika ya 12
 
Ndanda na Mtibwa Sugar huko Mtwr, hapatoshi matokeo sina ya huko Shinyanga na Mtwr
 
Yanga leo wanashinda 4 kwa mujibu wa hesabu nlizopewa na wadau. hali kwa upande wa Simba ni ngumu mpaka muda huu. sikuwepo hewani nashukuru WAdau wengine wanaleta updates,
 
ibrahim ajib simba 1 kagera sukari 0 half time
 
Nipo uwanja wa sokoine ,MBEYA CTY vs Prison htm bdo zero .@ viwanja vingine VIP huko
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom