Somo la subira kwako linakupiga chenga sana, ligi ya Ghana inaweza kuwa ni mbovu ila ikatoa mchezaji mzuri, haiwezekani ligi nzima ikawa na wachezaji wote wabovu. Na pia mchezaji anaweza akatoka kwenye ligi bora na asikupe ulichokitaraji kwake. Usajili ni kamari, kwani hujawahi kuona mchezaji kutoka ligi bora na akawa ni mchezaji mkubwa kitakwimu na akafeli kwenye timu nyingine? Jifunze kuwa mvumilivu, mpe mtu muda wa kutosha uwanjani ndipo uje utolee maoni. Mambo kama haya ndio yaliyokuponza kwa Gamondi, minyuzi kibao ya negativity kwake mwisho wa siku ukabaki mdomo wazi.