Simba sports club yatenga bajeti kabambe mashindano ya kimataifa

ZionGate

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
6,345
2,953
Simba imetangaza bajeti ya Sh6.1 bilioni kwa msimu huu 2019/2020 katika kuhakikisha klabu hiyo itatetea ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara na kurudi katika Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Bajeti hiyo ilitajwa kwenye mkutano mkuu wa klabu ya Simba uliofanyika jana jijini Dar es Salaam kwenye ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere.

Katika bajeti hiyo, klabu ya Simba imetenga Sh76.8 Milioni za usajili wa dirisha dogo utakaoanza hivi karibuni.

Mbali na usajili wa dirisha dogo, klabu ya Simba itatumia Sh 4.16 Bilioni kwa ajili ya mishahara ya wachezaji na Sh 408 kwa ajili ya bonusi.

Katika bajeti hivyo, vyanzo vya mapato vitaiingizia klabu ya Simba Sh 5.814 Bilioni ambayo ni pungufu ya Sh373 milioni katika mapato ya klabu.

Chanzo: Mwananchi
 
Umeelewa lakini? Hyo ni ya dirisha dogo msimu huu 2019/20, usajili wa ligi kuu na vikombe vingine vidogo. Sio next season ya 2020/21ya kimataifa hyo bajeti yake bado. Usijitoe ufahamu
kwa hiyo hao wachezaji watakaosajili kwa milioni 70 ndio watashindana na TP MAZEMBE, AK AHLY, WYDAD CASABLANCA? hahaha
 
M. 76.8 si mchezaji mmoja tu, tena wa humu humu bongo! Kwa hela hiyo hata Molinga Ndama Falcao hamumpati!
 
kwa hiyo hao wachezaji watakaosajili kwa milioni 70 ndio watashindana na TP MAZEMBE, AK AHLY, WYDAD CASABLANCA? hahaha
19/20 simba ilishatolewa champions league mkuu, na huo usajili ni dirisha dogo linalo funguliwa mwezi huu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom