Usajili wa Freddy Micheal Koublan, Simba SC tumepigwa!

Mr Alpha

JF-Expert Member
Jul 31, 2018
218
595
Ukweli usemwe tu katika sajili zilizofanyika simba msimu huu Fred Koublan ni usajili mbovu zaidi, ukimuangalia uwezo wake uwanjani ukitoa uwezo wake wa kucheza rafu za ovyo na kupiga maboko anabaki mtupu.

Kipindi cha usajili nilionya simba tabia ya kwenda kuchukua wachezaji kwenye ligi nyepesi hata kama ni wafungaji bora huko, nilisisitiza kwamba kwa hadhi ya simba saiv tuangalie wachezaji ligi kubwa mpaka Ulaya ila inaonekana maskout wa simba walikaza fuvu.

Huu ni usajili uliolenga kupata bidhaa bora kwa bei nafuu, hatimaye tumepigwa.

Alikuwa mfungaji bora kwenye ligi kuu ya Zambia ambayo kiasili ni ligi ya wakulima, kule hata ukimpeleka mzee mwenzangu John Rafael Bocco anaenda kuchukua kiatu cha mfungaji bora kila mwaka mpaka afikishe miaka 60.

Simba kwenye hili mliingizwa chaka, klabu imekuwa na hadhi kubwa lazima isajili kulingana na ukubwa wa timu. Huyu nashauri apelekwe kwa mkopo majin fc au kwa wazee wa ukwaju, timu itafute straika serious wa mabao tuache ubahili kwenye mambo serious.
 
Wee Fred the snake boy haujui? Simba la simba mwamedi
Ni kweli mtaalam, tatizo la Simba maamuzi yana mlolongo mrefu na kuna watu wengi wanakula cha juu hapo, tofauti na Yanga, pesa inatoka kwa Gharib moja kwa moja kwa Engineer kutafuta wachezaji!
 
Ikija suala lausajili kwa Simba kwa miaka hii miwili mitatu imekuwa tatizo kubwa. Ukichukua pesa aliyolipwa Fredy jumlisha na aliyolipwa Jobe unanua mshambuluaji mmoja matata ambaye atafanya kazi vizuri uwanjani. Lakini akli zao za kupenda urahisi ndio zinawaponza upate washambuliaji wawili kwa bei ya mshambuliaji mmoja.

Na wakati wa usajili kulikuwa na tetesi kuwa Manzoki na Adebayor eti wamekatalikwa na Benchika. Manzoki na Adebayor walioisha ni afadhali mara mia mbili kuliko hao wakina Fred na Jobe wanaorukaruka tu uwanjani.
 
Back
Top Bottom