Sielewi ni vigezo gani Raisi anatumia katika kuwachagua mawaziri na hasa wale wanaoshika wizara nyeti kama ya huyu Mama Sophia Simba.
Tokana na kuchambua maelezo ya mama huyu mama inaonesha wazi kwamba hapaswi kuwa katika baraza la mawaziri achilia mbali kuwa mkuu wa wilaya. Kama Raisi anataka kuwashirisha wanawake wa Tanzania katika baraza la mawaziri kuna wanawake wana akili timamu na uwezo wa kuongoza vyema kabisa kuzidi huyu mama.
Kuna wanawake kama Dr Suma Kaare ambaye amebobea vyema kabisa katika fani ya Utawala (hili linaweza kuthibitishwa kama mta - google na kuangalia kazi zake alizofanya), na pia kuna Mwanadada kama Rosemary Mwakitwange ambaye naye amebobea vyema katika masula ya utawala. Kwanini tuwe na mawaziri bomu na vilaza kama Sophia Simba?