SIMBA - Sitamuonea haya fisadi hata aje na bilioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

SIMBA - Sitamuonea haya fisadi hata aje na bilioni

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bongolander, Nov 10, 2009.

 1. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #1
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Na Gladness Theonest

  WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utawala Bora), Bibi Sophia Simba amesema hatamwonea haya fisadi yeyote hata aende na shilingi bilioni moja.

  Pia waziri huyo amewataka wanawake wa Tanzania na Taifa kwa ujumla kumwombea kwa kuwa ni mwanamke pekee aliye katika nafasi ngumu ya kupambana na mafisadi nchini. (
  Kweli mheshimiwa anapambana na mafisadi au anapambana na wanaopambana na ufisadi?)

  Bibi Simba aliyasema hayo mwishoni mwa wiki alipokuwa akifunga Kongamano la Wanawake Waombolezao kitaifa, lililofanyika katika kanisa la Sinza Christiane Centre jijini Dar es Salaam.

  Alisema kuwa fisadi yeyote asitarajie kwenda kwake kwa dhana potofu inayotafsiriwa na wengi kwamba wanawake ni dhaifu na kumpa rushwa ya bilioni moja akitegemea kuwa kesi dhidi yake itasitishwa isiende mahakamani, kwani atakuwa anajidanganya.

  "Wanawake wenzangu nikiwa kama mwanamke na kulingana na wadhifa wangu wa
  kusimamia utawala bora nchini, sitamwonea haya fisadi yeyote hata aje na bilioni moja ili tuyamalize. Hilo kwangu halitawezekana kwani natetea maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla," alisema Bibi Simba.

  Aliwatoa hofu wanawake nchini kuwa serikali inafanya kazi kwa nguvu zake zote katika masuala mbalimbali hasa la kupambana na mafisadi baada ya sheria ya Takukuru kufanyiwa marekebisho.

  Amewataka wanawake wote nchini kuiga mfano wake, kwa kukataa kutoa rushwa sehemu ambazo wanatakiwa wapate haki zao kama hospitalini na mahakamani.

  Waziri huyo aliwaonya viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa kuachana na tabia hiyo ili kulinda amani ya nchi hasa katika kipindi hiki tunachoelekea katika uchaguzi mkuu.

  "Nawaasa wanawake nchini na taifa kwa ujumla kuwapuuza viongozi wa dini ambao wanaingilia mambo ya siasa na dini, bali nawaasa wafanye kazi ya kuongoza watu kiroho na masuala ya siasa waachie wanasiasa," alisema Bibi Simba.

  Aidha amewataka wanawake nchini kutokubweteka kwa kutegemea maendeleo yatawafuata mahali walipo bali pale wanapoona kuwa serikali inatoa fursa ya mikopo kwa wanawake wawe mstari wa mbele kufuatilia nafasi hizo.

  Naye Mchungaji wa Kanisa hilo, Godfrey Emmanuel alisema akina mama na Taifa kwa ujumla hawana budi kusimama imara katika maombi ili kuwaokoa vijana ambao wamechakaa kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya.

  Kongamano hilo liliwakusanya wanawake wapatao 200 kutoka katika mikoa 26 ya Tanzania bara na visiwani na wengine kutoka nchi jirani za Kenya, Uganda na Congo.


  Source: MAJIRA
  Sunday, 27 September 2009 17:15
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Nov 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  anaibeba aibu ya Taifa, anabeba upuuzi wa kiwango cha juu, amekosa adabu kwa taifa, familia yake, chama chake , hata mbele ya Rais, haitaji huruma ila makali ya upanga, huyu uwelewa wako umepofushwa na pesa za mafisadi PAPA, yuko tayari kwa lolote ili mradi anapata mkate wake wa kila siku. Shame on U.
   
 3. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #3
  Nov 10, 2009
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,366
  Likes Received: 7,002
  Trophy Points: 280
  huyo mama sio mzima sasa nadhani ni upotevu wa muda kumjadili mgonjwa
   
 4. s

  shabanimzungu Senior Member

  #4
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 182
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  she is corrupt everyone knows.........she was behind the saga of a plot in Upanga charamee street...she gave it to on AZIM HOODA an Indian..............
   
 5. T

  The Infamous JF-Expert Member

  #5
  Nov 10, 2009
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 719
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  anatapatapa kama mfa maji, sasa anataka wanawake wenzake wamsupport, na mpaka asema I QUIT, Kama randy orton kumbana mbavu mpaka ajione hafai, she doenst know the ruleas of the game.
   
 6. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #6
  Nov 10, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  mimi nafikiri huyu mama si mgonjwa ila ni kama laana flani inamsumbua, maana anavyoropoka, anyoyaongea ni kama kuna kitu kiovu kinamtafuna, au ni ule msemo wa Wahenga kua laana ni hapahapa duniani ?
   
 7. B

  ByaseL JF-Expert Member

  #7
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 2,223
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  This woman is a double talker per excellence! Wakati Bwana Mengi alipotangaza orodha ya mafisadi papa, Sophia Simba alikuwa ni wa kwanza kumbeza Mengi kwamba anawatuhumu watu bila kuwa na ushahidi. Angalia sasa alivyo geuka full circle na kumtuhumu John Malecela kwamba alipata milioni 200 toka kwa mtuhumiwa wa ufisadi Jeetu Patel! Inasikitisha sana kuona baraza la mawaziri la Tanzania lina mtu kama huyu mama zaidi ya miaka 45 ya uhuru! I think this country deserves better than this otherwise we are getting a raw deal from our President. Mbona kuna wanawake wengi na wenye uwezo.
   
 8. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #8
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hawa ndio mafia group ya Tanzania, sababu kubwa za umaskini wa Tanzania ni kuwa na viongozi kama Sophia Simba kwenye madaraka makubwa ya nchi, Mawazo, roho na matendo ni usfisadi uliokubuhu. Mdomoni analaghai kuwa ni mtu safi.

  Kama anasoma JF au mtu wa kumfikishia taarifa ni kuwa Sophia Simba hutufai kabisa, step down ukale fedha yako ya ufisadi uliyokwisha pokea
   
 9. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #9
  Nov 10, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Napenda sana rushwa huyu! Ina maana akipewa 2b yupo tayali lakini sio 1b..Damn!
  Awali ya yote kesha enda Mirembe?
   
 10. vivian

  vivian JF-Expert Member

  #10
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 2, 2009
  Messages: 1,704
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  Hivi jameni Watanzania tunaelekea wapi? Hizi lawama zetu za mafisadi zinaishia humu kwenye JF au zinawagusa wahusika. We need to get rid of these mafisadi!!!! Hivi ile E-mail ya muulizerais@yahoo.com bado inatumika? if yes we need to use it!!!
   
 11. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #11
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,491
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sielewi ni vigezo gani Raisi anatumia katika kuwachagua mawaziri na hasa wale wanaoshika wizara nyeti kama ya huyu Mama Sophia Simba.

  Tokana na kuchambua maelezo ya mama huyu mama inaonesha wazi kwamba hapaswi kuwa katika baraza la mawaziri achilia mbali kuwa mkuu wa wilaya. Kama Raisi anataka kuwashirisha wanawake wa Tanzania katika baraza la mawaziri kuna wanawake wana akili timamu na uwezo wa kuongoza vyema kabisa kuzidi huyu mama.

  Kuna wanawake kama Dr Suma Kaare ambaye amebobea vyema kabisa katika fani ya Utawala (hili linaweza kuthibitishwa kama mta - google na kuangalia kazi zake alizofanya), na pia kuna Mwanadada kama Rosemary Mwakitwange ambaye naye amebobea vyema katika masula ya utawala. Kwanini tuwe na mawaziri bomu na vilaza kama Sophia Simba?
   
 12. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #12
  Nov 10, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,403
  Likes Received: 5,678
  Trophy Points: 280
  Nadhani mwandishi umemfananisha huyo atakuwa idd simba sio sophia simba fisadi halisi lililoitangazia umma hakuna asie fisadi ccm
   
 13. M

  Mmongolilomo Senior Member

  #13
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 135
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Huyu tumpime km alivyoshauri Mzee. Haiwezekani yye awe chanda na pete na ufisadi. Hebu atuletee budget yake ya kupata ukulu wa CWT. Nafikiri wanajaribu kuzua zogo ili mambo yenye muonekano wa maslahi ya jamii yasijadiliwe halafu turudi kutafutana kwa kutiana vidole mtu na mtu. Haki ya nani hata kwenye nchi ya Mabwege hapaswi kuongoza huyu mama
   
 14. M

  Misana Member

  #14
  Nov 10, 2009
  Joined: Feb 19, 2009
  Messages: 33
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Yaani katika mawaziri waliofilisika kisera ambao sijui kwanini rais hawashushi ni huyu Sophia Simba, hivi hana uhusiano na yule Iddi?? maana Simba wamezidi sasa kutajwa kwenye ufisadi (Nicol)
   
 15. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #15
  Nov 10, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mkuu,
  Gazeti la Majira halina habari hiyo kwa namna ulivyoiposti hapa JF,umekusudia kupotosha?
  Kama ulikuwa na maoni,ulikuwa uyaweke chini na uainishe kama ni yako siyo ndani ya stori yenyewe...ambayo source wenyewe hawakuandika hivyo.
   
 16. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #16
  Nov 10, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Amewatia aibu na kuwadhalilisha wanawake wote Tanzania! Hafai kamwe katika nafasi yoyote ya uongozi. Alimfitini Mama Kahama ili aje kutukana wanawake/viongozi wenziwe hadharani kwa kutetea uozo?

  Anataka mwanamke nani amtetee na kwa nafasi ipi? Aliyoidhalilisha hadharani? Hafai kamwe kuwa kiongozi wa ofisi nyeti kama hiyo aondolewe haraka! Shame on her! Halafu eti anasali kwa Rwakatare, unafiki mtupu!
   
 17. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #17
  Nov 10, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  nikiona sura yake mwenyewe naona aibu
   
 18. M

  MzeePunch JF-Expert Member

  #18
  Nov 10, 2009
  Joined: Jun 8, 2009
  Messages: 1,412
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  This woman is a psychiatric case. She surely needs to undergo treatment for her mental illness!
   
 19. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #19
  Nov 10, 2009
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  ......
   
 20. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #20
  Nov 10, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu point taken, hiyo blue in brackets ni swali langu mwenyewe. Thanks for bringing it to my attention
   
Loading...