LIKUD
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 16,452
- 30,865
Katika mechi hiyo ya fainali ya kombe la CAF Afrika. Simba SC walikubali kipigo cha magoli mawili kwa sifuri, kutoka kwa Stella Abidjan ya Ivory Coast. Habari za chini ya kapeti zinadai kuwa, baadhi ya wachezaji wa Simba SC waliuza mechi. Wachezaji wanao daiwa kushiriki katika tukio hilo haramu, ni pamoja na Mohamed Mwameja, George Masatu, na Hussein Masha.
Usiku wa siku hiyo, mchezaji na mnazi wa Simba Sport, mzee mzima Madaraka Suleiman, mzee wa Kiminyio, akiwa pande za Magomeni, alitonywa na mmoja wa mashabiki wa Simba Sport, kuwa amewaona Mwameja, Masatu, Masha et al, pande za Billicanas wakila bata.
Madaraka Suleiman alikasirika sana, akachukua watoto wa kihuni kutoka Kagera, akaenda nao hadi Bills, wao wakawadhibiti Masatu na Masha ( Watoto wa Pamba ), halafu yeye mtu mzima, akampa Mwameja kisago kikali kabla baunsa hawaja enda kuamulia ugomvi...
Azim Dewji anatajwa kuwa chanzo cha kuuzwa mechi hiyo. Ahadi ya KIA moja na fedha taslimu kwa kila mchezaji kama Simba wangeshinda, ilionekana kuwa hasara kubwa sana kwake, so akaona ni bora hizo KIA awape wachezaji wachache.....
Wapenzi wa Simba SC na soka la bongo kwa ujumla, mna maoni gani kuhusu mechi hii?