Mkuu hakuna haja ya kuchukua maneno yako, Simba ilishawahi kuchukua ubingwa bila kufungwa hata mechi moja na hao uliowataja hawakuwepo iweje leo itoke draw na The Express uanze kusema bila Okwi na Mafisango (rip) haiwezi kufanya kitu, nikwambie Okwi ataondoka na marehemu Mafisango Mungu amrehemu hayupo lakini Simba itafanya vizuri, kumbuka mwaka jana tulishiriki Kagame bila ya Okwi lakini tulifika fainali kwa kutufunga goli lililotokana na Uzembe wa beki wenu mliye naye sasa, ukilinganisha kikosi cha mwaka jana na mwaka huu, mwaka huu ni bora zaidi.