SIMBA SC na Malkia wa nyuki!

SIMBA SC na Malkia wa nyuki!

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Posts
5,139
Reaction score
1,153
KLABU ya Simba SC imemuandalia mapokezi ‘baab kubwa’ mfadhili wao wa ziara ya Oman, Mama Rahma Al Kharoos, Malkia wa Nyuki, anayetarajiwa kutua nchini Jumanne.
Ofisa Habari wa Simba SC, Ezekiel Kamwaga ameiambia BIN ZUBEIRY leo mchana kwamba, wanachama na wapenzi wa klabu hiyo wanatakiwa kufika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam siku hiyo kumpokea mfadhili huyo.
“Mama huyu ametusaidia sana kwa kweli, katika kambi yetu ya Oman alitumia zaidi ya Sh. Milioni 80 ambazo ziliisaidia sana timu kwa maandalizi, kwa hiyo tunaomba twende tukampokee siku hiyo, ili kulipa fadhila kwake,”alisema Kamwaga.
Kamwaga alisema kwamba Mama Rahma atakuwa Mkuu wa Msafara wa Simba itakapokwenda nchini Angola kucheza na Libolo ya huko katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu wiki iliyopita, Simba iliweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na hatua hiyo kwa ufadhili kamili wa Malkia wa Nyuki. Hayo yalikuwa majibu kwa wapinzani wao wa jadi, Yanga SC walioweka kambi ya wiki mbili pia nchini Uturuki.


RBP2.jpg


Malkia wa Nyuki
 
huyu si ndo mliki wa afrikan lyon hivi kweli italeta ushindani bongo bana..
 
huyu si ndo mliki wa afrikan lyon hivi kweli italeta ushindani bongo bana..

african lyon hii iliyofungwa 3-0 na simba!basi kazi ipo,yani aliiweka simba oman kujiandaa kucheza na timu yake?!!!!

Simba ilipokua Oman kwa mwaliko wa malkia wa nyuki pichani kushoto..

64279_277753972351445_1728549852_n.jpg
 
Watu wanaochaguliwa kuongoza Simba na Yanga pamoja na wanachama wanaonichagua huwa ni vichekesho kwa sababu wanashindwa kupanga mikakati ya kufanya vilabu vyao vijitegemee na kuanza kuabudu watu wanaotoa pesa kusaidia vilabu hivyo halafu timu zikianza kufanya vibaya wanawageuka na kudai wanarubuni wachezaji wanashindwa nini kujifunza toka vilabu vikubwa vya Hispania Barca na Madrid ambavyo pamoja na kuongozwa na wanachama vimekuwa na mafanikio makubwa ndani na nje ya uwanja
 
She was, so sio sasa na ktk maelezo yake alisema wazi kilichomtoa huko. Pia aliisaidia timu ya Taifa ya Twiga (ingawa nasikia waliopelekwa UK, USA walikuwa njemba flan....lol)....

huyu si ndo mliki wa afrikan lyon hivi kweli italeta ushindani bongo bana..
 
Vipi malkia wa simba koko ashatua?
[TABLE="class: tr-caption-container, align: center"]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="class: tr-caption"]Mfadhili wa Simba SC, Rahma AL Kharoos ‘Malkia wa Nyuki’ (kushoto), akimkabidhi jezi alizotoa kwa ajili ya timu Mwenyekiti wa klabu hiyo, Alhaj Ismail Aden Rage mchana wa leo, makao makuu ya klabu hiyo, Mtaa wa Msimbazi, Dar es Salaam.[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
african lyon hii iliyofungwa 3-0 na simba!basi kazi ipo,yani aliiweka simba oman kujiandaa kucheza na timu yake?!!!!

Simba ilipokua Oman kwa mwaliko wa malkia wa nyuki pichani kushoto..

64279_277753972351445_1728549852_n.jpg
Mpaka atawat.a vidole.
 
Back
Top Bottom