Simba SC kumleta Aristide Bance wa Burkina Faso nchini

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
20,663
20,418
Yule mshambuliaji nyota wa timu ya taifa ya Burkina Faso, Aristides Bance, huenda akatua nchini kuikabili Simba SC katika kombe la Shirikisho Afrika iwapo mambo yatakwenda vyema kama yalivyoanza. Simba imeirarua Gendarmarie ya Djibout kwa mabao 4-0 katika raundi ya awali, huku Al Masry imeirarua Green Buffaloes ya Zambia kwa mabao 4-0 pia. Iwapo Simba na Al Masry zitavuka na kuingia raundi ya Kwanza, basi zitakutana jijini Dar katika mchezo wa kwanza

Aristide Bance anaichezea timu hiyo ya Al Masry, na jana alitupia bao moja kati ya manne ambayo timu yake ilishinda. Hadi sasa nyota huyo yumo katika kikosi cha Burkina Faso, taifa ambalo limesumbua sana katika mechi za hivi karibuni na ilibaki kidogo tu wakate tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2014 kama sio kushindwa kwa goli la ugenini dhidi ya Algeria katika mchezo wa mwisho wa kukata tiketi hiyo

Mshambuliaji huyo amekwishacheza katika nchi kadhaa za Ulaya ikiwemo Finland. Pia alikuwa akikipiga ASEC Mimosas kabla ya kujiunga na Al Masry, na hadi sasa amekwishatupia mabao 21 katika mechi 67 alizoichezea nchi yake Burkina Faso, na amekwishatupia mabao 5 kati ya mechi 10 alizoichezea klabu yake ya sasa Al Masry katika ligi ya Misri.

Mwaka jana katika AFCON, aliingia na kubadili mchezo kabisa na ndani ya dakika 15 Burkina faso ikapata mabao mawili dhidi ya Tunisia

Simba waanze kumuangalia jamaa
 
bance.png
 
Back
Top Bottom