Simba Sc: Hatutaruhusu shabiki wa Yanga Sc kuingia uwanjani kushabikia wageni

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,879
Klabu ya Soka ya Simba imesema haitaruhusu Shabiki wa Klabu ya Yanga kuingia katika mchezo wao wa mkondo wa pili wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United mchezo utakaopigwa katika dimba la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Klabu hiyo, Haji Manara amesema watazuia kuingia shabiki wa timu hiyo kutokana na mechi hiyo ni ya kwao.

“Mechi hii ni ya kwetu sio ya hisani, kama unataka kuzomea tulia nyumbani au ishia pale Mianzini au Keko”, amesema Manara.

Manara amesema endapo mashabiki hao wataingia katika uwanja huo, amewaasa mashabiki wa Simba SC wasiwafanyie vurugu na kuwapiga, amewaomba Mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo ili kuishangalia timu hiyo.

“Plateau United sio timu ya kubeza, tunataka tucheze Soka tuwaburudisha Wana Simba na kuwafunga katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, tutumie vizuri nafasi ya CAF kuruhusu Mashabiki Elfu 30 kuingia Uwanjani”, ameeleza Manara.

Simba SC itarudiana na Plateau United Desemba 5, 2020 katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam baada ya mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa mjini Jos nchini Nigeria kuondoka na ushindi wa bao 1-0.
 
Safi, ila utopolo tulivyo na akili mbovu tutavaa majezi feki ya buku 2, yaliyofwetuliwa shimoni ya Plateau, tukijifanya ni mashabiki wao!
....ila naomba muuzie tiketi wenye zile kadi za simba tu najua wapo zaidi ya million hivyo 30k ni chap tu!
 
Safi, ila utopolo tulivyo na akili mbovu tutavaa majezi feki ya buku 2, yaliyofwetuliwa shimoni ya Plateau, tukijifanya ni mashabiki wao!
....ila naomba muuzie tiketi wenye zile kadi za simba tu najua wapo zaidi ya million hivyo 30k ni chap tu!
Kwenye mpira hakuna usengelema Kama huu
Mimi Yanga niitaenda na ole wake nguchiro yeyote wa Simba anizuie lazima nizae nae
 
Kwenye mpira hakuna usengelema Kama huu
Mimi Yanga niitaenda na ole wake nguchiro yeyote wa Simba anizuie lazima nizae nae
Subiri yanga ikicheza kimataifa utaingia. Mechi hii ni kwa mashabiki wa simba tu. Wapinzani mtashangilia kupitia azam tv😳 tabia zenu za kushangilia timu pinzani ndo zinawaponza
 
Kuishi kwingi kuona wengi!Mkiambiwa hamna msemaji man zezeta mnabisha.Huyu mtu anaangalia ligi za nchi nyingne kwali?Anajua kitu kinaitwa CLOBAL SOCCER PSYCHOLOGY?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom